mkalamatukio

Imetosha foundation yatoa msaada kwa kituo cha Buhangija, Shinyanga!


Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisis ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, Shinyanga ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban 300. Misaada hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo  imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.

Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji kula kila siku.

Mkuu wa kituo hicho alisema anashukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi ya dhati na watoto wa kituo hicho na kuguswa na changamoto zinazowakuta, kwani si mara nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka misaada kituoni hapo kitu ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3 zilizopita taasisi hiyo ilipeleka msaada wa chakula kituoni hapo.

Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani Bi Kathrin Hoff alielezwa kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na Imetosha kwa uhamasishaji inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia amepongeza sana hatua ya Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija kujitegemea badala ya kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni mhitimu toka chuo kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.
Baadhi ya missada iliyotolewa na Imetosha pembeni kulia ni mabelo mawili ya mguo.
Mkuu wa kituo hicho Bw Peter Ajali akiongea na watoto wa kituo hicho akieleza dhamira ya ya asasi ya Imetosha kwao.


Hapa wakimsikiliza Masoud Kipanya
Baadhi ya wasichana wa kituoni hapo wakifurahia msaada wa nguo za ndani na vifaa vya hedhi walivyokabidhiwa na mjumbe wa Imetosha aishiye Shinyanga Bibi Herriet

Picha na habari kwa hisani ya TBN kanda ya kati.

KADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI ANSI MMASI ATOA MSAADA KWA WALIOATHIRIKA NA MFURIKO MOSHI VIJIJINI.

Chakula cha msaada kwa ajili ya wananchi walio athirika na mafuriko wilaya ya Moshi vijijini kikushushwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya kwenda kukabidhiwa kwa wahusika.
Kada wa Chama cha Mapinduzi Ansi Mmasi akikabidhi msaada wa Chakula kwa afisa tarafa,Eveline Mmary ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya katibu tawala wa wilaya ya Moshi .
Afisa Tarafa wa Kilimanjaro akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika eneo la TPC wilaya ya Moshi vijijini.
Kada wa chama cha Mapinduzi Ansi Mmasi akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa Chakula kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko katika eneo la TPC wilaya ya Moshi vijijini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MKURUGENZI MUWSA ,MHANDISI CYPRIAN LUHEMEJA AWAAGA WAFANYAKAZI,NI BAADA YA KUHAMISHIWA DAWASCO.

 
Aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshu (MUWSA) mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa kauli ya kuwaaga baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Mtendaji mkuu  DAWASCO.
Kauli ya Mhandisi Luhemeja ya kuwaaga wafanyakazi hao ilionekana kama mwiba na kuzua simanzi kuu kwa watumishi hao waliofanya kazi na mkurugenzi huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi 10.
Mhandisi Luhemeja akijaribu kuwapatia wafanyakazi hao Lugha nzuri angalau wasibaki na majonzi.
Meneja Fedha wa MUWSA ,Joyce Msiru akizungumza jambo katika kikao hicho.
Hali ya huzuni ndio ilitawala katika viunga vya ofisi za Mamlaka hiyo.

Na Dixon Busagaga a Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MIPANGO NA SERA ZITEKELEZWE KUMUOKOA MAMA NA MTOTO MCHANGA

DSC_0334
Mratibu wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama Ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Chiku Lweno akielezea jitihada zinazofanywa na mradi wa Mama Ye katika kukabiliana na vifo vya Mama na mtoto ambapo aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelemisha jamii ili iweze kuepukana na vifo vya mama na mtoto ambalo nalo ni janga la taifa.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Musoma
SERIKALI imeshauriwa kuhakikisha sera na mipango mizuri iliyopo kwa afya ya mama na mtoto mchanga inasimamiwa na kutekelezwa ili kuliondoa taifa katika janga la kupoteza mama na watoto wakati wa uzazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Chiku Lweno katika mafunzo kwa waandishi wa habari mjini Musoma.
Alisema bila kutekeleza mipango mizuri ambayo Rais Jakaya Kikwete amekuwa championi wa masuala ya wanawake na watoto kitaifa na mataifa, tatizo la vifo kwa wanawake wenye pingamizi za uzazi na watoto wachanga.
Alisema kutokana na haja ya kutoa msukumo katika masuala ya uzazi wameamua kuwapatia elimu waandishi wa habari ili wawe chachu ya kutambua umuhimu wa ukunga na uzazi salama.
"Tunafunza waandishi wa habari ili waweze kusukuma mbele shahuri hili ili kila mtu katika nafasi yake atetee nafasi yake" alisema Lweno.

