Hamisi Dakota |
Awali Dakota aliwaita jukwaani Mkala Fundikira na Adam Fundikira na kusema "Nimewaita hawa hapa jukwaani kwa kuwa hawa wanatoka katika familia ya ki chifu ya Fundikira ambayo ndio ilikuwa mtawala wa mkoa huu kabla ya uhuru ingawa palikuwa na utawala wa kikoloni kama wasimamizi, hivyo nimewaita kwa heshima kwani usipowaheshimu watemi(Machifu) unaweza ukashitukia vyombo vinaungua bila ya sababu za msingi. Aliwahi kuja Totoo Ze Bingwa akaunguza vyombo hapa Tabora, ni vema tunapoenda katika miji ya watu tupige hodi" Dakota aliyesema hayo usiku wa alhamisi ya tarehe 2 April2013 ambapo bendi ya Mapacha watatu ilitumbuiza katika ukumbi wa Frankman Palace.
Dakota akisistiza jambo. |
Adfun Smiler na Mratibu wa Miss Tabora 2013 |
Mkala Fundikira na Hamisi Dakota |