Ujumbe mzito wa Imetosha watembelea kituo cha Buhangija mjini Shinyanga!
Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa
harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha
kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha
za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao
ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.
Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo. |
Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga |
Wajumbe wa Imetosha |
Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo |
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha |
Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba
wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula
mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa”
alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga
kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10.
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis
alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho
kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.
Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa
ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284
wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo
chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa
kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.
Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho
Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands! |
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga |
Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho |
Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali |
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira
Ujumbe wa Imetosha Foundation wawasili Mwanza!
Salome Gregory akifuatiwa na Balozi Mdimu na Issaya Mwakilasa wakiteremka toka katika ndege iliyowasafirisha toka Dar mpaka Mwanza. |
Picha ya kumbukumbu toka kushoto ni Issaya Wakuvwanga, Zaytuni Biboze, Salome Gregory, Henry Mdimu na Mkala Fundikira, Mwanza airport. |
Ujumbe wa taasisi ya Imetosha inayojishughulisha na utoaji elimu juu ya kumaliza unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini uliwasili jijini Mwanza leo hii saa 2 asubuhi kwa ziara ya siku 3 ambapo kati siku hizo tatu ujumbe huo utakutana na viongozi wa ki serikali na usalama wa baadhi ya mikoa na wilaya za kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Shinyanga. Lengo la mikutano hiyo ni kamati kujitambulisha kwa viongozi hao na kuwaeleza nini Imetosha inatarajia kufanya katika kanda hii mwezi ujao ambako pamekuwa na matukio mengi ya ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania.
Vile vile kamati itakuwa na siku moja ambapo itatembelea vyombo ya habari vya jijini hapa kabla ya kurejea Dar es Salaam.
Habari na picha na Mkala Fundikira wa Mkalamatukio/keronyingi blog
Kamati ya imetosha yatuma ujumbe mzito kanda ya ziwa!
Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari |
Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya janga hili. Ujumbe huo utaongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw Masoud Kipanya, Balozi Henry Mdimu Mgaya na katibu Salome Gregory,wajumbe watakaongozana na viongozi hao ni pamoja na Mkala Fundikira, Isaya Mwakilasa (wakuvwanga aka Baba Andunje) Zaytun Biboze, Kelvina John na msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika.
Mwenyekiti Masoud Kipanya akiongea katika kilele cha matembezi ya hamasa yaliyofanyika jijini Dar |
Dhumuni la safari hiyo itakayoupeleka ujumbe huo mpaka mkoani Shinyanga ni kwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali na usalama wa mikoa na za kanda hiyo iliyoathiriwa sana na janga la ukatili na mauaji ya watu wenye ualbino. Taasisi ya Imetosha imepanga kwenda kanda ya ziwa baadaye mwezi ujao ambapo timu itaenda maeneo yaliyoathiriwa na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa si kweli kwamba ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ualbino utapata mafanikio, elimu hizo zitatolewa kwa njia ya filamu mbali mbali, michezo ya kuigiza na matamasha ya muziki.
Hoteli ya Green Palm utakapofikia ujumbe wa Imetosha Foundation jijini Mwanza aka the Rock City. |
Isaya Mwakilasa wa (Orijino komedi) Henry Mdimu na familia ya Isaya aka Wakuvwanga |
Maktaba Baadhi ya wajumbe wa Imetosha wakijiandaa kwenda katika mchezo wa Simba na Yanga |
WANAFUNZI WA CARMAN AINSWORTH HIGH SCHOOL WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.
Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe balozi Liberata Mulamula.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe, balozi Leberata Mulamula.
Mhe, balozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.
Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.
Picha na habari kwa hisani ya Mubela Bandio wa Changamoto blog
Siku Mh Al Shaymaar Kweigir alipoweka uheshimiwa pembeni na kusema IMETOSHA!
Mh Al Shaymaar akicheza wimbo wa Imetosha na balozi Mdimu pamoja na baadhi ya watu waliohudhuria matembezi ya uhamasishaji wimbo huo uliimbwa na msanii wa reggae Jhikoman Manyika . |
Siku ya matembezi ya uhamasishaji dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino yaliyofanika kutoka viwanja vya Biafra mpaka viwanja vya leaders mbunge wa viti maalum Mh Al Shaymaar Kweigir aliamua kuuvua uheshimiwa kwa muda na kujichanganya na wadau wengine walijitokeza kiwanjani hapo kwa kucheza kwa hisia kubwa yenye kuinesha kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Imetosha foundation za kuelimisha na hatimaye kutokomeza kabisa unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino duniani! Matembezi na tamasha viliandaliwa na Imetosha foundation kwa dhamini toka IPTL, Legendary Music, EFM Radio, TDL, Coca Cola, Ultimate security na Flexible studios
Mwenyekiti wa Imetosha foundation akimpongeza Mh Al Shaymaar baada ya matembezi. |
MC mkongwa Mzee Mdachi akiwa katika pose! |
Nyie chukueni selfie mie nimevutiwa na ya jukwaani! |
Rose Manumba na Jamila wakiwakilisha! |
Monica Joseph kulia akiongea na baadhi ya wadau wa harakati za Imetosha |
Emmanuel Masaka akijiuliza Nitumie camera gani hapa???? |
Kelvina na Jestina wa Jestina George blog |
Wajumbe wa Imetosha foundation! |
Picha zote na Mkala Fundikira wa keronyingi blog
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)