Alisema suala la mama na mtoto mchanga ni masuala mtambuka ambapo mambo mengi lazima yaunganishwe yafikiriwe na kutambuliwa ili kudhibiti vifo vya wanawake na watoto wachanga.
Alitaja masuala hayo kama upangaji wa bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kusaidia kupatikana kwa wakunga wataalamu na vifaa vyao vya kazi na maeneo ya kufanyia kazi. Aidha kuwapo kwa ukubali wa wakunga na elimu ya uzazi.
Alisema ni vyema waandishi wa habari kama watia chachu kuelimishwa mambo mengi yanayohusiana na uzazi salama ambapo ndani yake kuna masuala ya bajeti na ufuaji wa wataalamu na ufuatuiliaji wa sera na sheria zilizopo katika kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.
Alisema anaamini waandishi wa habari wakielewa mambo hayo watasaidia kukomaa nalo na kuwezesha kila mtu kuwajibika.
DSC_0278
Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja yaliyofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) kuelekea kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mara.
Naye Afisa Muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Saturini Manangwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari alisisitiza haja za waandishi kutambua dhana ya afya ya mama na mtoto kuwa ni kitu mtambuka kutokana na suala la lenyewe kutegemeana.
Alisema serikali inapohimizwa kuwekeza kwa mkunga kunatokana na ukweli kuwa huduma ya mama na mtoto mchanga itakujwa bora kwa kuwa na mkunga bora mwenye vifaa na anayefahamu wajibu wake kuanzia ujauzito wa mama hadi kujifungua kwake.
Alisema uwekezaji huo unagusia changamoto nyingi zilizopo sasa kama upungufu wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa, miundombinu na masuala anuai ambayo yameegemezwa na utambuzi wa bajeti na umuhimu wake kama kipaumbele.
Alisema kwamba katika upangaji bajeti kila kitu kinategemea huwezi kusema unazidisha hiki na unakiacha hiki.
Alisema mathalani katika hali bora ya ukunga na uwezo wa kumsaidia mhusika ,viwango vya dunia vilivyoweka na Shirika la Afya Duniani (WHO) kila mkunga mmoja ahudumie angalau watu sita, lakini sehemu kubwa ya dunia haifikii hivyo.
Aidha alisema kwa Tanzania kiwango ni mkunga mmoja ahudumie watu 20-25 lakini kwa sasa Tanzania mkunga mmoja anahudumia zaidi ya watu 50.
Kimsingi alisema Tanzania ina tatizo la wakunga na pamoja na serikali kuanzisha vyuo vya kufunza wakunga na kukubali mashirika ya dini nayo kufanya hivyo hali bado ni tete.
Hata hivyo alisema ni kupitia wakunga waliowataalamu upo uwezekano wa kuzuia vifo visivyo vya lazima.
DSC_0253
Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akizungumzia nia ya chama hicho ni kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa anapata huduma za mkunga mtaalamu.

