Maandalizi ya hafla ya Mh Samuel Sitta kutangaza nia ya kugombea urais yaiva!
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wa mkoani Tabora na wa nje ya mkoa wakiwasili Itetemia Hatimaye Mh Samuel Sitta leo atatangaza nia kijijini kwao Itetemia ambako atatambikiwa kimila na kupewa cheo cha Mwizukulu mkulu ikimaanisha (mjukuu mkubwa) Samuel Sitta ni mjukuu wa mtemi wa zamani wa Unyanyembe Marehemu Mtemi Saidi Fundikira baada ya kutambikiwa hapa Ikulu ya Unyanayembe ndipo atatangaza nia ya kuomba kuteuliwa na CCM ili agombee urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Samuel Sitta ni mwanasiasa mkongwe hapa nchini Tanzania. Matangazo ya hafla hii yanarushwa moja kwa moja na VOT FM 89.0 ya mjini Tabora pamoja na Radio one stereo. |
Wanyanyembe wakiwasili katika Ikulu yao Itetemia |
Baadhi ya viongozi wa ngoma ya Uswezi |
Apolo, Salu SECURITY na Adam Fundikira wakiwa Itetemia |
Mbunge wa Tabora mjini Mh Aden Rageh akiwasili Itetemia |
Mh Rageh akikaribishwa na kiongozi wa CCM mkoa wa Tabora |
Waswezi |
Ngoma za Lugaya |
Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira |
Wayege wakicheza ngoma |
Habari na picha kwa hisani ya
Mkala Fundikira wa TBN central zone
AKI NA UKWA WA BONGO WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWENYE TASNIA YA FILAMU
Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao
Aki na Ukwa wa Bongo wakipiga kazi ...
Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels
Wasanii wa komedi maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.
Wakizungumza na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa' wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.
Baadhi ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali zaidi zipo katika matengenezo.
Mbali na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza na kuimba.
"Kwa sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.
Pia kupata taarifa zaidi za wasanii wa Komedi Tanzania tembelea mtandao wao wa www.komedizonetz.blogspot.com
NAIBU KAMANDA WA UCCM WILAYA YA MOSHI VIJIJINI INNOCENT MELLECK ATOA MSAADA WA KITI CHA WALEMAVU CHA BAISKELI KWA MTOTO FELISTA SHIRIMA
Melleck alikabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa mtoto Felista kwa ajili ya kusaidia wakati wa kwenda shuleni. |
Mama mzazi wa mtoto Felista Shirima akieleza kwa uchungu namna ambavyo mtoto wake alivyopata ulemavu wa kudumu. |
Babu wa mtoto Felista,Anold Shirima akiwasilisha ombi kwa jamii la kupata wakili kwa ajili ya usikilizwaji upya wa kesi dhidi ya watu waliosababisha ajali ya mtoto huyo. |
Naibu Kamanda wa jumuiya ya vijana wa CCM(UVCCM) Innocent Melleck akizungumza mara baada ya kutembelea familia ya mtoto Felista wa kijiji cha Rauya Marangu wilaya ya Moshi vijijini. |
Baadhi ya atoto na ndugu wengine waliofika nyumbani kwa mtoto huyo. |
Mellecky pia alikabidhi Pempers kwa ajili ya mtoto huyo. |
Familia na wanandugu wngine wa mtoto Felista wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck mara baada ya kukabidhi msaada wa baiskeli . |
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CHADEMA ,JAFARY MICHAEL AFUNGUA MATAWI MAPYA MOSHI
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema na meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi katika kata ya Longuo mjini Moshi. |
Ofisi mpya ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Longuo B . |
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema taifa na meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael akikata utepe kufungua ofisi mpya ya kata ya Longuo B. |
Meya Michael akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufungua ofisi ya kata ya Chadema. |
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema akitia saini katika kitabu cha wageni wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Longuo B. |
Diwani wa kata ya Longuo B,Ray Mboya akitia saini katika kitabu hicho. |
Baadhi ya makada wa Chadema manispaa ya Moshi wakishuhudia zoezi hilo. |
Ofisi mpya ya Chadema kata ya, Longuo
manispaa ya Moshi ikafunguliwa rasmi. Na Dixon Busagaga wa globu ya Jamii kanda ya Kasakazini. |
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)