Mama wa marehemu(mwenye nguo nyeupe) |
Akizungumzia jumuiya yao ya wana Kinondoni mjumbe Abdul Kazembe alisema "Jumuiya imefarijika kuchangia mazihi ya mwenzetu aliyetutoka ghafla lakini huu ni mwanzo tu jumuiya inajipanga kufanya makubwa zaidi, tukianzia katika kikao cha wanajumuiya wote mara baada ya kuhitimishwa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo tutakutana pale mango garden siku ya jumapili tarehe 26/7/2015 kuanzia saa 10 jioni ili kuteua viongozi wa muda na kisha kuijadili rasimu ya katiba ya jumuiya yetu ambayo iliratibiwa na mwanajumuiya Yahaya Pori"
Jumuiya hiyo ambayo pia inajiendesha kupitia mitandao ya Facebook na Telegram ambapo wanajumuiya wamejiunga na kujadili mambo yanayoihusu Jumuiya tu. Pia jumuiya inatarajia kufungua akaunti ya benki ili kujiendesha kiufasaha zaidi.
Baadhi ya wanajumuiya wakiwa makaburini kumzika rafiki yao George Nganda. |
Msanii wa vichekesho Steve Nyerere na mdau Riziki Nyoni wakifuatilia mazishi |
Majonzi yalitawala! |
Mc wa shughuli ya mazishi akiongea jambo |
Wanajumuiya wa KINONDONI wakipiga picha ya mwisho katika kaburi la mpendwa wao George Nganda |
Toka kulia Issa Mndeme, Evelyin Minja, Emmy Stephen |
Toka kulia ni Issa Mndeme, Abdula Kazembe na Yohabu Chikwanda.
Kapumzike kwa amani George! |
Picha na habari na Mkala Fundikira