Zetrida Ezekiel atoka na Ringa na Yesu!

Zetrida Ezekiel atoka na Ringa na Yesu!


Zetrida Ezekiel ni mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili aishiye mkoani Kigoma, amekuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili ambaye ni mwana kwaya wa  kikundi maarufu na kikongwe cha nyimbo za injili cha MKE MWEMA cha mjni Kigoma. Zetrida ameolewa na ni mama wa watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.

Lakini baada ya kupata rai nyingi na kwa muda mrefu toka kwa wachungaji wake na watu mbali mbali kuwa atengeneze albamu yake kama mwanamuziki wa kujitegemea,hatimae mwezi wa August mwaka huu Zetrida alikuja Dar es Salaam na kuanza kazi ya kutengeneza albam yake binafsi.
Zetrida Ezekiel akiwa katika pozi.



Album yake inayoitwa Ringa na Yesu ina nyimbo nane na nyimbo zote amezifanyia Tika records chini ya mtayarisha muziki maarufu nchini aitwaye Ephraim Kameta ambapo nyimbo sita katika albam yake hiyo zilitengenezwa na Kameta na mbili zikitengenezwa mtayarisha muziki machachari PG zote katika studio za Tika records pia. Katika albam hiyo kuna nyimbo kama Ringa na yesu liyobeba jina la albam Malaika, waombee maadui zako na nyingine nyingi zenye kiwango cha hali ya juu.

Akiongea na mtandao huu kwa njia ya simu Zetrida alipoulizwa ana mipango gani ya kufanya video ya albam hiyo Zetrida alisema "Natamani sana hata leo nianze kuandaa video lakini pesa inagomba kwa saa hasa baada ya kutoka kuandaa albam hii ya audio ambaye imechukua pesa nyingi kuandaa, inabidi nijpange tena kwanza"
Na alipoulizwa nini mipango yake ya baadae baada ya lutoa albamhiyo alisema "Mipango yangu ya baadae ni kumtangaza Yesu ndani na na nje ya Tanzania kwa kuwa ni kitu kilicho ndani ya damu yangu" Pia alielezea changamoto alizokutana nazo wakati akitayarisha albam hiyo ni pamoja kutofanya kazi kwa wakati uliopangiwa jambo ambalo hutokana na sababu mbali mbali ikiwemo katikizo la umeme, ambapo inatokea kazi iliyokuwa ifanyike jana inahamishiwa leo na wa leo ama utafanya kazi mida mibaya au kupangiwa siku nyingine. Lakini nashukuru sana kuwa nimeeza kumaliza albam hiyo bila tatizo.

Mwisho kabisa Zetrida alipenda kutoa shukurani zake akisema "Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa ujasiri wa kufanya albam yangu mwenyewe na pili mume wangu kwa kuniruhusu kufanya kazi hii ya uimbaji pia kujitoa kwake kwa hali na mali, vile vile bila kumsahau Mchungaji Joseph Malumbu wa Kijichi Mtongani ambaye alihusika katika usimamaizi wa albam ya Ringa kwa Yesu. Pia niwaombe tu wapenzi wa muziki wa injili waipokee albam yangu na wainunue kwa wingi kwani humo kuna nyimbo nzuri sana zenye kumtukuza Bwana Yesu hivyo kila mmoja ajipatie nakala yake sasa kwani tayari albami ipo madukani.
Kwa mialiko popote ndani na nje ya Tanzania wasiliana naye kwa nambari
+255675 406917/ +255756823477
au kwa barua pepe
zetridaezekiel@yahoo.com