Muuguzi huyo mwandamizi pia alisema katika juhudi za serikali kunaanzishwa mafunzo ya mwaka mmoja ambapo yatatoa maofisa afya ambao kazi yao kubwa itakuwa kujua idadi ya wanawake wajawazito na wagonjwa katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa zahanati iliyo karibu.
Alisema ofisa huyo kazi yake haitakuwa hospitalini au kwenye zahanati bali kwenye jamii akitambua idadi ya wagonjwa wake na kutoa taarifa sahihi ya hali ya afya ya kitongoji chake kwenye zahanati.
Mmoja wa washiriki Belina Nyakeke ambaye ni mwandishi wa habari wa magazeti alisema kwamba amefurahishwa na mafunzo hayo ambayo yamempa nafasi ya kutambua wajibu wake katika kusaidia kuondoa tatizo la vifo vya mama na mtoto mchanga.
Alisema japokuwa mafunzo ni ya muda mfupi lakini yamemfumbua macho kutambua wajibu na haki kwa wananchi na serikali.
Naye Ahmed Makongo akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemfanya atambue wajibu wake kusaidia kusukuma mambo yaende sawa kwa upande wa waamuzi na pia wananchi husika kwa kuzingatia mafunzo hayo yaliyoletwa kwao na Mama Ye na UTTPC chini ya Ufadhili wa Shirika la Mpango wa watu Duniani (UNFPA)
DSC_0219
Afisa muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa akizungumzia changamoto za upungufu wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa, miundombinu n.k wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mjini Musoma mkoani Mara.
DSC_0299
Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) anayeshugulikia mifumo ya Afya, Felista Bwana akitoa takwimu za nchi zinazoongoza kwa vifo vya mama na mtoto kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mjini Musoma.
DSC_0244
Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen, mkoani Mara, Belina Nyakeke (katikati) akishiriki kwenye mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika mjini Musoma na kufadhiliwa na Shirika la UNFPA.
DSC_0207
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima mjini Musoma, Igenga Mtatiro akiuliza swali kwa Afisa muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa (hayupo pichani).
DSC_0229
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Mara ambao pia wanachama wa vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) walioshiriki mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mradi wa Mama Ye kwa kushirikiana na UTPC na kufadhiliwa na UNFPA.
DSC_0267
DSC_0260
DSC_0197
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
DSC_0242
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya (kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo.
KAWAIDA DSC_0334 Mratibu wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama Ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Chiku Lweno akielezea jitihada zinazofanywa na mradi wa Mama Ye katika kukabiliana na vifo vya Mama na mtoto ambapo aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelemisha jamii ili iweze kuepukana na vifo vya mama na mtoto ambalo nalo ni janga la taifa.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog). Na Mwandishi wetu, Musoma SERIKALI imeshauriwa kuhakikisha sera na mipango mizuri iliyopo kwa afya ya mama na mtoto mchanga inasimamiwa na kutekelezwa ili kuliondoa taifa katika janga la kupoteza mama na watoto wakati wa uzazi. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Chiku Lweno katika mafunzo kwa waandishi wa habari mjini Musoma. Alisema bila kutekeleza mipango mizuri ambayo Rais Jakaya Kikwete amekuwa championi wa masuala ya wanawake na watoto kitaifa na mataifa, tatizo la vifo kwa wanawake wenye pingamizi za uzazi na watoto wachanga. Alisema kutokana na haja ya kutoa msukumo katika masuala ya uzazi wameamua kuwapatia elimu waandishi wa habari ili wawe chachu ya kutambua umuhimu wa ukunga na uzazi salama. "Tunafunza waandishi wa habari ili waweze kusukuma mbele shahuri hili ili kila mtu katika nafasi yake atetee nafasi yake" alisema Lweno. Alisema suala la mama na mtoto mchanga ni masuala mtambuka ambapo mambo mengi lazima yaunganishwe yafikiriwe na kutambuliwa ili kudhibiti vifo vya wanawake na watoto wachanga. Alitaja masuala hayo kama upangaji wa bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kusaidia kupatikana kwa wakunga wataalamu na vifaa vyao vya kazi na maeneo ya kufanyia kazi. Aidha kuwapo kwa ukubali wa wakunga na elimu ya uzazi. Alisema ni vyema waandishi wa habari kama watia chachu kuelimishwa mambo mengi yanayohusiana na uzazi salama ambapo ndani yake kuna masuala ya bajeti na ufuaji wa wataalamu na ufuatuiliaji wa sera na sheria zilizopo katika kuhakikisha usalama wa mama na mtoto. Alisema anaamini waandishi wa habari wakielewa mambo hayo watasaidia kukomaa nalo na kuwezesha kila mtu kuwajibika. DSC_0278 Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja yaliyofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) kuelekea kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mara. Naye Afisa Muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Saturini Manangwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari alisisitiza haja za waandishi kutambua dhana ya afya ya mama na mtoto kuwa ni kitu mtambuka kutokana na suala la lenyewe kutegemeana. Alisema serikali inapohimizwa kuwekeza kwa mkunga kunatokana na ukweli kuwa huduma ya mama na mtoto mchanga itakujwa bora kwa kuwa na mkunga bora mwenye vifaa na anayefahamu wajibu wake kuanzia ujauzito wa mama hadi kujifungua kwake. Alisema uwekezaji huo unagusia changamoto nyingi zilizopo sasa kama upungufu wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa, miundombinu na masuala anuai ambayo yameegemezwa na utambuzi wa bajeti na umuhimu wake kama kipaumbele. Alisema kwamba katika upangaji bajeti kila kitu kinategemea huwezi kusema unazidisha hiki na unakiacha hiki. Alisema mathalani katika hali bora ya ukunga na uwezo wa kumsaidia mhusika ,viwango vya dunia vilivyoweka na Shirika la Afya Duniani (WHO) kila mkunga mmoja ahudumie angalau watu sita, lakini sehemu kubwa ya dunia haifikii hivyo. Aidha alisema kwa Tanzania kiwango ni mkunga mmoja ahudumie watu 20-25 lakini kwa sasa Tanzania mkunga mmoja anahudumia zaidi ya watu 50. Kimsingi alisema Tanzania ina tatizo la wakunga na pamoja na serikali kuanzisha vyuo vya kufunza wakunga na kukubali mashirika ya dini nayo kufanya hivyo hali bado ni tete. Hata hivyo alisema ni kupitia wakunga waliowataalamu upo uwezekano wa kuzuia vifo visivyo vya lazima. DSC_0253 Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akizungumzia nia ya chama hicho ni kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa anapata huduma za mkunga mtaalamu. Muuguzi huyo mwandamizi pia alisema katika juhudi za serikali kunaanzishwa mafunzo ya mwaka mmoja ambapo yatatoa maofisa afya ambao kazi yao kubwa itakuwa kujua idadi ya wanawake wajawazito na wagonjwa katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa zahanati iliyo karibu. Alisema ofisa huyo kazi yake haitakuwa hospitalini au kwenye zahanati bali kwenye jamii akitambua idadi ya wagonjwa wake na kutoa taarifa sahihi ya hali ya afya ya kitongoji chake kwenye zahanati. Mmoja wa washiriki Belina Nyakeke ambaye ni mwandishi wa habari wa magazeti alisema kwamba amefurahishwa na mafunzo hayo ambayo yamempa nafasi ya kutambua wajibu wake katika kusaidia kuondoa tatizo la vifo vya mama na mtoto mchanga. Alisema japokuwa mafunzo ni ya muda mfupi lakini yamemfumbua macho kutambua wajibu na haki kwa wananchi na serikali. Naye Ahmed Makongo akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemfanya atambue wajibu wake kusaidia kusukuma mambo yaende sawa kwa upande wa waamuzi na pia wananchi husika kwa kuzingatia mafunzo hayo yaliyoletwa kwao na Mama Ye na UTTPC chini ya Ufadhili wa Shirika la Mpango wa watu Duniani (UNFPA) DSC_0219 Afisa muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa akizungumzia changamoto za upungufu wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa, miundombinu n.k wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mjini Musoma mkoani Mara. DSC_0299 Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) anayeshugulikia mifumo ya Afya, Felista Bwana akitoa takwimu za nchi zinazoongoza kwa vifo vya mama na mtoto kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mjini Musoma. DSC_0244 Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen, mkoani Mara, Belina Nyakeke (katikati) akishiriki kwenye mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika mjini Musoma na kufadhiliwa na Shirika la UNFPA. DSC_0207 Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima mjini Musoma, Igenga Mtatiro akiuliza swali kwa Afisa muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa (hayupo pichani). DSC_0229 Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Mara ambao pia wanachama wa vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) walioshiriki mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mradi wa Mama Ye kwa kushirikiana na UTPC na kufadhiliwa na UNFPA. DSC_0267 DSC_0260 DSC_0197 Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo. DSC_0242 Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya (kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo. 

