PICHA ZA MAZISHI YA NYAWANA FUNDIKIRA
MAMAA NYAWANA AMEPUMZISHWA KATIKA MAKAZI YAKE YA MILELE KATIKA MAKABURI YA ITETEMYA HAPA MKOANI TABORA, NJE KIDOGO NA MJI
MAZISHI YAMECHELEWESHWA KUTOKANA NA KUCHELEWA KUWASILI KWA MWILI HUO WA MAREHEMU
Umati unaosubiri mwili wa Nyawana umevunja rekodi!
Kadri muda uendavyo ndivyo watu wamezidi kufika ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo ya Gongoni, Tabora mjini. Hata hivyo mwili wake umechelewa kidogo kuwasili mjini hapa lakini watu wameendelea kujazana wakikaa juani bila taabu yeyote. Hii ni ishara kuwa watu wa Tabora walimkubali sana Nyawana ambaye wao walipenda kumwita Mamaa Nyawana au Jembe! kwani watu wapatao elfu moja wamejitokeza kushuhudia au kutoa heshima za mwisho kwa Nyawana.
Sheikh akitoa mawaidha mawili matatu kwa wahudhuriaji |
Voice of Tabora ( Vot fm 89.0fm) kurusha live shughuli za mazishi ya Nyawana Fundikira
Mac Denny akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa VOT fm 89.0 redio walipokuwa wakiwasilisha ubani wao kwa Baba mdogo wa marehemu Bw Adam Fundikira |
Fundi mitambo Dj Faster akiandaa urushaji Live shuhuli ya maziko ya Nyawana |
Gari la matangazo live la Vot fm 89.0 |
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakimsikiliza ustaadh nyumbani kwa Baba mkubwa wa marehemu Nyawana Gongoni, Tabora. |
SAFARI YA MWILI WA MAMAA NYAWANA FUNDIKIRA TOKA DAR KUELEKEA TABORA
Msanii wa kundi la taarabu la mashauzi classic Thabit Abdul akiwa amebeba jeneza la mwili wa marehemu msanii Nyawana Fundikila pamoja na wausika wengine kwa ajili ya kupereka kwenye gari iliyomsafirisha kwenda tabora kwa ajili ya maziko
Kisomo cha Marehemu Nyawana Leo Tabora!
Ndugu, Jamaa na Marafiki Wakiwa Katika Kisomo cha Marehemu Nyawana Leo Tabora
Shekhe Katika Kisomo cha Marehemu Nyawana Leo Tabora!
DJ Fimbo (aliyevaa prova ya njano)Mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha redio VoT FM ambacho marehemu alishawahi fanyia kazi
Ndugu, jamaa na marafiki katika wakati mgumu wa maombolezo
majonzi mazito
[Picha na mkalamatukio.blogspot.com]
Nyawana kuzikwa kesho Tabora!
NYAWANA |Mama wa matashititi enzi za uhai wake
MULARD | MUME WA ZAMANI WA NYAWANA [CHANZO CHA PICHA]
Mwanamuziki maarufu wa Taarabu marehemu Nyawana Fundikira anatarajiwa kuzikwa kesho mchana au jioni kutegemeana na uwasili wa mwili wa marehemu mkoani Tabora. Ambapo baada ya kufanyiwa yale yote muhimu mkoani Dar mwili wake utasafirishwa kwa njia ya gari mpaka mjini Tabora kwa mazishi.
Mazishi yake yatafanyika kijijini kwao Itetemya yalipo makaburi na Ikulu ya familia ya kichifu ya Fundikira na Mtemi Isike Mwana Kiyungi. Nyawana Fundikira ambaye ameacha watoto wawili Said Murad (22) na Queen Murad (15) ambao alijaliwa kuwapata katika ndoa yake yake ya kwanza na Bw. Omar Khamis Murad (pichani). Murad mwanamichezo maarufu sana mjini Tabora ni meneja wa uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)