Bandora uso kwa uso na Mh Aden Rageh ubunge Tabora mjini!

Bandora uso kwa uso na Mh Aden Rageh ubunge Tabora mjini!

Bandora Salum Mirambo akiwasilia katika ofisi za CCM wilaya ya Tabora kuchukua fomu za ubunge wa Tabora mjini
Wagombea ubunge wa jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh Aden Rageh na Bandora Mirambo leo 
hii walikutana uso kwa uso walipofika ofisi za CCM wilaya kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge wa wa Tabora mjini. Wote wawili katika kuonesha siasa si chuki wala ugomvi walilakiana na kusalimiana kwa uzuri kabisa.


Wawania kuteuliwa na CCM wakisabahiana
 Mh Aden Rageh ndiye mbunge aliyemaliza muda wa ubunge wa Tabora mijni ambapo alishinda ubunge huo mwaka 2010 kwa kumuangusha  kwenye kura za maoni ndani ya CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2005 marehemu Siraju Kaboyonga ambaye naye alimshinda Henry Mgombelo mwaka 2005 aliyekuwa mbunge mwaka 2000 . Hali hii imeonesha kuwa wapiga kura wa Tabora wamekuwa na tabia ya kutorudisha mbunge katika kiti hicho kwa mara ya pili mfululizo, Mh Rageh ambaye alipata kuwa mwenyekiti kilabu cha Simba cha jijini Dar bila shaka atakuwa na kibarua kigumu cha kuuvunja mwiko huo.

Bandora Mirambo ni mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Salu Security yenye makao yake makuu mjini Sinyanga na matawi kadhaa mikoa ya kanda ya ziwa.

Tabasamu kubwa!