Kijji cha Amani kinavyoonekana |
Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya.
Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.
Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa |
Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa |
Hpa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro |
Job DONE |
Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini |
Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa |
Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho |
Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo. |
Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa kunguni na wadudu wengine. |
Rundo la mahindi likiwa limotolewa nje kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni nani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa. |
Baadhi ya panya waliokutwa ndani ya chumba cha mkazi mmoja wa kjijini hapo leo. |
Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni |
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid Mkala Fundikira kushoto akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma. |
Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa. |
Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji |
Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita kiasi. |