Msanii Moses Bushagama aka Mez B afariki dunia leo!
Mez B enzi za uhai wake! |
Msanii Moses Bushagama aka Mez B aliyewahi kung’ara na ngoma ya kikuku cha mama Roda ambayo mimi Mkala Fundikira nilimfanyia video yake katika miaka ya 2000 katika studio za Royal Productions, pamoja na nyimbo zingine nyingi amefariki dunia leo mjini Dodoma ambako mama yake huishi baada ya kuugua kifua kikuu(TB). Binafsi nimeshtushwa na kifo chake hasa baada ya kupata habari za kifo chake bila kufahamu kama alikuwa akiugua kwa muda.Mez alikuwa na kipaji cha aina yake na sauti laini, tutamkumbuika daima.
Mungu ilaze pema roho yake!
Picha kwa hisani ya Dj Choka
Homa ya mchezo kati ya Coastal union na Simba sports club yapamba moto!
Wakazi wa jiji la Tanga, viunga vya vyake na mikoa ya jirani leo hii watapata burudani inayotarajiwa kuwa ya kupendeza leo hii jioni mnamo saa 10.15 za jioni wakati Wekundu wa Msimbazi Simba SC itakapoingia katika stadia ya Mkwakwani kucheza mchezo wa Vodacom Premier league 2014/15 dhidi ya Coastal union ya jijini hapa kuwania pointi 3 muhimu hasa kwa Simba ambayo imekua ikifanya vibaya msimu huu na kupelekea hofu kwa washabiki wake kuwa uenda ikateremka daraja. Mpambano huo bila shaka utaoneshwa LIVE na kituo cha Televisheni cha AZAM ambacho mitambo yake imeonekana mje ya uwanja wa Mkwakwani, kama ionekanavyo hapo chini.
OB Van ya Azam Tv ikiwa tayai kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Mkwakwani stadium. |
Sare za Simba SC zikiwa zimeanikwa kwa mauzo nje ya uwanja wa Mkwakwani |
Mshabiki wa Simba kushoto akijadili bei ya fulana ya timu hiyo ya jijini Dar es Salaam karibu na uwanja wa Mkwakwani. |
Mfereji mpya wa maji wahatarisha watumia barabara ya Boma Tabora!
Kushoto unaonekana mfereji wa maji. |
Barabara ya Boma inavyoonekana pichani |
Promota wa Lennox Lewis aamua kuwa mwanamke!
Frank Maloney akishangilia ushindi wa Lenox Lewis |
Frank Maloney(61) promota maarufu wa ndondi wa zamani ambaye amewahi kuwa promota wa bingwa wa zamani wa uzito wa Juu Lennox Lewis ameamua kujibadili kuwa mwanamke na Kujiita Kellie. Kwa kauli yake Maloney alisema "Nimekuwa nikijisikia hivi tangu utotoni mwangu, hatimaye nimechoka kuishi kivulini. Pia alieileza ugumu ulikuwa ni kumfahamisha mkewe anachotaka kufanya, pia ameeleza atafanya operesheni ya badiliko la kijinsia, na kuwa hafanyi hayo ili awe na mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote bali ndivyo alivyokuwa akijisikia awe kwa miaka yote.
Maloney anavyoonekana sasa akiwa kama Kellie. |
Ajuza Kellie akiweka pozi |
Picha na habari kwa hisani ya mailonline na sunday mirror
Over pass yaporomoka na kuua watu wawili Brazil!
Barabara mpya ya juu (over pass) iliyokuwa ikijengwa mjini Belo Horizonte nchini Brazil iliporomoka jana (Alhamisi) na kuanguakia malori matatu, gari dogo na basi la kusafirishia abiria na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 19. Hata hivyo maafisa wa uokoaji wameeleza kuna nafasi kubwa ya miili mingine kupatikana chini ya barabara hiyo. Barabara hiyo ilijengwa ili kupunguza msongamano katika kipindi hiki cha world cup nchini Brazil ambapo mjini Belo Horizonte ambapo pana uwanja wa Mineirao ambao utatumika kwa mchezo wa nusu fainali siku ya jumanne katika mfululizo wa fainali za kombe la dunia 2014.
Kwa juu inaonekana over pass hiyo ikiwa imelala ardhini baada ya kuporomoka |
Basi lililoangukiwa na barabara ambamo dereva wake ni mmoja wa watu wawili waliokufa papo hapo hapo jana. |
Gari dogo lililoangukiwa na over pass mijini Belo Horizonte, nchini Brazil. |
Malori mawili yanaonekana kubanwa na over pass hiyo huku waokoaji wakishauriana |
Uwanja wa Mineirao utakaochezewa mchezo nusu fainali mjini Belo Horizonte uliopo Km 3 toka eneo la ajali. Picha kwa hisani ya AFP/ habari na mirror online |
HAWA NDIYO WAREMBO WA REDDS MISS KANDA YA KATI 2014 [DODOMA]
Washindi watatu bora wa mashindano ya REDDS MISS KANDA YA KATI 2014, Mshindi akiwa ni Dorice Mole (katikati) akitokea mkoa wa singida, wa pili ni Zenna Motte (kushoto) akitokea Tabora katika Chuo Kikuu cha SAUT-TABORA na wa tatu ni Adelaide (kushoto). Warembo hao wakifurahia ushindi huo usiku wa tarehe 20 Juni, 2014
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)