Breaking news! Mwanamuziki wa Taarabu Nyawana Fundikira afariki dunia mchana huu!
Mama Nyawana enzi za uhai wake
Mwanamuziki wa muziki wa taarab Nyawana Isale au Maarufu Nyawana Fundikira aka Mamaa Matashtiti amefariki leo hii mchana jijini Dar es Salaam alipokuwa akikimbizwa hospitalini baada kuzidiwa Inafahamika kuwa ameugua Malaria kwa siku kadhaa, kwa habari zaidi kuhusu kifo chake na mazishi tutaendela kujuzana humu na kwingineko. RIP mwanawane Nyawana! Picha kwa hisani ya taarabuzetublog!