Nina asili ya Tabora! - Ommy Dimpoz!
Msanii anayekuja juu kwa kasi kama moshi wa kifuu Ommy Dimpoz ambaye hivi juzi alihojiwa na kituo maarufu cha redio mkoani Tabora CG fm 89.5, alisema pamoja na kuimba katika wimbo wa wasanii wa Kigoma lakini yeye pia ana asili ya Tabora kwa kuwa Mama yake mzazi aliziliwa na kukulia hapa kabla ya kuhamia Dar, na pia aliweka wazi kuwa baba yake ndio mtu wa Kigoma. Ommy Aliyekuwa akihojiwa na Ibrahim Haruna na DJ Kessy wa CGfm 89.5 ambao ni wadhamini wa Redds Misss Tabora 2013.