Hatimaye wakazi wa kijiji cha Amani Tabora usiku wa leo watalala bila kero ya kunguni!

Hatimaye wakazi wa kijiji cha Amani Tabora usiku wa leo watalala bila kero ya kunguni!

Kijji cha Amani kinavyoonekana
Taasisi ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal Nsyepa General Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za jijini Dar es Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu kama kunguni na wengineo katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa Tabora. Hatua hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye uathirika wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia wakazi wa hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine wajengewe vyoo zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye hali ya kutumika, huku vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka. Akiongea na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo alisema"kwa kweli tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada huu, kwani tumekuwa tukilala kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala kwa raha kama watu wengine" pia aliongeza "Ila tu jamani msituchoke, bado tunakumbushia ombi la kujengewa vyoo zaidi kwani idadi yetu na ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni changamoto, lakini pia tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na muuguzi wapate mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"

Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.

Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya. 

Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.

Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa

Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa
Hpa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro

Job DONE

Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini


Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa
Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho
Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo.

Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa  kunguni na wadudu wengine.
Rundo la mahindi likiwa limotolewa nje kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni nani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa.
Baadhi ya panya waliokutwa ndani ya chumba cha mkazi mmoja wa kjijini hapo leo.
Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid Mkala Fundikira kushoto akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma.

Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa.
Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji
Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita  kiasi.
Habari na picha kwa hisani ya TBN Central zone!