Mh Samuel Sitta apewa cheo cha Mwizukulu Mkulu (Mjukuu mkubwa) wa Utemi wa Unyanyembe!

Mh Samuel Sitta apewa cheo cha Mwizukulu Mkulu (Mjukuu mkubwa) wa Utemi wa Unyanyembe!

Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira akiwatambikia Mh Magreth Sitta na Mh Samuel Sitta ambaye ni binamu yake kabla hajatangaza nia ya kugombea urais.

Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira leo hii asubuhi alimpa cheo cha Mwizukulu mkulu Mh Samuel Sitta katika kutambua safari yake ya kukiomba chama chake cha CCM kimpe ridhaa ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.
Mh Samuel Sitta akiwa na mkewe Mh Magreth Sitta wakisubiri kutambikiwa.
Mtemi wa Unyanyembe Msgata Fundikira akisisitiza jambo katika hafla fupi ya kumpa cheo Mh Samuel Sitta
Mtemi Msagata akimvika mgololoMh Sitta

Mtemi Msagata Fundikira, Mh Rageh, Mh Samuel Sitta na Mlinzi Mh Sitta wakitokea sehemu maalumu palipofanyika tambiko.
Picha na Habari na Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE