mkalamatukio

JK ALOPOKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UHOLANZI JIJIJINI THE HAGUE

Sonigwe(red top) akisubiri kusalimiana na Mh Rais Kikwete alipokutana na wa Tazania wanaoishi Holland
 Watanzania waishio Uholanzi walikusanyika siku ya Jumatatu Juni 9, 2015 katika hoteli ya Crowne Plaza jijini The Hague kukutana na kumsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa nchini humo kwa mwaliko wa Mfalme Willem-Alexander
 Wajumbe walioongozana na Rais Kikwete katika ziara hiyo
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Ujumbe wa Rais Kikwete
 Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. William Masilingi akimkaribisha mgeni
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Wadau wa Uholanzi wakiwa na furaha kumuona JK
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi wakiimba wimbo wa Taifa

  Mama Balozi na wageni wakiimba  wimbo wa Taifa
 Rais Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi

 Wadau wa Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 DJ Khatibu akikorofisha mambo

  Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi wa Zanzibar Mhe. Ramadhani Abdalla Shaban akitambulishwa
 Sehemu ya wageni waalikwa
 Wafanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania The Hague
 Baadhi ya maafisa waandamizi wa Tanzania
  Sehemu ya umati wa Watanzania waishio Uholanzi
 Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Uholanzi akisoma risala yao
 Sehemu ya ujumbe wa Rais Kikwete
 Sehemu ya ujumbe wa Rais Kikwete
 Mtanzania anayeendesha shirika lisilo la kiserikali linalotoa misaada Tanzania akitambulishwa
  Mtanzania anayeendesha shirika lisilo la kiserikali linalotoa misaada Tanzania akitambulishwa
  Mtanzania anayeendesha shirika lisilo la kiserikali linalotoa misaada Tanzania akitambulishwa
 Rais Kikwete akimpongeza kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania bada ya kusoma risala
 Meza kuu ikifurahia muziki wa Tanzania ulipokuwa unaporomoshwa kuchagiza hafla hiyo
  Meza kuu ikifurahia muziki wa Tanzania ulipokuwa unaporomoshwa kuchagiza hafla hiyo
 Wajumbe wa kamati ya maandalizi wakipeleka zawadi kwa Rais Kikwete
  Meza kuu ikifurahia muziki wa Tanzania uliokuwa unaporomoshwa kuchagiza hafla hiyo
  Zawadi kwa Rais Kikwete
 Balozi Masilingi akielezea zawadi maalumu kwa Rais Kikwete
  Rais Kikwete akipokea zawadi maalumu ya Watanzania waishio Uholanzi toka kwa Balozi Masilingi
  Rais Kikwete akipokea zawadi maalumu ya Watanzania waishio Uholanzi toka kwa Balozi Masilingi
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa Watanzania Uholanzi
  Picha ya Kumbukumbu
  Rais Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi
  Rais Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi
  Rais Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi
 Rais Kikwete akipata picha za kumbukumbu na Watanzania waishio Uholanzi

RC GAMA AKANA KUFANYA UDALALI WA ARDHI.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza na wanahabari (hawako pichani) juu ya tuhuma zilizoibuliwa bungeni dhidi yake.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa na mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga katika mkutano huo na wanahabari.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ya habari mkoani Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SIKU moja baada ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kumlipua mkuu wa Mkoa wa , Leonidas Gama kwa madai ya kufanya udalali na ufisadi katika uporaji wa ardhi ya wananchi, mkuu huyo amejitokeza mbele ya wanahabari na kukanusha tuhuma hizo.

Katika utetezi wake Gama alirejea kauli yake aliyoitoa miaka sita iliyopita ya kuwa yeye ni msafi huku akiitupia mzigo halmashauri ya wilaya ya Rombo tuhuma za kiasi cha sh Mil 500 zilizotajwa kutolewa wawekezaji wa Kichina kama fidia kwa wananchi katika ardhi kilipojengwa kiwanda cha kutengeneza Saruji.

Alisema tuhuma zilizotolewa Bungeni dhidi yake si za kweli na kwamba ni za kisiasa huku akitaja sababu ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni kutokana na juhudi zake za kupambana na Pombe haramu katika wilaya ya Rombo pamoja na Urejeshwaji wa wafanyabiashara katika soko la kati la mjini Moshi.

“Nataka niwaambie hii ni siasa,zipo issue nyingi zilizochangia kuibuka kwa haya mambo ,lakini nawaambieni mbili tu,Issue ya kwanza Pombe Rombo,na msimamo wangu juu ya Pombe Rombo ndio imezaa hii,la pili ni soko la Moshi mjini,watu wana agenda zao kwenye soko hilo ,wananchi wamerudi pale ,imewaumiza watu.”alisema Gama.

“Watu walitaka Pombe ya Gongo iharalishwe,mimi nimesema hadharani anayetaka pombe ya Gongo ihararishwe si mwenzetu mu mshughulikie kwa maana si mwenzetu sasa hili limeleta nongwa”aliongeza Gama.

Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo ,Gama amekiri mtoto wake aliyetajwa kwa jina la Mayunga Leonidas Gama kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda hicho huku akihakikisha kiwanda hicho kinajengwa katika mkoa wa Kilimanjaro badala ya Bagamoyo kama walivyo pendelea
wawekezaji hao.

