MAPINDUZI YAFELI BURUNDI

MAPINDUZI YAFELI BURUNDI

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.

Wananchi wa Burundi wakimpokea Rais Nkurunziza kijijini kwao Ngozi
Mashahidi wameiambia BBC kwamba rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia wamemlaki kwa shangwe na vigelegele

Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Generali Niyombare aliyeendesha jaribio la mapinduzi lililoshindwa aelezwa kuwa mafichoni huku akitafutwa na mamlaka za nchi hiyo ya Burundi.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.
Habari na picha kwa hisani ya BBC Swahili