Uwanja wa the Emirate London ya kaskazini |
Dangote ambaye ana pesa nyingi kuliko mmiliki wa sasa wa Arsenal Stan Kroenker mwenye 67% ya hisa na mwanahisa mwingine Mrusi Alisher Usmanov.
Aliko Dangote(58) bilionea m Nigeria, mwenye mapenzi na Arsenal Football club ya jijini London, England. |
Lakini Dangote alibainisha kuwa mpango wa kununua kilabu hicho maarufu kama the gunners haupo hivi karibuni, alisema "Tunawekeza kiasi cha dola bilioni 16 katika miradi tofauti miaka michache ijayo, kwani nataka kupeleka biashara zangu katika kiwango fulani, na nikimaliza hilo ndipo ofa ya kuinunua Arsenal itafuata" Pia Dangote amepata kukaririwa akisema kocha Arsene Wenger anatakiwa kubadili mfumo wa timu yake. Arsenal imekuwa na sifa ya kutandaza soka safi na la kuvutia lakini wameshindwa kushinda ubingwa wa England kwa karibu miaka 11 na kabla ya mwaka jana ambapo walishinda kombe la FA walikuwa hawajashinda kikombe chochote kwa miaka 9.
Mwanahisa mkuu wa Kilabu hicho Bw Stan Kroenker amenunua hisa zaidi hivi karibuni na haielekei ana mpango wa kukiuza kilabu hicho katika miaka ya karibuni.
Dangote pia anajenga kiwanda cha saruji mjini Mtwara ambapo wakazi wengi wa mkoa huo watapata ajira za muda na za kudumu.
Stan Kroenker (67) bilionea Mmarekani ndiye mbia mwenye hisa kubwa katika kilabu cha Arsenal kwa sasa |
Kocha Wenger amatakiwa kubadili mfumo wa timu yake na Dangote |