Katika hali ya kusikitisha Mama Hawa Haji Kamanga (71) alifariki leo hii saa 2.40 Hospitalini Ocean Road baada ya kupigania uhai wake kwa siku kadhaa alizokuwa na hali mbaya sana lakini ilielekea alipigana kubaki hai mpaka pale wajukuu zake wawili walipofika toka America siku ya Jumamosi na kwenda moja kwa moja Ocean Rd Hospital kumuona Bibi yao. Wajukuu zake hao Kaela Jr (3)na Hadassah Bianca (1) walipofikishwa wodini Marehemu akaambiwa wajuu zako wamekuja kukuona inasemekana marehemu aliyekuwa na hali mbaya kwa wakati huo alitabasamu na kujaribu kusema kitu lakini hakuweza kutoa sauti, lakini bila shaka alifurahi kujua hatimaye wajukuu zake wamemkuta akiwa hai, na hatimaye akaamua muda ulikuwa sahihi kuacha kupigania uhai wake. Mama Hawa Kamanga ana watoto kadhaa wanaoishi nchini Marekani. Marehemu alilazwa Ocean Road wiki mbili hivi baada ya kuhamishiwa hapo kutokea katika hospitali ya Dk Mvungi ambako alilazwa kwa uchunguzi wa awali. Kwa sasa mipango ya mazishi inafanyika na tutaendelea kufahamishana humu na kwingineko.
Inna Lillah wa inna illahi Rajiun!