WAZIRI HAWA GHASIA AZINDUA MAFUNZO YA MADEREVA WA MABASI YA MWENDO WA HARAKA DAR ES SALAAM LEO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akijaribu kuendesha moja ya basi la mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam
Babasi ya wendo wa haraka yaliyoingia nchini kutoka nchini china,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Mohamed Mpinga (kushoto), akibadilishana mawazo na wadau wa usafirishaji kabla ya uzinduzi huo.
Meza kuu hiyo ikiwa na viongozi mbalimbali.
Msemaji wa Mradi wa DART, Sabri Mfuruki, akizungumza (katikati) akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji, William Masanja.
Wanahabari wakichukua taarifa katika uzinduzi huo.
Wakufunzi wa kutoa mafunzo kwa madereva hao kutoka China wakitambulishwa.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi ndani ya mchuma wakati wa uzinduzi huo. Hapo wanakwenda Kimara kutoka Ubungo na kisha kurudi Ubungo 'Hakika na Raha tupu'
Wanachi na wadau wengine wakiangalia mabasi hayo.
Dotto Mwaibale
MADREVA waliobahatika kuanza kupata mafunzo ya kimataifa ya kuendesha mabasi ya mwendo wa haraka chini ya mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka (DART), wametakiwa kuzingatia mafunzo hayo kwa makini.
Mwito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, wakati akizinduzi mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo.
"Mafunzo mtakayopata nawaombeni muyapokee kwa bidii na umakini mkubwa kwani yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa" alisema Ghasia.
Ghasia alisema mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo hayatalenga tu kuendesha magari bali pia namna ya kuwahudumia wateja.
Alisema anaamini mafunzo hayo yatawejengea madereva hao weredi na dinadhamu katika kazi yao ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kuandamwa na utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alisema mradi huu wa mabasi yaendayo kasi ni mradi wa aina yake hapa nchini na barani Afrika kwa ujuma na utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi na ni msingi wa maendeleo ya nchi.
Mahitaji ya madereva wanao hitajika katika mradi huo ni 330 na kuwa mradi huu ulioanza ni wa awamu ya kwanza na utakuwa wa awamu tano.
NHIF yawataka bloggers kujiunga na mfuko wa bima ya afya!
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akifungua semina ya kati ya mfuko huo na Ma blogger wanachama wa Chama habari za mitandao ya kijamii Tanzania Bloggers Nertwork TBN inayofanyika katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kurasini TEC jijini Dar es salaam, Katika semina hiyo mablogger hao wameaswa kujiunga na huduma ya KIKOA ili kujihakikishia huduma bora za afya zinazotolewa na mfuko huo kupitia bima hiyo, Katika picha kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mablogger TBN Bwana Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa Chama hicho Bi. Khadija Khalili.
Mhariri wa mtandao wa Bagamoyo News Bw. Sayed Abdul akitoa shukurani kwa niaba ya Mablogger mara baada ya mgeni rasmi kufungua semina hiyo inayofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Maaskofu.
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza katikasemina hiyo wakati alipokuwa akitoa mada kwa wana TBN inayofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Maaskofu.
Mmiliki wa Blogu ya K-VIS Blog Khalfan Said akishiriki katika semina hiyo pamoja na washiriki wengine.
Baadhi ya mablogger wakishiriki katika semina hiyo.
Robert Okanda kushoto na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti kulia Rachel Palangyo katikati na John Kitime wakiwa katika semina hiyo.
Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora
Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.
Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.
Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
|
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia |
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa. |
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3 |
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa. |
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum. |
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania. |
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema. |
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato. |
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema. |
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache. |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo. |
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi. |
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi |
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.
Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
|
Team Irene wakifuatilia mchakato |
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN central zone
Tabora Wanufaika na Mafunzo ya ULINGO – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP)
ULINGO WA WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na UNWomen.
Mafunzo hayo yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo pale Student Center.
Wanufaika na watia nia za kugombea nafasi mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wakifuatila mafunzo hayo yaliyotolewa na Hilda Stuart Dadu kutoma TWCP
Watia nia wakichukua kumbukumbu za mafunzo hayo mapema leo hii
Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo akifuatilia jambo kwa umakini.
Wakti mafunzo yakiendelea na maswali yakiulizwa kwa ufafanuzi zaidi kutoka kwa wawezeshaji.
Hilda Stuart Dadu wa ULINGO (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati mafunzo yakiendelea.
Muwezeshaji Emmiliana akitoa zoezi kwa wanafunzi wake ili kukazia zaidi kile walichofundishwa na kukifanya kwa vitendo.
Miongoni mwa wanakundi wakijadiliana jambo baada ya kupewa zoezi na muwezeshaji wa mafunzo.
Picha ya pamoja ya wanufaika wa mafunzo ya ULINGO na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watia nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mafunzo hayo yamekuja wakati huu ambao ndiyo haswa muda mwafaka wa uchaguzi mkuu wa ngazi za udiwani, ubunge na Urais.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)