mkalamatukio

Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora


Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.
Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.



Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum.
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.

Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
Team Irene wakifuatilia mchakato
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN central zone

Tabora Wanufaika na Mafunzo ya ULINGO – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP)

ULINGO WA WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na UNWomen.

Mafunzo hayo yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo pale Student Center.
t-wcp (2)
Wanufaika na watia nia za kugombea nafasi mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wakifuatila mafunzo hayo yaliyotolewa na Hilda Stuart Dadu kutoma TWCP
t-wcp (3)
Watia nia wakichukua kumbukumbu za mafunzo hayo mapema leo hii
t-wcp (4)
Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo akifuatilia jambo kwa umakini.
t-wcp (5)
Wakti mafunzo yakiendelea na maswali yakiulizwa kwa ufafanuzi zaidi kutoka kwa wawezeshaji.
t-wcp (6)
Hilda Stuart Dadu wa ULINGO (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati mafunzo yakiendelea.
t-wcp (1)
t-wcp (7)

t-wcp (8)
Hawa, mgombea wa ubunge wa viti maalumu kwa tiket ya chadema akiuliza swali kwa muwezeshaji t-wcp (12)

t-wcp (11)
Muwezeshaji Emmiliana akitoa zoezi kwa wanafunzi wake ili kukazia zaidi kile walichofundishwa na kukifanya kwa vitendo.
t-wcp (13)
Miongoni mwa wanakundi wakijadiliana jambo baada ya kupewa zoezi na muwezeshaji wa mafunzo.
t-wcp (10)

t-wcp (9)
Picha ya pamoja ya wanufaika wa mafunzo ya ULINGO na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watia nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mafunzo hayo yamekuja wakati huu ambao ndiyo haswa muda mwafaka wa uchaguzi mkuu wa ngazi za udiwani, ubunge na Urais.

Wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM Tabora mjini wajinadi Itetemia!

Mh Aden Rageh kushoto na Bandora Mirambo wakifuatilia mkutano.

Makada wa CCM Wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM Tabora mjini leo hii mchana walijinadi kwa wapiga kura wao wa kata ya Itetemia, ambao wakiungana na wengine kwa jimbo la Tabora mjini watapiga kura siku ya tar 1/8/2015kumchagua mmoja wao ili aikiwakilishe chama hicho kayika uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Wagombea hao ambao kila mmoja wao alijieleza mbele ya wajumbe hao kwa dakika 5 walitoa maelezo yao mbele ya wajumbe ya kuwa wakichaguliwa wataboresha hali za maisha, uchumi, elimu na kilimo.

Siku ya kesho wagombea hao wataelekea Ntalikwa ambako pia watajinadi kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu katika kuelekea kura za maoni mapema mwezi ujao.
Bandora Mirambo akibadilishana mawazo na mgombea mwenzie Emmanuel Mwakasaka mara baada ya kujinadi.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Itetemia (Kushoto) Rashid Kamanda Tall(kiongozi wa msafara) na katibu wa CCM kata ya Itetemia.




Wajumbe
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wilaya ambao watapiga kura tarehe 1/8/2015 kumchagua mgombea wa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.
Bw  Bandora Salum Mirambo.
Bw Emmanuel Mwakasaka
Amon Mkoga.
Mh Aden Rageh.
Bw William Masubi Chimaguli.
Ramadhani Mauli Mkangara mgombea akijinadi na kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum.
Viongozi wa mkutano toka kushoto ni Rashid Tall, Ali Kazikupenda na Mohamed Kazete.



Mkaziwa Kipalapala Thomas Mwiniko aliyeuliza baadhi ya maswali kwa wagombea.
Amon Mkoga kushoto na Salum Mkangara wakifuatilia mkutano
 Habari na picha na mkalamatuio blog