Mlinzi mahiri wa kilabu cha Real Madrid Sergio Ramos amuambia uongozi wa kilabu hicho nguli kuwa anataka kujiunga na Manchester United na si vinginevyo kitendo hicho kimewapendeza mashabiki wengi wa soka hasa nchini England ambao wanaichukulia Real Madrid kama klabu onevu yaani inajiona yenye haki ya kuchukua mchezaji yeyote toka kilabu chochote na wakati wowote, kitu ambacho kimekuwa kikivikwaza vilabu vingine na hata mashabiki wao.
Real Madrid na wao sasa wanaonja joto ya jiwe toka kwa mchezaji wao, na Man united wanaitumia nafasi hiyo kuiteteresha Real Madrid. Duru zingine za habari zinaeleza kuwa hiyo ni janja ya Ramos kupata mkataba mpya na mnono toka Los Bloncos, imefahamika Ramos si mmoja wa wachezaji wanaolipwa vinono na Real Madrid hivyo anatumia mwanya huu ili kujipatia mshahara mnono.
Haya ni baadhi ya maoni ya baadhi wasabiki wa soka wengine si washabiki wa Man united lakini wanaonesha kukasirisha na kitendo cha Real kutaka wachezaji wa vilabu vingine huku wao wakigoma kuuza wao wanapotakiwa. |
Habari na picha kwa hisani ya
mailonline imefasiriwa na Mkala Fudikira