“Kiwanda cha saruji kinachojengwa pale Rombo, nilikuwa na uwezo wa kukipeleka popote ninapotaka mimi, lakini mimi binafsi ndiye niliyefanya juhudi kiwanda kile kijengwe Kilimanjaro, mimi binafsi na wala sio mtu mwengine, nimefanya juhudi hizo kwa lengo la kuongeza
ajira kwa wananchi na kuinua uchumi wa mkoa huu”, alisema Gama .

“Historia ya Kiwanda hiki iko wazi, na  nililipeleka hadi kwenye kikao cha ushauri wa mkoa (RCC),na naomba nieleweke kwamba, ni juhudi zangu na za mtoto wangu, nilitamka kwenye kikao kile na wala sikuficha, mtoto wangu ambaye ametajwa yeye ana rafiki yake wa kichina, wala si kweli kwamba hii kampuni mimi nimekwenda kuichukua China kwa gharama za serikali” aliongeza Gama.

Alisema katika kikao hicho (RCC), Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walishiriki katika kikao hicho na kwamba baada ya mvutano ndipo makubaliano yakawa kiwanda kijengwe wilaya ya Rombo .

“Toka siku ile mimi kama mkuu wa mkoa nikakabidhi madaraka wilaya yaRombo,kwa hiyo shughuli zote za ujenzi ,shughli zote za kutafuta viwanja zilifanywa na halmashauri ya wilaya ya Rombo na sio Gama”alisema Gama.

Alisema waliolipa fidia na kununua viwanja ni halmashauri ya wilaya na hata eneo kilipojengwa kiwanda hicho ni mali ya halmashauri ya wilaya ya Rombo na si cha mwekezaji kama inavyoelezwa .

“Nimeelezwa kweye tuhuma kuwa nimepewa milioni 500,hii ni hadithi ya kisiasa ,sijapokea kiasi hicho cha fedha wala sikijui,hata hizo hisa 20,000 nilizoambiwa ninazo kwa kweli sina ,kama ningekuwa nazo ni haki yangu kwa sabau sijavunja sharia lakini sin ahata hisa moja.”alisema
Gama.

“Swala mtoto wangu kuwa na hisa si dhambi na ni haki yake kisheria,kwa sababu yeye ndiye aliyewatafuta hao watu na ni rafiki zake ,wala si mimi niliyewaleta kama amenunua hisa huko ni hiari yake,mimi sina hisa kama Gama,sijapokea milioni 500 kama gama,mimi si dalali na kama ni udalali wa ardhi hiyo itakuwa ni halmashauri ya wilaya ya Rombo na si
gama.”alisema Gama.

Alipoulizwa endapo kama halmashauri ya wilaya ya Rombo itakuwa inamiliki sehemu ya hisa katika kampuni hiyo kutokana na utolewaji wa ardhi yake ,Gama alisema wenye majibu ni halmashauri ndio watakuwa wanajua ni mikataba gani wameingia na wawekezaji hao.

Kuhusu eneo la Uwekezaji wa soko la Lokolova, Gama alisema ameshangazwa na kauli za kuwa yeye ni fisadi wa ardhi katika eneo hilo wakati makubaliano ya kuanzishwa kwa soko la kimataifa na mji mdogo wa kibiashara ulipitishwa katika kikao cha RCC ambacho pia Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema alihudhuria na kusifia mpango huo.

Sakata la Kiwanja cha Mawenzi, Gama alisema yeye kama mkuu wa Mkoa, alichokifanya ni kuishauri Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kufuata Sheria za umilikishwaji wa Ardhi ili kuepusha Halmashauri kufilisiwa kwa kukiuka taratibu.

Juzi wakati akiwasilisha bungeni maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti yay a wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2015/2016,msemaji mkuu wa kambi hiyo Halima Mdee alimrushia tuhuma Gama za kuhusika katika kutumia fedha za serikali kwenda nchini China kutafuta watu wawili wanaotajwa kama wawekezaji.

Katika taarifa hiyo Mdee alidai katika hali isiyo ya kawaida na ya kushangaza watu hao katika ardhi iliyokwisa lipiwa fidia kwa fedha za umma ,ilianzishwa kampuni binafsi ya Jun Tu 

Mwisho.

MSAFARA WA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA WAWASILI WILAYANI KAHAMA USIKU HUU KWA BASI,KESHO KUANZA RASMI ZIARA YA KAGERA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kamati ya Ulinzi na Usalama usiku huu ndani ya wilaya Kahama mkoani Shinyanga tayari kwa mapumziko,ambapo kesho ataianza rasmi ziara yake katika kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera,Ndugu Kinana ndani ya Biharamulo atapokea taarifa za chama na Serikali na baadae kuzungumza na Wafugaji wa kanda ya Ziwa (Mikoa ya Geita,Kagera,Mwana na Shinyanga)  na baadae kueleke Bukoba mjini.

