mkalamatukio

Hatimaye baba wa Gary na Phil Neville azikwa kijijini kwao Bury!


Gary na Phil Neville wakiwa wamebeba jeneza la baba yao pichani chini!
Neville Neville (65) alifariki  wikinchini Australia kwa shambulizi la moyo.
 Baba wa wachezaji malejendari wa kilabu cha Manchester United Gary na Phil Neville, Neville Neville (65) alifariki kwa shambulizi la moyo mapema mwezi huu huko Australia ambako alikuwa na binti yake Tracey Neville katika mashindano ya Kombe la dunia ya mpira wa pete binti huyo ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya netball ya Uingereza.

David Beckham ambaye alicheza mpira na ndugu hao wawili alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri waliohudhuria mazishi hayo, wengine ni Sir Alex Ferguson, Dennis Law, Sam Alardyce, Steve Bruce, Ryan Giggs, Nicky But, Paul Scholes, Bryan Robson, Sandra Beckham(mama wa David Becham) Phil Jagielka(Kapteni wa Everton)

Kundi dogo la watu walikusanyka nje ya kanisa la parish mjini Bury kutoa heshima zao za mwisho kwa Neville Neville. Nevile Neville (65) alizikwa jana kijijni kwake Bury nje kidgo ya jiji la Manchester.
Steve Bruce kocha wa Hull city akiwasili kanisani
Meneja msaidizi wa Man united Ryan Giggs akiwasili na mkewe.
Paul Scholes na mkewe.
Meneja wa zamani wa West Ham United Sam Alardyce
David Beckham na mama yake Sandra.
Ryan Giggs, Nicky Butt na Steve Bruce wakijadili jambo.
Gary Neville akiwaliwaza mama na dada yake baada ya mazishi.
Tracy Neville akilia baada ya kumzika baba yao Neville Neville.
Malejendari wa Man united kushoto Sir Alex na Dennis Law


Phil Jagielka wa Everton.


Kanisa la Parish kijini Bury
Habari na picha kwa hisani ya themirronline

Jumuiya ya marafiki wa Kinondoni yapata uongozi wa muda

Toka kushoto waliosimama ni Abdul Kazembe (mjumbe) Mahmoud Kamusi(Mjumbe)Adam Tuga Bush (mjumbe)
Toka kushoto waliokaa Florah Samuel (mweka hazina msaidizi) Suzane Bagilla (katibu mkuu) Yahya Poli (Mwenyekiti) Mkala Fundikira (makamu wa mwenyekiti) na Jully Kitundu (mjumbe)
Jumuiya ya marafiki wa Kinondoni (Kinondoni Group) jana ilifankiwa kufanya mkutano wa kujadili na kuipitisha rasimu ya katiba na kuteua viongozi wa muda ambao walipewa jukumu la kuhakkisha jumuiya inapata usajili katika kipindi cha mwezi mmoja. 

Kikao hicho kilichoendeshwa na mwenyekiti wa kikao Bw Yahaya Poli kilikuwa na ajenda mbili 

1. Kuijadili na kuipitisha rasimu ya katiba ya jumuiya hiyo.
2. Kuteua viongozi wa na kamati tendaji ya muda.

Mkutano huo ulifanikiwa kuijadili na kuipitisha katiba hiyo pia mkutano uliwateua Bw Yahaya Poli kuwa mwenyekiti, Mkala Fundikira kuwa makamu wa mwenyekiti, Suzzane Bagila kuwa katib mkuu, Bw Ivan Minja kuwa katibu msaidizi na Ismail Kagambo kuwa mhazini mkuu akisaidiwa na Anna Samuel, vile wanajumuiya wanne waliteuliwa kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji ambao ni Abdul Kazembe, Jully Kitundu, Adam Bush na Mahmoud Kamusi. Hawa wanaungana na uongozi na kuwa 10 wanaunda kamati ya utendaji itakayokuwa chini ya Mwenyekiti Yahaya Poli. Dhumuni la kuanzisha jumuiya hiyo ni kujiunga pamoja na kusaidiana na kuwekeza katika fursa mbali mbali zitakazojitokeza

Akizungumzia uteuzi wake Bw Poli alisema"Napenda niwashukuru wajumbe wote wa mkutano huu kwa kuniamini na kunipa fursa ya kuiongoza jumuiya ya Kinondoni, naahidi kuitendea haki fursa hii na kuiongoza jumuiya kuelekea maendeleo ya ki uchumi na kijamii. Na naahidi kujitoa kwa hali na mali ili kuona tunapiga hatua za ki maendeleo siku hadi siku. Vile niwashukuru waratibu wetu Bw Ivan Minja na Bw Mkala Fundikira kwa kutukutanisha hapa leo, nitawaomba waendelee na moyo huo huo na jumuiya itafika mbali ki maendeleo.Alimaliza.

