Azam yailaza Rhino Fc!

Azam yailaza Rhino Fc!

Timu ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam leo hii imeilaza timu ya Rhino Rangers ya mjini Tabora kwa goli 2 kwa sifuri kwa magoli ya Gaudence Mwaikimba kwa shuti kali lililopita kulia mwa lango la kipa wa Rhino Fc mnamo dakika ya 56,baada ya kazi nzuri ya wachezaji wa Azam Fc upande wa kulia mwa uwanja.
Baadhi ya maelfu  ya mashabiki wa soka mjini Tabora wakifuatilia kwa makini mchezo kati ya Azam Fc na Rhino Rangers uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
Huku Rhino Rangers ikijaribu kusawazisha bao hilo la Mwaikimba ilijikuta ikongezwa bao la pili kupitia mchezaji wa kiungo Seif Kalihe mnamo dakika ya 77 ya mchezo huo uliodorora. Timu ya Rhino Rangers itabidi ijilaumu kwa kutocheza kwa kujituma kama ambavyo ilicheza katika mchezo dhidi ya Simba ambapo waliweza kuibana Simba na kutoka nayo sare ya goli 2-2. Mchezo ujao wa Rhino utakuwa dhidi ya JKT Oljoro wikiendi ijayo mjini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.   
Patashika langoni mwa Azam
Basi la wachezaji wa Rhino Rangers likitoka uwanjani baada ya mchezo wao dhidi ya Azam Fc kwisha.