Muandaaji wa Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahama Yusuph
Baada ya kufanya shindano la vipaji kwa mafanikio makubwa mnamo tarehe 23/5/2014 ambapo washiriki watano waliiingia fainali, sasa shindano la Miss Dar Indian Ocean litafanyika jumamosi ya tarehe 7/6/2014 katika viwanja vya Nyumbani Lounge, kiaina inaelekea waandaaji wamejipanga vema sana nadau na mashabiki wa tasnia hii wameombwa kujitokeza kwa wingi siku ya tukio ambapo wakali wa THT watatumbuiza hafla hiyo.