mkalamatukio

UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA


DSC_0048
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akisalimiana na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya Mbogwe, Geita. Kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha na Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla na wa pili kushoto ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi.

Na Zainul Mzige wa modewjiblog
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.
Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.
Misaada hiyo kwa pamoja ilikabidhiwa Jumamosi iliyopita katika halfa ambaye mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
Majaliwa alishuruku UNFPA kwa msaada huo na kutaka utumike vizuri ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
“ Nimeona vifaa vya hospitali vingi na vya gharama kubwa, sasa ni wajibu wetu kuvitunza na kuvitumia vizuri. Mfano gari tu limegharimu shilingi milioni 80. Huu ni msaada mkubwa sana na kwa niaba ya serikali nawashukuru sana UNPFA, tutaendelea kushirikiana”, alisema Majaliwa .
Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwaagiza vingozi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa gari hilo linatumika kusafirisha wagonjwa tu na sio vinginevyo.
DSC_0062
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.

“ Gari hili litumike kwa matumizi ya wagonjwa tu. Sitegemei kusikia kuwa linapeleka wafanyakazi sokoni kununua nyanya. Na Mkurugenzi atenge bajeti ya mafuta ya gari hili muda wote”, aliagiza Majaliwa.
Hafla ya makabidhiano ya misaada hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya siku ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa Fistula duniani yaliyofanyakia kitaifa katika viwanja vya shule ya msingi Masumbwe katika Wilaya ya Mbogwe , Mkoani Geita.
Akizungumuza katika hafla hiyo Mwakilishi msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dkt. Rutosha Dadi alisema msaada wa vifaa walivyotoa utasadia kumaliza tatizo la Fistula na kuboresha huduma zingine za afya .
“ Tumefanya ukarabati mkubwa sana katika jengo la upasuaji na kutoa vifaa vya kisasa kama vile Ultrasound”, alisema Dkt. Dadi.
DSC_0072
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha (wa nne kulia) akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na umati wa wakazi wa Mbogwe waliokusanyika kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa miradi ya AMREF, kanda ya ziwa Dkt. Awene Gavyole, Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, Katibu Tawala wa mkoa wa Geita, Charles Palanjo, mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita, Joseph Kisalla, Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon pamoja na Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0204
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Mbogwe mkoa wa Geita.
IMG_1150
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akisisitiza jambo wakati wa kutoa salamu za Umoja wa Mataifa.
DSC_0149
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla akizungumza na wakazi wa Mbogwe ambapo aliwataka kufika katika vituo vya afya vilivyokaribu na makazi yao kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Fistula pindi wanaonapo dalili na moja kwa moja kuwasiliana na Hospitali yake inayotoa huduma za matibabu bure ikiwemo usafiri na malazi mpaka mgonjwa anapopona na kumrejesha anakoishi.
IMG_1089
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon akitoa salamu za Vodacom ilivyobega bega katika kupamba na ugonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/- kutoka Taasisi ya Vodacom Foundation kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa Fistula nchini wakati wa maadhimisho yanayofanyika kila mwaka Mei 23.
DSC_0248
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon, kwa niaba ya hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Fistula nchini wakati wa maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita mwishoni mwa wiki, Katikati ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla.
DSC_0254
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- kwa Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla (kushoto) na anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.
DSC_0182
Bi. Esther Ernest akitoa ushuhuda wake baada ya kuteseka na ugonjwa wa Fistula kwa takribani miaka 8 na jinsi jamii ilivyomnyanyapaa akiwemo mume wake hadi alipopatiwa matibabu na kupona kabisa hali iliyompelekea kurudisha furaha na nuru katika uso wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0928
Kikundi cha maigizo cha Mrisho Mpoto kikitoa elimu kwa njia ya maigizo jinsi Wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wanavyonyanyapaliwa na waume zao na kudhalilishwa kwa jamii ikiwemo kuitwa majina ya kila aina kutoka na kutokwa na haja ndogo muda wote bila breki.
IMG_0947
Mwigizaji wa kikundi cha sanaa za maigizo cha Mrisho Mpoto akilia kwa uchungu kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula na kunyanyapaliwa na mumewe wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0969
