Shabiki wa Chelsea mpigania haki za binadamu atuhumiwa kwa ubaguzi Paris!

Shabiki wa Chelsea mpigania haki za binadamu atuhumiwa kwa ubaguzi Paris!


Bw Richard Barklie akihutubia kongamano la haki za binadamu nchini India
Imebainika kuwa askari polisi wa zamani na mpigania haki za binadamu Bw Richard Barklie ni mmoja kati ya mashabiki watatu wa Chelsea waliomzuia mtu mweusi Suleyman Syla kupanda treni kwa kuwa ni mweusi. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya mchezo wa ubingwa wa ulaya (UEFA Champions league) kati ya Paris Saint Germain(PSG) na Chelsea uliochezwa jijini Paris Ufaransa jumanne iliyopita. Bwana Barklie alibainika baada ya Metropolitan Police ya Uingereza kuonesha picha za washukiwa wa tukio hilo zilizokamatwa na kamera za cctv za stesheni hiyo ya treni za ardhini maarufu kama METRO.

Bw Barklie ambaye pia ni mkurugenzi katika taasisi ya hiari mjini Belfast Northen Ireland ya WAVE TRAUMA CENTRE ameshasimamishwa kazi na taasisi hiyo kupisha upelelezi.

Barklie ambaye ni mmiliki wa tiketi ya msimu ya Chelsea fc akiwa na wenziwe watatu walimsukuma Bw Syla asiingie ndani ya treni (METRO) huku wakiimba (we are racists we are racists this is how we ike it) Sisis ni wabaguzi na hivi ndivyo tupendavyo. Police nchini England imeshawatambua watuhumiwa lakini hakuna aliyekamatwa mpaka sasa, Idara hiyo ya polisi imeeleza upelelezi utaingia hatua inayofuata.

Hata hivyo kupitia mwanasheria wake Bw Barklie amakanusha kuhusika na vitendo vya kibaguzi vilivyotokea siku hiyo lakini anakiri kuwepo eneo la tukio, na amedhamiria kujisafisha.

Metropolitan police pia imeeleza haiwezi kukamata mtu kwa makosa aliyoyafanya nje ya Uingereza, kwa mawazo yangu basi bila shaka Polisi ya Paris itabidi iiombe serikali ya England washukiwa wapelekwe Ufaransa kwa mahojiano na pengine kushtakiwa iwapo itaonekana wana kesi ya kujibu.

Kilabu cha Chelsea kupitia meneja wa timu Jose Mourinho kimeelzwa kusikitishwa na tukio hilo na kuwa kitawafungia wote watakapatikana na kesi ya kujibu. Taarifa ya msemaji wa kilabu hicho cha jijini London ameelza kuwa mmiliki wa timu hiyo Bw Roman Abramovich ametiwa kinyaa na kitendo hicho. Pia kilabu hicho kimeshamkaribisha Bw Syla London katika mchezo wa marudiano kati ya timu hizo mbili.
Picha ya Bw Barklie iliyochukuliwa toka cctv.
Hotuba India
Barklie akiwa katika harakati za haki za binadamu barani Afrika.
Bw Suleyman Syla ndiye mhanga wa tukio la kibaguzi lililotokea stesheni ya treni za chini ya ardhi (METRO) jijini Paris Ufaransa.
Picha na habari kwa hisani ya mailonline/AFP/Metropolitan police