Wana jumuiya ya Kinondoni kuteua viongozi baada ya mfungo wa Ramadhani!

Wana jumuiya ya Kinondoni kuteua viongozi baada ya mfungo wa Ramadhani!


Wanajumuiya wa kikundi cha Kinondoni wakibadilishana mawazo baada ya mazishi ya marehemu George Nganda

Mratibu wa kikundi cha wana Kinondoni Bw Ivan Minja amesema kikundi hicho kitateua vingozi wa muda katika kikao kitakachofanyika jijini Dar es Salaam baada ya mfungo wa Ramadhan, kikao hicho kitakachoteua uongozi wa muda wakati kitafanyika siku ya Jumapili ya tarehe 26/7/2015 pale Mango Garden Kinondoni Vijana kuanzia saa 10 za jioni. Akielezea ajenda kuhusuku kikao jicho Minja alisema ajenda kuu itakuwa kwanza kuteua viongozo wa muda kisha wajumbe wote wataijadili rasimu ya katiba yao ambayo imetungwa na Bw Yahya Pori ambaye ni mwanachama katika jumuiya hiyo. Jumuiya ambayo imeanzishwa kwa dhumuni kuu la kusaidiana katika dhiki na faraja inaundwa na wakazi nawalikuwa wakazi wa maeneo ya kinondoni na si wilaya ya Kinondoni.

Vidole viwili, maana yake nini Jamila Kaimika?
Ivan Minja (Mratibu) Anna Dada na Esther Shayo. Aliyesimama ni Goodsense.



Toka kushoto Esther, Mkala Fundikira(Mratibu) Evelyn Minja na Emmy Stephen.




Picha ya pamoja

Vijana wa Kino Group wakiwa katika pose!

Picha na Abdul Kazembe