Msanii mahiri wa sanaa ya kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akimliwaza Mwanamke anayenyanyapaliwa na mumewe kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula ambao unatibika bure kabisa bila gharama yoyote na Hospitali ya CCBRT.
IMG_1006
Mume wa mwanamke anayeumwa Fistula wakisoma vipeperushi vya CCBRT vinavyotoa elimu, dalili na nini cha kufanya pindi unapojigundua ni Fistula pamoja na jirani yake wakati wa mchezo wa maigizo kwenye maadhimisho hayo.
IMG_1009
Mrisho Mpoto akiendelea kutumia sanaa ya maigizo kuelemisha umati wa wakazi wa wilaya ya Mbogwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_1030
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kushoto) na Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita, Dkt. Joseph Kisalla wakifuatilia igizo la unyanyapaa kwenye jamii kwa wanawake wanaougua Fistula wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0170
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifurahi jambo kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0235
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza Balozi wa Fistula CCBRT, Elizabeth Jacob na kumkabidhi pesa taslimu Sh. 20,000/- kama motisha ya kazi anazofanya za kuwasafirisha wagonjwa wa Fistula jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
DSC_0238
Balozi wa Fistula CCRT, Elizabeth Jacob akionyesha pesa alizokabidhiwa kama zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0241
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza na kumkabidhi pesa taslimu sh. 100,000/ kama motisha ya kazi anazofanya za kuelimisha jamii kwa kutumia sanaa na maigizo Mrisho Mpoto aliyekuwa akisheresha sherehe hizo.
DSC_0023
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla ( kushoto) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) wakimuangalia mtoto Nyambole Kulubone mwenye tatizo la mdomo wa Sungura akiwa amebebwa na mama yake Mariam Sanda (22) Mzazi huyo aliyehudhuria katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula aliahidiwa na Bi. Haika Mawalla (kushoto) mtoto wake atatibiwa bure katika hospitali CCBRT baada ya kusikia matangazo jirani na eneo liliofanyika sherehe hizo ambapo kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita.
DSC_0025
Mariam Sanda (22) akiwa amembeba mwanae mwenye mdomo wa Sungura.
DSC_0098
Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbongwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_0958
DSC_0101
IMG_0897
IMG_0891
IMG_1359
Burudani kutoka kwenye kikundi cha Mrisho Mpoto.
IMG_1393
DSC_0272
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Petr Shilogile (kushoto) akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa uliofadhiliwa na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania na ujenzi kusimamiwa na AMREF kabla ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0275
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua cha jiwe la msingi huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi (kulia) akishuhudia tukio hilo.
DSC_0277
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi.
DSC_0281
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akishuhudia tukio hilo.
DSC_0282
Sasa limezinduliwa rasmi.
DSC_0287
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile (kulia) akitoa maelezo kwenye chumba cha kujifungulia kina mama kilichowekwa vifaa vyote muhimu kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0289
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0318
Wafadhali wa ujenzi na vifaa kwenye kituo hicho Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa baada ya kuzinduliwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile.
DSC_0340
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akielezea changamoto waliozokuwa nazo hapo awali za kipimo cha "Ultra sound" kilichonunuliwa na UNFPA ambacho hivi sasa kitapatikana kituoni hapo kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0360
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0362
Mh. Kassim Majaliwa na Dkt. Rutasha Dadi wakipiga makofi.
DSC_0373
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akijaribu gari hilo.
DSC_0386
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akitoa angalizo la matumizi mabovu kwa DED wa Mbogwe na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya.
DSC_0388
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi funguo za gari hilo la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, Abdala Idd Mfaume.
DSC_0411
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mara baada ya makabidhiano hayo.
DSC_0421
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Muhanga wa Fistula, Bi. Ester Ernest (walioketi kulia), Balozi wa Fistula CCBRT, Bi. Elizabeth Jacob (wa pili kushoto), Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Palanjo (kushoto) na waliosimama kutoka kushoto ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, MC pamoja na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.

