Valencia ndiye mchezaji mwenye kasi kuliko wote duniani!

Valencia ndiye mchezaji mwenye kasi kuliko wote duniani!

Nyota wa Arsenal Theo Walcot amekuwa akifikiriwa ndiye mcheza soka mwenye kasi kuliko wote duniani, lakini imebainishwa kuwa kiungo wa timu ya Man United Antonio Valencia ametajwa na FIFA kuwa ndiye mcheza soka mwenye kasi kuliko wote ulimwenguni, inasadikika kuwa kiungo huyo anakadiriwa kufikia mwendo kasi wa kilometa 22 kwa saa. Na orodha ya wachezaji na kasi ni kama ifuatavyo hapo chini.
1. Antonio Valencia km 22 (kwa saa) Man united
2. Gareth Bale km 21.56 (kwa saa) Real Madrid
Orodha hiyo pia imeonesha kuwa Aaron Lenon wa Totenham Hotspurs anashika nafasi ya tatu na ya nne imechukuliwa na Christiano Ronaldo huku Lionel Messi akiangukia nafasi ya sita.
Habari na picha kwa hisani ya mtandao wa the express