Shinji Kagawa acheza na moto Old Trafford

Shinji Kagawa acheza na moto Old Trafford

Moyes akiwa na Shinji Kagawa ziarani Japan kiangazi hiki.
Mshambuliaji mchezeshaji wa ki Japan anayechezea kilabu cha Man United Shinji Kagawa ameeleza kuchukizwa kwake na kutopangwa na David Moyes katika kikosi cha kwanza cha Man United tangu msimu huu umeanza aliongea na vyombo vya habari baada ya kuisaidia timu yake ya taifa Japan kuishinda Ghana kwa goli 3-1 ambapo yeye alifunga goli moja. Aliulizwa kwa nini hachezi mechi za Man united na waandishi wa habari naye alijibu" Jibu la swali hilo analijua David Moyes ni vema mmuulize yeye"
Kagawa: Anafikiri anapaswa kuwemo katika kikosi cha kwanza Man united ingawa alichelewa kuripoti mazoezini.
Kutokana na kuwa na mechi za timu yake ya taifa katika kombe la shirikisho alizocheza Kagawa alijikuta akicheza mechi moja tu ya maandalizi ya msimu mpya ambapo pia alipewa mapumziko ya wiki mbili zaidi ya wenzie na hivyo kumfanya kuwa asiye na utayari wa kuanza msimu.

Kwa maoni yangu David Moyes anatakiwa amkumbushe Kagawa kuwa Man united ni kilabu kilichopata mafanikio makubwa huku kikiwa na usiri mkubwa ndani ya kilabu hicho, na sijapata kumsikia mchezaji akilalamika katika vyombo vya habari juu yakutopangwa na Sir Alex Ferguson kwa kuwa hakuruhusu mchezaji yeyote kuongea na vyombo vya habari hasa kwa habari hasi kama hiyo. Sir Alex amepata kusema mara nyingi kuwa meneja ni lazima awe ndio mhimili wa kila kitu katika klabu na meneja asiruhusu mchezaji kujiona mkubwa kuliko kikosi kizima, ndio maana nasema Moyes amkumbushe Kagawa jukumu lake.