Mh Aden Rageh kushoto na Bandora Mirambo wakifuatilia mkutano.
Makada wa CCM Wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM Tabora mjini leo hii mchana walijinadi kwa wapiga kura wao wa kata ya Itetemia, ambao wakiungana na wengine kwa jimbo la Tabora mjini watapiga kura siku ya tar 1/8/2015kumchagua mmoja wao ili aikiwakilishe chama hicho kayika uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.
Wagombea hao ambao kila mmoja wao alijieleza mbele ya wajumbe hao kwa dakika 5 walitoa maelezo yao mbele ya wajumbe ya kuwa wakichaguliwa wataboresha hali za maisha, uchumi, elimu na kilimo.
Siku ya kesho wagombea hao wataelekea Ntalikwa ambako pia watajinadi kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu katika kuelekea kura za maoni mapema mwezi ujao.
|
Bandora Mirambo akibadilishana mawazo na mgombea mwenzie Emmanuel Mwakasaka mara baada ya kujinadi. |
Mwenyekiti wa CCM kata ya Itetemia (Kushoto) Rashid Kamanda Tall(kiongozi wa msafara) na katibu wa CCM kata ya Itetemia. |
Wajumbe |
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wilaya ambao watapiga kura tarehe 1/8/2015 kumchagua mgombea wa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao. |
Bw Bandora Salum Mirambo. |
Bw Emmanuel Mwakasaka |
Amon Mkoga. |
Mh Aden Rageh. |
Bw William Masubi Chimaguli. |
Ramadhani Mauli Mkangara mgombea akijinadi na kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum. |
Viongozi wa mkutano toka kushoto ni Rashid Tall, Ali Kazikupenda na Mohamed Kazete. |
Mkaziwa Kipalapala Thomas Mwiniko aliyeuliza baadhi ya maswali kwa wagombea. |
Amon Mkoga kushoto na Salum Mkangara wakifuatilia mkutano |
Habari na picha na mkalamatuio blog