Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora

Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora


Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.
Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.



Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum.
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.

Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
Team Irene wakifuatilia mchakato
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN central zone