BABA YAKE MSANII STEVE NYERERE AFARIKI!
Marehemu Francis Festus Mengele, enzi za uhai wake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Francis Festus Mengele.
Shangazi wa Msanii, Steve Nyerere, Grace Mengele (katikati), akiwa na wadogo zake Steve Nyerere wakati akiwasili makaburi ya Kinondoni kwa mazishi ya mpendwa wao, Francis Mengele.
Watoto wa marehemu na dada zake wakiwa kwenye ibada ya maziko makaburi ya Kinondoni.
Ibada ya maziko ikiendelea.
Hali ilivyokuwa wakati wa mazishi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele
likishushwa kaburini.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele
likishushwa kaburini.
Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mazishi hayo.
Ni huzuni tupu.
DC Makonda akiwa udongo kwenye kaburi la Francis Mengele wakati wa mazishi.
Kaburi likijengwe baada ya kuwekwa mwili wa marehemu kaburini.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele.
Waombolezaji wakiwasili makaburi ya Kinondoni tayari
kwa mazishi.
Hali ilivyokuwa makaburini.
Hali ilivyokuwa makaburini.
Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye maziko hayo.
Na Dotto Mwaibale
WASANII mbalimbali wa filamu na bongo fleva wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya baba ya msanii mwenzao Steve Mengele 'Steve Nyerere, aliyofanyika juzi makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msanii Jacob Stephen JB ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi ya marehemu Francis Mengele baba yake na msanii huyo aliyefariki wiki iliyopita kutokana na maradhi ya mapafu.
Wasanii wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Micky, Vicent Kigosi 'Ray' Elizabeth Michael 'Lulu' Chuchu Hans, Kajala Masanja 'Kajala' , Mtunzi na muongozaji wa filamu Myovela Mswaisa na wengine wengi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyeongoza mazishi hayo alisema kifo cha Mengele ni pigo kubwa katika wilaya hiyo ya Kinondoni na familia kwa ujumla.
"Mengele alikuwa na mchango mkubwa katika wilaya yetu ya Kinondoni katika kulipa kodi kutokana na biashara zake alizokuwa akizifanya na wingi huu wa watu waliojitokeza katika mazishi yake inaonesha jinsi alivyokuwa akishirikiana na wenzake hasa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kimara alikokuwa akisali" alisema Makonda.
Makonda alitumia fursa hiyo kuiomba Manispaa ya Kinondoni ndani ya miezi mitatu kuhakikisha inajenga choo katika makaburi hayo ya Kinondoni kwani ni aibu kwa eneo hilo kukosa choo hivyo kuwafanya wananchi wanaofika kwa ajili ya maziko kukosa huduma ya choo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
-0712-727062)

Prof Mark Mwandosya asaka wadhamini Kilimanjaro
Prof,Mwandosya akiteta jambo na RC Gama mara baada ya kukutana. |
Prof,Mark Mwandosya akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi ,Angela Kairuki walipokutana katika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaro. |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimpatia kipaza sauti Prof Mwandosya asalimie wajumbe waliokuwa katika ukumbi huo. |
Profesa Mwandosya akizungumza katika ukumbi huo. |
Prof Mwandosya akitoka katika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaromara bada ya kusalimia. |
Prof, Mwandosya akiagana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama mara baada ya kusalimia . |
Prof,Mark Mwandosya akiondoka ukumbini hapo
kuendelea na safari ya kusaka wadhamini mkoani Arusha. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini. |
Pamoja na kukosa tunzo ya Kili ki mizengwe Christian Bela apagawisha Tabora!
Christian Bella akijimwaga jukwaani. |
Bella akifanya yake jukwaani. |
Mashabiki wa Malaika Band wakpozi |
Hapo sasa! |
Baadhi ya mashabiki wakijmwaga! |
Music Producer Dula K kulia na msanii Masha Kay kushoto wakiwa na mdau. |
Wacha wee Benny Ngwasuma akijiachia |
Papaa Allex Ntonge mwaya mwaya! |
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN CENTRAL ZONE
Makamba alivyovunja rekodi ya mapokezi na wadhamini Iringa
Mh. January Makamba akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi Jesca Mambatavangu mara baada ya January kusaini kitabu cha wageni katika ofisi za Chama.
Mchngaji Kiwanga wa Iringa mjini akimkaribisha Mh. January Makamba na Mkewe katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa. Mchngaji huyo alimwombea na kumpa baraka zote za kugombea nafasi ya urais kupitia CCM.
Baadhi ywa wanachama wa Waendesha Bodaboda waliojitokeza kumpokea na kumsapoti Mh. January Makamba katika zoezi lake la kusaka wadhamini ndani ya chama ili aweze kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Mh. January Makamba na Mkewe wakisalimiana na baadhi ya vijana na wanachama wa CCM mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wiliya ya Iringa Mjini.
Mh. January Makamba na Mkewe wakiwapungia mkono baadhi ya vijana na wanachama wa CCM waliofika kumsapoti mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wiliya ya Iringa Mjini.
Mh. January Makamba akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa Mjini. Aliyesmama kulia kwake ni Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Zongo Lobe Zongo na kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Abeid Kiponza.
Mh. January Makamba akipunga Mkono kwa wanachama wa Iringa waliokuja kumuunga mkono mara baada ya kutoka kuewka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa Mjini.
Badhi ya vijana wa Iringa waliohuria katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini wakimsikiliza Mh. January Makamba huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti tofauti.
Mh. January Makamba na Mkewe wakiimba pamoja na wanachama wa CCM waliojitokeza katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini katika kumsapoti na kumdhamini kumuwezesha kushinda katika kinyang'anyiro cha kupewa ridhaa ya kugombea urais kupita CCM.
Mh. January Makamba akikabidhiwa fomu yenye majina ya wanachama waliomdamini na Mwenyekiti wa CCM wilya, Abeid Kiponza. Fomu hiyo in idadi ywa wanachama 630 waliojitokeza kumdhamini ikiwa ni kutoka wilaya ya Iringa Mjini na Kilolo.
Mh. January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya Iringa Mjini walijitokeza kumsapoti na kumdhamini. January amepata sahihi 630 za wanachama wa CCM kumdhamini, idadi hiyo ni ya wilaya ya Iringa Mjini na wilaya ya Kilolo. Picha Zote na Mpigapicha Wetu.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)