Rais Kikwete na Jopo la watu mashuhuri waanza kazi New York


Rais Kikwete na Jopo la watu mashuhuri waanza kazi New York

Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .
Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.
Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.

Bilionea Dangote bado anataka kuinunua Arsenal!

Uwanja wa the Emirate London ya kaskazini
Bilionea mNigeria mfanyabiashara wa saruji Bw Aliko Dangote ameeleza nia yake ya kuinunua klabu ya Arsenal ya England. Dangote ambaye ndiye mtu tajiri kuliko wote katika bara la Afrika ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani bilioni 15 aliuambia mtandao wa bloomberg kuwa "Naweza kuinunua Arsenal lakini si kwa bei ya kiwazimu ila kwa bei ambayo wamiliki watashawishika kuniuzia"

Dangote ambaye ana pesa nyingi kuliko mmiliki wa sasa wa Arsenal Stan Kroenker mwenye 67% ya hisa na mwanahisa mwingine Mrusi Alisher Usmanov.
Aliko Dangote(58) bilionea m Nigeria, mwenye mapenzi na Arsenal Football club ya jijini London, England.

Lakini Dangote alibainisha kuwa mpango wa kununua kilabu hicho maarufu kama the gunners haupo hivi karibuni, alisema "Tunawekeza kiasi cha dola bilioni 16 katika miradi tofauti miaka michache ijayo, kwani nataka kupeleka biashara zangu katika kiwango fulani, na nikimaliza hilo ndipo ofa ya kuinunua Arsenal itafuata" Pia Dangote amepata kukaririwa akisema kocha Arsene Wenger anatakiwa kubadili mfumo wa timu yake. Arsenal imekuwa na sifa ya kutandaza soka safi na la kuvutia lakini wameshindwa kushinda ubingwa wa England kwa karibu miaka 11 na kabla ya mwaka jana ambapo walishinda kombe la FA walikuwa hawajashinda kikombe chochote kwa miaka 9.

Mwanahisa mkuu wa Kilabu hicho Bw Stan Kroenker amenunua hisa zaidi hivi karibuni na haielekei ana mpango wa kukiuza kilabu hicho katika miaka ya karibuni.

Dangote pia anajenga kiwanda cha saruji mjini Mtwara ambapo wakazi wengi wa mkoa huo watapata ajira za muda na za kudumu.
Stan Kroenker (67) bilionea Mmarekani ndiye mbia mwenye hisa kubwa katika kilabu cha Arsenal kwa sasa
Kocha Wenger amatakiwa kubadili mfumo wa timu yake na Dangote
source Mirroronline