(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

UNESCO yasisitiza upendo kwa watoto wenye ualbino!


      DSC_0945
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akiambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (kushoto) walipotembelea shule msingi Mitindo ya watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kulia ni Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO Tanzania, Bi. Annica Moore.
Na Modewjiblog team

Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO)Tanzania, Zulmira Rodrigues amesisitiza umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ulemavu wa ngozi katika jamii baadala ya kuwatenga .Zulmira alisema hayo alipotembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi ya Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza mwishoni mwa juma
Shule hiyo ya serikali ina wanafunzi zaidi ya 1000 wakimo wenye ulemavu 202 .Kati yao 81 ni wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wanahifadhiwa na serikali katika shule hiyo maasa 24 kufuatia wimbi la mauaji la watu wenye ulemavu wa ngozi katika mikoa ya kanda ya ziwa .Hata hivyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania alionekana kupatwa huzuni kubwa kutokana hali ya maisha ya watoto hao .“ Nimehuzunika sana (I am so sad). Sio tabia ya watu wa Afrika kuwatenga watu wanyonge (weak people)”alisema huku akitokwa na machozi mara baada ya kuwatembelea watoto hao na kuongea nao pamoja na uongozi wa shule hiyo.Alisema ni muhimu watoto hao wenye ulemavu wa ngozi kuwa wanavaa nguo za mikono mirefu ili kuwakinga na jua kwa ajili ya kulinda afya zao.Hata hivyo Zulmira alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kutoa wito kwa wadau wote kuunga mkono juhudi hizo.
DSC_0955
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Katika ziara hiyo, Zulmira alikuwa amefuatana na mbunge wa viti maalum anayewakilisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) Mh. Al shaymaa Kwegyir. Mbunge huyo pia alisema kitendo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kukosa malezi na mapenzi ya wazazi ni changomoto kubwa iliyopo kwa sasa.
Alisema ni jukumu la watu wote kulinda na kusadia kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. “Ufumbuzi wa matatizo ya wetu wenye ulemavu wa ngozi sio kazi ya serikali tu, ni jukumu la kila mtu”,mbunge huyo alisisitiza. Aliahidi kuwasilisha bungeni baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi walemavu waliopo katika shule hiyo ya Mitindo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kurwa Ng’hwelo alisema serikali inatumia zaidi ya shilingi milioni 10 kuwa ajili ya mahitaji ya chakula kwa wanafunzi wote wenye ulemavu wapatao 202 kila mwezi. Shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wanaosadia wanafunzi hao walemavu.
DSC_0968
Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo akitoa maelezo ya idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hapo ambao ni 202 huku 81 wakiwa na albinism kwa Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyetembelea shule hiyo kuangali changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0979
Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo akimwonyesha mazingira ya eneo la shule hiyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues aliyeambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
DSC_0989
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa kutwa wanaosoma katika shule ya msingi Mitindo mara baada ya kuwasili shuleni hapo akiwa ameambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
DSC_0993
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza na wanafunzi hao waliofurahia ujio wake.
DSC_0997
Pichani ni moja ya jengo lililojengwa na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
DSC_1009
Mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) akitoka bwenini kuelekea chumba maalum kwa ajili ya kujipatia chakula cha mchana katika shule ya msingi Mitindo huku akionekana kutembea kwenye jua kali pasipo na kuwa na nguo ndefu ya kufunika hadi mikononi kujikinga na mionzi ya jua inayopelekea kupata saratani ya ngozi.
DSC_1017
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism) ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akila chakula cha machana huku akijikuna kutokana na maumivu makali anayosikia ya majeraha ya mionzi ya jua iliyoharibu mikono yake na kubadilika rangi ambayo athari yake baadae ni saratani ya ngozi.
DSC_1025
