Roy Keane amshambulia vikali Ferguson!

Roy Keane amshambulia vikali Ferguson!

Nyakati za furaha:Sir Alex na nahodha wa zamani wa Man united Roy Keane wakibeba juu moja ya makombe ya EPL waliyoyashinda pamoja
Katika hali isiyoshangaza wengi Roy Keane amemshambulia kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson kuwa anapenda nguvu na utawala hata sasa ingawa si meneja tena wa Man united. Keane anayefahamika vema kwa utata wake ndani na nje ya uwanja amefikia kusema kuwa Brian Clough ndiye kocha bora aliyewahi kufundishwa naye na si Sir Alex kocha mwenye rekodi bora kuliko yeyote katika historia ya ligi ya Uingereza na ambaye yeye Keane aliwezeshwa kushinda mataji 7 ya premier league, makombe manne ya FA, kombe moja la ulaya na kombe 1 la klabu bingwa ya dunia na ngao za hisani zisizohesabika. Lakini Keane ambaye Alex Ferguson amemuelezea kuwa ni mwenye ulimi mchafu kuliko kingine chochote na kuwa anaweza kumfanya mtu mwenye kujiamini sana kunyong'onyea na kuwa kama mtoto mdogo asiyeweza kujitetea kwa kutumia ulimi wake mchafu(maneno) bado anaumizwa na kitendo cha Ferguson kumtimua Old Trafford baada ya yeye Keane kuwasema vibaya wachezaji wadogo wakiwemo Rio Ferdinand, Darren Fletcher kuwa hawapaswi kuichezea Man United alisema maneno hayo baada ya Man united kufungwa bao 4-1 Mwaka 2005 dhidi ya Middlesborough. Ndipo Ferguson akaamua kumfukuza Roy Keane pamoja na kuwa Fergie alihakikisha Roy Keane analipwa mshahara wake wote uliobaki na pia Roy Keane akapewa mechi ya Testimonial amabzo hupewa mchezaji aliyecheza timu moja kwa muda usiopungua miaka 10. Roy Keane aliichezea Man united kwa miaka 12 na nusu.
Alex Ferguson, ameelezwa na Roy Keane kuwa ni mwenye kupenda nguvu na kutawala.
Habari na picha kwa hisani mirroronline