Msanii mkali wa Bongo Flava Belle9 atakuwa ni mmoja wa wasanii watatu watakaoburudisha Tamasha la Club Royal Funga Mwaka Bash litakalofanyika mjini Tabora katika ukumbi maarufu wa New Royal Garden. Akiongelea tamasha hilo mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo Mashaka Chura aka Mzee wa maini na Figo mkurugenzi wa Chura Fashion alisema maandalizi yamekamilika, wapenzi wa muziki wa Bongo Flava wanaotarajia kwenda kujiachia Ijumaa hii wajitokeze kwa wingi dukani kwake ambapo kuna pamba mpya na kali za kila aina ili watakapoingia katika tamasha hili la kuuaga mwaka 2013 wawe wametisha. Tamasha hilo pia litashuhudia wasanii Squizer na Ziggy Dee aliyetamba na wimbo wa Eno Mic pia wakitumbuiza ukumbini Royal Garden. Tamasha hili limewajia kwa udhamini wa Serengeti Breweries Ltd, Clouds Media Group, Chura Fashion, Gonala Pharmacy, Millenium Barber shop, Tabora Rest House, Nbs Classic, Mtingoni Company Ltd, Mussoma Batteries, CgFm 89.5, VoT fm 89.0 na Clouds Media Group.