mkalamatukio

Picha mbali mbali katika mazishi ya George Nganda!


Toka kushoto ni Dada July Kitundu, Dada Rita na Mama Desouza


Majonzi yatawala makaburini!

Kamanda wa CCM tawi la Kinondoni Bwawani Bw Steve Nyerere kulia akiwa na wadau wengine

Msanii Hard Mad naye alihudhuria mazishi

Wadau wa Pazi club











Issa Mndeme na Mratibu wa Kundi la wana Kinondoni Ivan Minja wakiweka shada la maua ktk kaburi

Florah Mwakpesile na Florah Samuel




Picha na Abdul Kazembe na Mkala Fundikira

Hatimaye George Nganda azikwa na mamia ya watu!


Mama wa marehemu(mwenye nguo nyeupe)
Kijana George Nganda aliyefariki majuzi kuamkia juzi hatimaye leo hii majira ya saa 9 mchana alipumzishwa katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni Fm. Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo wana jumuiya ya Kinondoni ambao katika umoja wao walijitolea kumsitiri kijana mwenzao rafiki yao mpendwa wao Bw George Nganda (38) kwa kuchangia sanduku, sanda na mashada. Akiongea na mtandao huu mmoja wa wajumbe wa jumuiya hiyo Bi Anna Samuel (Dada) alisema inasikitisha kumpoteza rafiki yetu mpendwa lakini tunakubali kuwa sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi. 

Akizungumzia jumuiya yao ya wana Kinondoni mjumbe Abdul Kazembe alisema "Jumuiya imefarijika kuchangia mazihi ya mwenzetu aliyetutoka ghafla lakini huu ni mwanzo tu jumuiya inajipanga kufanya makubwa zaidi, tukianzia katika kikao cha wanajumuiya wote mara baada ya kuhitimishwa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo tutakutana pale mango garden siku ya jumapili tarehe 26/7/2015 kuanzia saa 10 jioni ili kuteua viongozi wa muda na kisha kuijadili rasimu ya katiba ya jumuiya yetu ambayo iliratibiwa na mwanajumuiya Yahaya Pori"

Jumuiya hiyo ambayo pia inajiendesha kupitia mitandao ya Facebook na Telegram ambapo wanajumuiya wamejiunga na kujadili mambo yanayoihusu Jumuiya tu. Pia jumuiya inatarajia kufungua akaunti ya benki ili kujiendesha kiufasaha zaidi.
Baadhi ya wanajumuiya wakiwa makaburini kumzika rafiki yao George Nganda.
Msanii wa vichekesho Steve Nyerere na mdau Riziki Nyoni wakifuatilia mazishi 
Majonzi yalitawala!
Mc wa shughuli ya mazishi akiongea jambo

Wanajumuiya wa KINONDONI wakipiga picha ya mwisho katika kaburi la mpendwa wao George Nganda
Toka kulia Issa Mndeme, Evelyin Minja, Emmy Stephen
Toka kulia ni Issa Mndeme, Abdula Kazembe na Yohabu Chikwanda.
Kapumzike kwa amani George!
Picha na habari na Mkala Fundikira

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA


Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA)

Na Dotto Mwaibale

MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020, Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.

Alisema magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5 hadi 10.

"Tathmini ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.

Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Aidha, alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.  

"Hadi sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha  kliniki za magonjwa yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya Afya.

Anaongeza kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.

Semina ikiendelea.

George Nganda afariki dunia!


George Nganda (38) mkazi na mzaliwa wa Kinondoni B Mtaa wa Isere alifariki dunia juzi usiku kuamkia jana baada ya kuugua mapafu. Akiongea na mtandao huu Bw Ivan Minja ratibu wa Kundi la wakazi na waliokuwa wakazi wa Kinondoni ameeleza kusikitishwa na kifo cha ghafla cha kijana mwenzao ambaye wamekuwa wote katika mitaaa ya Kinondoni, Bw Minja alisema "Kama jumuiya ya wana Kinondoni tunatoa pole nyingi kwa wafiwa nikimaanisha familia ya marehemu lakini pia pole ziende kwa wanachama wote wa Kundi la Kinondoni katika  mitandao ya Facebook na Telegram. aliendelea kuesma "George alikuwa rafiki yetu na tutamkosa sana baada ya kututoka. aliongeza "Kama jumuiya tumekuwa tukihimizana kuchanga pesa kidogo ili tumzike mwenzetu aliyetangulia mbele za haki na kwa kweli michango inaenda vizuri sana, labda nichukue fursa hii kuwapongeza wanachama wote ambao wametoa michango na miwahimize ambao hawajatoa watoe ili pesa hizo zisaidie shughuli za msiba na hatimaye mazishi.

Marehemu George Nganda ambaye hakuacha mke wala mtoto atazikwa kesho saa kumi katika makaburi ya Mwembe jini