Jumuiya hiyo ina wanachama zaidi 2300 katika mtandao wa Facebook inakojulikana kama Kinondoni Group, ambapo iliasisiwa na Bw Ivan Minja huku Bw Mkala Fundikira akiendesha kundi la Telegram kupitia simu za mkononi. Makamu mwenekiti wa jumuiya hiyo alisema kamati tendaji imepewa kazi ya kuhakikisha jumuiya inasajiliwa ili wanachama wengi zaidi wa Kinondoni Group katika mtandao wa kijamii wa Facebook waweze pia kupata fursa ya kujiunga na jumuiya yao ya marafiki wa Kinondoni na wafaidike na matunda yote yatakayotokana na kuwa mwanajumuiya hai. Kikao hicho kilichofanyika Mamaz Tavern(Mamaz pub zamani) kilihudhuriwa na wanajumuiya 16 huku wengine wengi wakitoa udhuru kadhaa.
Mwenyekiti mteule Yahaya Poli akisisitiza jambo katika mkutano wa jana.
Makamu wa mwenyekiti (katikati) Mkala Fundikira na katibu Suzzy Bagilla (kulia) wakimsikiliza mwenyekiti.

Toka kushoto ni Fatyy Dula, Dada Rukia, Emmy Stephen, Dada Mariam, Ivan Minja na Kaka Poli

Toka kushoto ni Adam Bush, Florah Samuel, Mahmoud Kamusi na Abdul Kazembe.


Mudrikati Swedi kulia na suzzy Bagila.

Dax kushoto na Issa Mndeme wakifuatilia kikao.
Makofi kidogo.
Dada Jully Kitundu na Adam Bush.
Rukia Mussa na Emmy Stephen.
Picha ya pamoja





Picha na Camilius Kamili wa mkalamatukio blog

WAZIRI HAWA GHASIA AZINDUA MAFUNZO YA MADEREVA WA MABASI YA MWENDO WA HARAKA DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika  Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akijaribu kuendesha moja ya basi la mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika  Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam
 Babasi ya wendo wa haraka yaliyoingia nchini kutoka nchini china,
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Askari wa usalama barabarani wakipiga picha mabasi hayo.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Mohamed Mpinga (kushoto), akibadilishana mawazo na wadau wa usafirishaji kabla ya uzinduzi huo.
 Meza kuu hiyo ikiwa na viongozi mbalimbali.
 Msemaji  wa Mradi wa DART, Sabri Mfuruki, akizungumza (katikati) akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji, William Masanja. 
 Wanahabari wakichukua taarifa katika uzinduzi huo.
 Wakufunzi wa kutoa mafunzo kwa madereva hao kutoka China wakitambulishwa.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi ndani ya mchuma wakati wa uzinduzi huo. Hapo wanakwenda Kimara kutoka Ubungo na kisha kurudi Ubungo 'Hakika na Raha tupu'
Wanachi na wadau wengine wakiangalia mabasi hayo.


Dotto Mwaibale

MADREVA waliobahatika kuanza kupata mafunzo ya kimataifa ya kuendesha mabasi ya mwendo wa haraka chini ya mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka (DART), wametakiwa kuzingatia mafunzo hayo kwa makini.

Mwito huo umetolewa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, wakati akizinduzi mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika  Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo.

"Mafunzo mtakayopata nawaombeni muyapokee kwa bidii na umakini mkubwa kwani yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa" alisema Ghasia.

Ghasia alisema mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa  mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo hayatalenga tu kuendesha magari bali pia namna ya kuwahudumia wateja.

Alisema anaamini mafunzo hayo yatawejengea madereva hao weredi na dinadhamu katika kazi yao ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kuandamwa na utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alisema mradi huu wa mabasi yaendayo kasi ni mradi wa aina yake hapa nchini na barani Afrika kwa ujuma na utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi na ni msingi wa maendeleo ya nchi.

Mahitaji ya madereva wanao hitajika katika mradi huo ni 330 na kuwa mradi huu ulioanza ni wa awamu ya kwanza na utakuwa wa awamu tano.