Ndugu Kinana amewasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha uhai wa chama,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Nzega usiku huu Dkt.Hamis Kingwangalla,mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho usiku huu wilayani Nzega mkoani Tabora akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana pia aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kujenga chama na nchi kwa ujumla
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na washabiki wa chama hicho wilayani Nzega usiku huu kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha chama na nchi kwa ujumla
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akimshukuru Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla kwa mapokezi mazuri wilayani humo,ndugu Kinana amewasili wilayani humo mnamo majira saa nne usiku na ushehe akitokea jijini Dar kwa basi maalum akiwa emeambatana na ujumbe wake akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
 Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla  akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana .

PICHA NA MICHUZI JR.KAHAMA.

Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni huru na haki kwa yeyote kugombea asema Mh Samuel Sitta!

Moja ya kikundi cha ngoma za kimila cha Waswezi wakimsikiliza Mh Samuel Sitta.
Mh Samuel John Sitta ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa Mtemi wa himaya ya Unyanyembe Mtemi Said (Swetu) Fundikira aliyetawala kuanzia mwaka 1917 mpaka mwaka 1927 ni mwanasiasa mkongwe kwa siasa za Tanzania jana akijibu swali la mwandishi wa habari toka CG Fm 89.5 ambaye aliuliza "kwa kuwa tayari wana Ccm, 8 washatangaza nia ya kutaka kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nini wewe usingeamua kujiunga na mmoja wao ili kumuongezea nguvu, badala ya na wewe kutangaza nia? Mh Sitta akajibu "Kila mtu anajipima yeye mwenyewe uwezo wake kisha anaamua cha kufanya, vile vile urais ni huru na ni haki kwa mtu yeyote kugombea. Mdogo wangu Kigwangwala na yeye ana mpango wa kugombea, ni jambo zuri. Aidha Mh Sitta akaongeza kusema "lakini hata wewe ndugu mwandishi ungeweza kugombea, nashangaa sijui kwa nini hugombei" Jibu hili liliwafanya watu wengi waliohudhuria hapo Itetemia jana kuangusha vicheko.
Kikundi cha kina mama wakicheza na kuimba
Mheshimiwa Sitta akisalimiana na baadhi ya watu waliofika Itetemia jana

Mzee Ifuma Abdallah akimsindikiza Bibi Kagori Said Fundikira (Mama mzazi wa Mh Samuel Sitta) na kulia ni Agnes Kijoh Sitta(binti ya Mh Sitta)
Kushoto ni Kefa Kijoh na Agnes Kijoh Sitta wakisalimia wageni
Habari na picha Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE

Mheshimiwa Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!

Mh Samuel Sitta akitangaza nia leo mchana Itetemia Tabora
Mheshimiwa Samuel Sitta leo hii alitangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitangaza nia yake hiyo mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.

Akieleza sababu tano zilizomfanya atangaze nia yake ambazo ni 

Mabango nayo yalikuwepo!

Mh Sitta akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora leo mchana.
Mh Magreth Sitta akisalimia wananchi wa Itetemia

1.Muungano
Toka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.

2. Mchakato wa katiba
Pamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.

Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba.
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini
Binafsi naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.

3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda
Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza  huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira  chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.

4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa
Rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.

5. Kuimarisha CCM kiuchumi
Chama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake  kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni "wafadhili" 

Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui

Agness Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia leo

Aidha Mh Sitta akijibu swali toka kwa mwandishi wa habari aliyeuliza "Mh Sitta unasemaje juu ya shutuma za waziri mkuu aliyejiuzuru wadhfa wake kuwa wewe na Mh Mwakyembe mlikuwa na wivu naye ndio maana mkamuonea mpaka ikabidi ajiuzuru? Mh Sitta akajibu "Bwana mwandishi kwa nini swali hilo humuulizi yeye mwenyewe aseme ni kipi alichoonewa? Mchakato wa uchunguzi ulifanyika mwaka 2008 mpaka sasa ni miaka 7 hivi sasa muda wote huu alikuwa wapi hata leo aseme alionewa? Jibu ambalo lilipelekea vicheko na vigerere toka kwa wananchi walioudhuria hafla hiyo. 

Mh Samuel Sitta apewa cheo cha Mwizukulu Mkulu (Mjukuu mkubwa) wa Utemi wa Unyanyembe!

Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira akiwatambikia Mh Magreth Sitta na Mh Samuel Sitta ambaye ni binamu yake kabla hajatangaza nia ya kugombea urais.

Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira leo hii asubuhi alimpa cheo cha Mwizukulu mkulu Mh Samuel Sitta katika kutambua safari yake ya kukiomba chama chake cha CCM kimpe ridhaa ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.
Mh Samuel Sitta akiwa na mkewe Mh Magreth Sitta wakisubiri kutambikiwa.
Mtemi wa Unyanyembe Msgata Fundikira akisisitiza jambo katika hafla fupi ya kumpa cheo Mh Samuel Sitta
Mtemi Msagata akimvika mgololoMh Sitta

Mtemi Msagata Fundikira, Mh Rageh, Mh Samuel Sitta na Mlinzi Mh Sitta wakitokea sehemu maalumu palipofanyika tambiko.
Picha na Habari na Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE