mkalamatukio

Nikon Hd SLR camera inauzwa!

Mtazamo wake kwa juu.
  • Extensive in-camera retouching including raw development and straightening
  • 12.9 megapixel DX-format CMOS sensor (effective pixels: 12.3 million)
  • 3.0-inch 920,000 pixel (VGA x 3 colors) TFT-LCD (same as D3 and D300)
  • Live View with contrast-detect AF, face detection
  • Image sensor cleaning (sensor shake)
  • Illuminated focus points
  • Movie capture at up to 1280 x 720 (720p) 24 fps with mono sound
  • IS0 200-3200 range (100-6400 expanded)
  • 4.5 frames per second continuous shooting (buffer: 7 RAW, 25 JPEG fine, 100 JPEG Normal)
  • Expeed image processing engine
  • 3D tracking AF (11 point)
  • Short startup time, viewfinder blackout and shutter lag
  • Slightly improved viewfinder (96% frame coverage)
  • Improved user interface
  • New optional compact GPS unit (fits on hot shoe)
  • Same battery and vertical grip as D80
  • Vignetting control in-camera
  • 72 thumbnail and calendar view in playback
Kwa mbele D90 inavyoonekana

Kwa nyuma ambako pana settings zote


For more details please call 
0754 666 620

Valencia ndiye mchezaji mwenye kasi kuliko wote duniani!

Nyota wa Arsenal Theo Walcot amekuwa akifikiriwa ndiye mcheza soka mwenye kasi kuliko wote duniani, lakini imebainishwa kuwa kiungo wa timu ya Man United Antonio Valencia ametajwa na FIFA kuwa ndiye mcheza soka mwenye kasi kuliko wote ulimwenguni, inasadikika kuwa kiungo huyo anakadiriwa kufikia mwendo kasi wa kilometa 22 kwa saa. Na orodha ya wachezaji na kasi ni kama ifuatavyo hapo chini.
1. Antonio Valencia km 22 (kwa saa) Man united
2. Gareth Bale km 21.56 (kwa saa) Real Madrid
Orodha hiyo pia imeonesha kuwa Aaron Lenon wa Totenham Hotspurs anashika nafasi ya tatu na ya nne imechukuliwa na Christiano Ronaldo huku Lionel Messi akiangukia nafasi ya sita.
Habari na picha kwa hisani ya mtandao wa the express

BOB JUNIOR | MASAI NYOTAMBOFU | SAMIR NA MASELE CHA POMBE KUBURUDISHA SIKUKUU YA EID EL HAJ TABORA


Bob junior aka Mr Chocolate Flavor
BOB JUNIOR | MR CHOCOLATE | RAIS WA MASHAROBARO | MTAALAMU WA VIOUNO
NI MSANII NA PRODUCER ANAYETAMBA NA VIBAO KAMA KIMBIJI, ANDAZI  NA NYINGINE NYINGI, KWA MARA YA KWANZA ATADONDOSHA BONGE MOJA LA SHOO SIKU YA EID EL HAJ NDANI YA UWANJA WA ALLY HASSAN MWINYI KWA KIINGILIO CHA 3000 WAKUBWA NA 1000 WATOTO, KUANZIA SAA 8 MCHANA NA USIKU ITAKUWA KATIKA UKUMBI WA THEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU) KWA SH 5,000/= NA SH 10,000/= TU KWA V.I.P | NI TAREHE 15 OKTOBA, 2013
 MASAI NYOTAMBOFU MWANAMZIKI NA MSANII WA VICHEKESHO ANAYETAMBA KATIKA VITUKO SHOO YA CHANEL TEN, ATACHEKESHA NA KUIMBA NYIMBO ZAKE MBILI, HAPATATOSHA SIKU HIYO
 KUTANA NA MASELE CHA POMBE | MCHEKESHAJI MAHIRI WA VIYUKO SHOO, NJOO KUTANA NA SWAGA ZA KULEWA BILA KUNYWA LIVE KATIKA MAJUKWAA MAWILI MCHANA NDANI YA ALLY HASSAN MWINYI KWA KIINGILIO CHA SH 3,000/= WAKUBWA NA 1000/= WATOTO MA USIKU NDANI YA UKUMBI WA TEKU (DIAMOND TALKIES) KWA SH 5000/= NA 10,000/= V.I.P
NA SAMIR KUHAMISHIA BAHARI YAKE NA MCHEZO WA KINYULINYULI NDANI YA ARDHI YA WANYAMWEZI.
------------
SHOO INAENDA KWA UDHAMINI WA GONALA PHAMACY | FRANKMAN PALACE HOTEL | NBS CLASSIC (KAMPUNI YA USAFIRI) | CLOUDS FM NA CG FM 89.5
-------------

Bob Junior kuburudisha wakazi wa Tabora siku ya Eid El Haj!

Bob Junior
Msanii machachari wa muziki wa kizazi kipya Bob Junior aka Sharobaro aka Rais wa wasafi hatimaye kwa mara ya kwanza atafanya onesho la kukata na shoka mjini Tabora katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Haj litakalofanyika Jumanne ya tarehe 15/10/2013. Akithibitisha hilo mratibu wa onesho hilo kubwa Mkala Fundikira ambalo litawaleta pia wasanii wa vichekesho Masele cha pombe na Masai nyota mbofu wa kipindi cha ucheshi cha Vituko show alisema kila kitu kipo tayari kwa sasa yeye na jopo la waandaaji wenzie wanamalizia vitu vidogo vidogo tu na kuisubiria siku ya onesho. Pia Mkala alisema kuna msanii mwingine wa Bongo Flava ataungana na hao ambao amewataja kuja Tabora kumwaga burudani atamtaja siku zijazo.

Washiriki wa Miss TPSC Tabora watembelea Cg fm

Nice Mbelwa(Meneja vipindi)akiwatambulisha washiriki wa Miss TPSC 2013 kwa mhariri wa habari wa Cg fm 89.5 Bw Titus Filipo.
Washiriki wa shindano la Miss TPSC 2013 jana walitembelea kituo cha  redio cha CG fm 89.5 ambapo walioneshwa jinsi ambavyo kituo hicho kinavyofanya kazi, vile vile walitembelea chumba cha habari, cumba cha utayarishaji na studio ambako walihojiwa na Nice Mbelwa na Vivian Pyuza.
Mkurugenzi wa Cg fm 89.5 Bw George Charles ambaye pia ni injinia wa kituo hicho cha redio.
Mtangazaji Vivian Pyuza akiwa studioni tayari kwa mahojiano na washiriki wa Miss TPSC

warembo pose!

Mratibu wa shindano la Miss TPSC 2013

Mmetuona? Joyce Lilian na Perpetua.


Paulina akijibu moja ya maswali toka kwa Nice Mbelwa na Vian Pyuza wa Cg fm 89.5 jana

Mshiriki Lulu akiwekwa mtu kati kwa maswali na watangazaji wa Cg fm 89.5

Mshiriki Miss Saada akicheka baada ya kuulizwa swali la kizushi

MSANII: ALLY NIPISHE amepania kuwaona live mashabiki wake wa Tabora

MSANII: ALLY NIPISHE
Msanii wa kizazi kipya anayetamba na vibao kama Ntalila, Nipulika, Daima na milele, Binadam (aliyoimba na AT) na kibao kikali kinachotamba hivi sasa cha MY amepania kuwaona live mashabiki wake wa Tabora huku akimtafuta "MY" siku ya shoo kali ya kumsaka Mrembo wa Chuo Cha Utumishi wa UMMA Tawi la Tabora.

NI TAREHE 27-09-2013
UKUMBI:  TPSC (UHAZILI )FUNCTION HALL
MUDA: MBILI USIKU MPAKA CHWEE
ALLY BAUCHA | PRODUCER, ACTOR NA DANCER
HAPATATOSHA JUKWAA LITAKAPOVAMIWA TENA KWA SUPRISE AMBAYO KILA ATAKAYE KUWEPO ATAJIVUNIA KUMWONA MSANII WA TOFAUTI SANA BONGO ANAYEBEBA SIFA YA NGULI MOJAWAPO NA MFALME WA DUNIA. 
#SUPRISE HAISEMWI WAZI FIKA JIONEE#
BAUCHA ATAKIPIGA KIBAO CHAKE KIPYA KWA MARA YA KWANZA TABORA HUKU AKIKELESHA MASHABIKI KWA KIBAO CHAKE MAARUFU CHA "KELELE"
----------
WADHAMINI:
------
GONALA PHAMACY,SCREENMASTERS,SALUM MCHELE ELECTRONICS|
 FRADO BUSINESS CARE| ALOY SON BLOG| GAMALO PUB|
ROYAL PRODUCTIONS| MKWABI ENTERPRISES LIMITED| MSWAPE ALUMINIUM WORKS| MILLARDAYO.COM|
CG FM 89.5| TABORA REST HOUSE| NBS CLASSIC| CLOUDS FM|
NDIBS COLLECTION| HOLIDAY PARK.
---------

Shinji Kagawa acheza na moto Old Trafford

Moyes akiwa na Shinji Kagawa ziarani Japan kiangazi hiki.
Mshambuliaji mchezeshaji wa ki Japan anayechezea kilabu cha Man United Shinji Kagawa ameeleza kuchukizwa kwake na kutopangwa na David Moyes katika kikosi cha kwanza cha Man United tangu msimu huu umeanza aliongea na vyombo vya habari baada ya kuisaidia timu yake ya taifa Japan kuishinda Ghana kwa goli 3-1 ambapo yeye alifunga goli moja. Aliulizwa kwa nini hachezi mechi za Man united na waandishi wa habari naye alijibu" Jibu la swali hilo analijua David Moyes ni vema mmuulize yeye"
Kagawa: Anafikiri anapaswa kuwemo katika kikosi cha kwanza Man united ingawa alichelewa kuripoti mazoezini.
Kutokana na kuwa na mechi za timu yake ya taifa katika kombe la shirikisho alizocheza Kagawa alijikuta akicheza mechi moja tu ya maandalizi ya msimu mpya ambapo pia alipewa mapumziko ya wiki mbili zaidi ya wenzie na hivyo kumfanya kuwa asiye na utayari wa kuanza msimu.

Kwa maoni yangu David Moyes anatakiwa amkumbushe Kagawa kuwa Man united ni kilabu kilichopata mafanikio makubwa huku kikiwa na usiri mkubwa ndani ya kilabu hicho, na sijapata kumsikia mchezaji akilalamika katika vyombo vya habari juu yakutopangwa na Sir Alex Ferguson kwa kuwa hakuruhusu mchezaji yeyote kuongea na vyombo vya habari hasa kwa habari hasi kama hiyo. Sir Alex amepata kusema mara nyingi kuwa meneja ni lazima awe ndio mhimili wa kila kitu katika klabu na meneja asiruhusu mchezaji kujiona mkubwa kuliko kikosi kizima, ndio maana nasema Moyes amkumbushe Kagawa jukumu lake.