Na hii ndio hali halisi ya binti huyu katika mikono yake kutokana na kutembea kwenye jua bila kusitiri mikono yake na nguo ndefu.
DSC_1026
+Baadhi ya watoto wa bweni wenye Albinism wakijipatia chakula cha mchana jikoni.
DSC_1043
Mtoto mwingine aliyeathiriwa na mionzi ya jua miguuni na kupelekea kubadilika rangi kuwa mwekundu kutokana na kukosa nguo ndefu za kujisitiri na mionzi ya jua... wakiendelea kujinoma na chakula cha mchana.
DSC_1033
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akionyesha uso wenye huzuni kubwa kutokana na mazingira magumu waliyonayo watoto hao shuleni hapo. Kushoto ni Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir aliyeambatana na Bi. Zulmira Rodrigues kutembelea shule hiyo. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo.
DSC_1068
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mitindo, Kalunde Cosmas alipofanya ziara fupi ya kutembelea shule hiyo na kujionea changamoto zinazowakibili watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).
DSC_1036
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akimwonyesha mwandishi wa modewji blog (hayupo pichani) majeraha ya kuungua na jua kwa mmoja wa watoto mwenye albinism shuleni hapo.
DSC_1053
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyekuwa akijipatia chakula cha mchana.
DSC_1073
Mdau Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha mchana mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo wa wazazi wake kwa kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika shuleni hapo.
DSC_1101
Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule ya msingi Mitindo alipowatembelea na Bi. Zulmira Rodrigues.
DSC_1106
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisaidiana na Mdau Semeni Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa shule ya msingi Mitindo.
DSC_1113
Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO, Bi. Annica Moore aliyeambatana na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (hayupo pichani) akifurahi jambo wakati akigawa zawadi ya juisi mmoja watoto wenye albinism shuleni hapo.
DSC_1119
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendelea na zoezi la ugwaji zawadi ya juisi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio wa shule ya msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza alipowatembelea mwishoni mwa juma akiwa ameambata na Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (hayupo pichani).
DSC_1085
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa macho wakijumuika na wenzao wenye ulemavu wa ngozi na masikio kujipatia chakula cha mchana.
DSC_1087
Mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism anayeonekana kukosa lishe bora inayostahili kutokana na umri wake ambapo modewjiblog imebaini kuwa mtoto huyu ana "Utapiamlo" kutokana na kukosa lishe hiyo bora. Dalili moja wapo ni tumbo lake kuwa kubwa na gumu.
DSC_1137
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnywesha juisi mtoto mdogo kuliko wote anayelelewa kwenye shule ya msingi Mitindo ya watoto wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi, macho na masikio alipofanyia ziara fupi mwishoni mwa juma mkoani Mwanza.
DSC_1144
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnyeshwa juisi mtoto menye ulemavu wa macho alipotembelea shule ya msingi Mitindo iliyopo wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
DSC_1160
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa na uso wa huzuni kutokana na mazingira ya watoto hao na kupelekea kumwaga machozi kwa uchungu yeye kama mama mwenye kuthamini upendo. Kushoto ni Mh. Al Shaymaa Kwegyir.
DSC_1163
Bw. Abdulaziz Mbegele wa kitengo cha Logistic kutoka UNESCO, akimnywesha juisi mtoto mwenye ulemavu wa macho wakati wa ziara hiyo na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.
DSC_1091
Mtoto alyefahamika kwa jina moja tu Kevin mwenye umri wa miaka 11 ambaye alifikishwa kwenye shule hiyo akiwa mdogo sana na wazazi wake kumtelekeza hadi leo huku akiwa hamjui mama, baba, mjomba, dada, kaka wala shangazi..... kisa amezaliwa na albinism....!
DSC_1097
Mtoto Kevin akipata "self" na mjomba wake mpya Zainul Mzige wa modewjiblog aliyeambatana na ugeni huo.
DSC_1202
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na waandishi wa habari na kutoa hisia zake kuhusiana na changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa nguvu na kusisitiza upendo kwa watu wenye albinism.
DSC_1195
DSC_1216
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)