Kadri muda uendavyo ndivyo watu wamezidi kufika ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo ya Gongoni, Tabora mjini. Hata hivyo mwili wake umechelewa kidogo kuwasili mjini hapa lakini watu wameendelea kujazana wakikaa juani bila taabu yeyote. Hii ni ishara kuwa watu wa Tabora walimkubali sana Nyawana ambaye wao walipenda kumwita Mamaa Nyawana au Jembe! kwani watu wapatao elfu moja wamejitokeza kushuhudia au kutoa heshima za mwisho kwa Nyawana.
Sheikh akitoa mawaidha mawili matatu kwa wahudhuriaji |