Mheshimiwa Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!
Mh Samuel Sitta akitangaza nia leo mchana Itetemia Tabora |
Akieleza sababu tano zilizomfanya atangaze nia yake ambazo ni
Mabango nayo yalikuwepo! |
Mh Sitta akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora leo mchana. |
Mh Magreth Sitta akisalimia wananchi wa Itetemia |
1.Muungano
Toka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.
2. Mchakato wa katiba
Pamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.
Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba. |
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini |
3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda
Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.
4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa
Rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.
5. Kuimarisha CCM kiuchumi
Chama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni "wafadhili"
Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui |
Agness Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia leo |
Aidha Mh Sitta akijibu swali toka kwa mwandishi wa habari aliyeuliza "Mh Sitta unasemaje juu ya shutuma za waziri mkuu aliyejiuzuru wadhfa wake kuwa wewe na Mh Mwakyembe mlikuwa na wivu naye ndio maana mkamuonea mpaka ikabidi ajiuzuru? Mh Sitta akajibu "Bwana mwandishi kwa nini swali hilo humuulizi yeye mwenyewe aseme ni kipi alichoonewa? Mchakato wa uchunguzi ulifanyika mwaka 2008 mpaka sasa ni miaka 7 hivi sasa muda wote huu alikuwa wapi hata leo aseme alionewa? Jibu ambalo lilipelekea vicheko na vigerere toka kwa wananchi walioudhuria hafla hiyo.
Mh Samuel Sitta apewa cheo cha Mwizukulu Mkulu (Mjukuu mkubwa) wa Utemi wa Unyanyembe!
Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira akiwatambikia Mh Magreth Sitta na Mh Samuel Sitta ambaye ni binamu yake kabla hajatangaza nia ya kugombea urais. Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira leo hii asubuhi alimpa cheo cha Mwizukulu mkulu Mh Samuel Sitta katika kutambua safari yake ya kukiomba chama chake cha CCM kimpe ridhaa ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao. |
Mh Samuel Sitta akiwa na mkewe Mh Magreth Sitta wakisubiri kutambikiwa. |
Mtemi wa Unyanyembe Msgata Fundikira akisisitiza jambo katika hafla fupi ya kumpa cheo Mh Samuel Sitta |
Mtemi Msagata akimvika mgololoMh Sitta |
Mtemi Msagata Fundikira, Mh Rageh, Mh Samuel Sitta na Mlinzi Mh Sitta wakitokea sehemu maalumu palipofanyika tambiko. |
Picha na Habari na Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE
Maandalizi ya hafla ya Mh Samuel Sitta kutangaza nia ya kugombea urais yaiva!
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wa mkoani Tabora na wa nje ya mkoa wakiwasili Itetemia Hatimaye Mh Samuel Sitta leo atatangaza nia kijijini kwao Itetemia ambako atatambikiwa kimila na kupewa cheo cha Mwizukulu mkulu ikimaanisha (mjukuu mkubwa) Samuel Sitta ni mjukuu wa mtemi wa zamani wa Unyanyembe Marehemu Mtemi Saidi Fundikira baada ya kutambikiwa hapa Ikulu ya Unyanayembe ndipo atatangaza nia ya kuomba kuteuliwa na CCM ili agombee urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Samuel Sitta ni mwanasiasa mkongwe hapa nchini Tanzania. Matangazo ya hafla hii yanarushwa moja kwa moja na VOT FM 89.0 ya mjini Tabora pamoja na Radio one stereo. |
Wanyanyembe wakiwasili katika Ikulu yao Itetemia |
Baadhi ya viongozi wa ngoma ya Uswezi |
Apolo, Salu SECURITY na Adam Fundikira wakiwa Itetemia |
Mbunge wa Tabora mjini Mh Aden Rageh akiwasili Itetemia |
Mh Rageh akikaribishwa na kiongozi wa CCM mkoa wa Tabora |
Waswezi |
Ngoma za Lugaya |
Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira |
Wayege wakicheza ngoma |
Habari na picha kwa hisani ya
Mkala Fundikira wa TBN central zone
AKI NA UKWA WA BONGO WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWENYE TASNIA YA FILAMU
Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao
Aki na Ukwa wa Bongo wakipiga kazi ...
Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels
Wasanii wa komedi maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.
Wakizungumza na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa' wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.
Baadhi ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali zaidi zipo katika matengenezo.
Mbali na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza na kuimba.
"Kwa sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.
Pia kupata taarifa zaidi za wasanii wa Komedi Tanzania tembelea mtandao wao wa www.komedizonetz.blogspot.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)