mkalamatukio

Wajue top five wa vipaji Miss Dar Indian Ocean!

Shindano la urembo la Miss Dar Indian Ocean likiwa linakaribia, siku ya ijumaa  tarehe 23/5/2014 wapenzi wa tasnia ya urembo jijini Dar na wilaya zake walishuhudia mchuano mkali wa kugombea ushindi wa kipaji katika ukumbi wa Chichi hotel ambapo warembo watano kati ya 15, walifanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la kipaji zitakazofanyika siku ya kumtafuta Miss Dar Indian Ocean ambayo ni Jumamosi ya tarehe 7/6/2014 katika ukumbi huo huo maridhawa wa Chichi hotel. Onesho hilo lilihudhuriwa na kamati ya Miss Tanzania pamoja na Miss Tanzania 2012 Salha Israel, pamoja na wadhamini kama CXC na wengine wengi. Dalili zinaonesha show ya Miss Dar Indian Ocean itakuwa si mchezo kwani kwa onesho dogo tu la kipaji ukumbi na jukwaa vilipambwa vilivyo na kampuni maaurfu ya Vayle Springs. Mtandao huu ulipoongea na muandaaji wa shindano hilo Bibi Rahma Yusuf ambaye anaanda shindano hilo kupitia kampuni yake ya Rahmat Entertainments alisema kwa kujiamini "Hii ni trela tu muvi yenyewe ni tarehe 7June ukikosa show hiyo bora uhame mji" Onesho hilo la vipaji lilidhaminiwa na Chichi hotel.
Kutoka kushoto ni Suzzete Fetrick, Mary Amos, Sasha Deogratius, Camilla John na Getrude Massawe, hawa ndio walioingia fainali za Miss Dar Indian Ocean Talent show.
Judges: Kutoka kushoto ni jaji Hassan, Husna Sajent na Iddi Zonki
Kutoka kushoto ni muandaaji wa Miss Mwanza Bw Dotto, Yusuf Omari aka Boy George, Salha Israel na katibu wa Miss Tanzania Bw Bosco Majaliwa wakifuatilia kwa makini shindano la vipaji.

Picha zaidi za semina ya Redds Miss Tanzania!

Kulia ni wakala wa Redds Miss Njombe
Tunachukua notice
Tom Chilala mwenye shati jeupe na Khadija Kalili kushoto kwake


Hidan Ricco na Ephraim Makoye wa kamati ya Miss Tanzania

Kulia ni wakala wa Miss Singida 
Baadhi ya waandaji mawakala wakifuatilia semina kwa umakini
Muandaaji wa Redds Miss Temeke Bw Kisaka na William Malecela wa Blog ya wananchi.

Semina ya mawakala wa Redds Miss Tanzania yafanyika

Mkurugenzi wa Lino International inayoratibu shindano la Miss Tanzania Bw Hashim Lungenga akisisitiza jambo alipokuwa akifungua semina ya mawakala wa Miss Tanzania 2014.
Semina ya kuwafunda mawakala wa Redds Miss Tanzania 2014 ilifanyika kuanzia jana arehe 25/03/2014 katika Hoteli ya Regency ya jijini Dar es Salaam, semina hiyo ambayo hukutanisha kamati ya Miss Tanzania, mawakala na wadhamini hufanyika kila mwaka baada ya uzinduzi rasmi wa shindano hilo kubwa la urembo nchini. Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake baridi cha Redds Premium cold ndiye mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo mchakato wake huanzia katika vituo, wilaya, mkoa na hatimaye na shindano la Taifa yaani Redds Miss Tanzania
Kutoka kushoto ni katibu wa Miss Tanzania Bw Bosco Majaliwa, Mshauri wa ufundi Bw Ramesh Patel, Hashim Lundenga, Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa na mshindi wa pili wa shindano hilo.


Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa

Kutoka kushoto Bw Bosco Majaliwa, Ramesh Patel na Bw Hashim Lundenga
Wakala wa kituo cha Dar na Awetu wa gazeti la KIU

Baadhi ya mawakala wa Miss Higher Learning

Muandaaji wa Redds Miss Njombe, Miss Sylvia

Kutoka kushoto ni Miss Jacky, Tom Chilala wa star T na Khadija kalili wa Tanzania Daima





Mpigie kura Ally Baucha ashinde Kili Music Awards!

Msani machachari Ally Baucha ambaye kupitia wimbo wake Kelele aliomshirikisha Ally Kiba ameteuliwa kushiriki katika kinyang'anyro cha kugombea tuzo za Msanii anayechipukia ambapo amepewa namba 23 na vile vile amepewa namba 26 katika kugombea tuzo ya msanii bora mtumbuizaji wa kiume. Ili kumpigia kura Baucha fuata maelekezo hapo juu.

Mama Agnes Matle Ngula afariki leo asubuhi!

Bibi Agnes Matle Ngula enzi za uhai wake
Aliyekuwa naibu waziri wa fedha  Bw Venance Ngula leo hii asubuhi amempoteza mkewe Bibi Agnes Matle Ngula ambaye alikuwa akiugua kwa muda sasa. Mtoto wa kwanza wa marehemu Wali Francis Ngula anayeishi New Jearsey America anatarajia kuwasili jijini Dar kwa mazishi ya mama yake mpendwa siku ya Alhamisi. Tutaendelea kujuzana mipango ya mazishi hpa na kwingine. Mungu ailaze pema peponi roho ya mama yetu mpendwa Mama Agnes Ngula.
AMEN!
Bw na Bibi Venance Ngula wakiteta jambo enzi za uhai wa Bibi Agnes Matle Ngula
Mama Ngula akibandikwa mabusu na mwanae Wali Francis Ngula na mkewe Enika Kombe Ngula muda mfupi baada ya harusi yao mwaka juzi .
Mtoto wa mwisho wa mama Agnes, Nancy Ngula akiwa na marehemu 
Bibi Agnes Matle Ngula enzi za ujana wake.
Francis Wali Ngula
Habari na picha kwa hisani ya Francis na Nancy Ngula

Shabiki wa Liverpooll auawa kwa kumkejeli shabiki wa Arsenal!

Raha iliyoje 5-1????
Shabiki wa miaka mingi wa Liverpool Anthony Mutheiya alikufa muda mfupi baada ya firimbi ya mwisho katika mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal jumamosi iliyopita baada ya kuchomwa kwa kisu na shabiki wa Arsenal aliyetambulika kama David Mwangi ambaye anadaiwa alikimbia eneo la tukio Marethe Bar mjini Meru, Kenya ambapo wawili hao walitazama mchezo huo pamoja, ilisemekana Mutheiya alimkejeli Mwangi kupita kiasi na kwa muda mrefu juu ya matokeo ya mchezo huo ambapo Mwangi akashindwa kuvumilia na ndipo alipochomoa kisu na kumchoma nacho Mutheiya ambaye alikimbizwa hospitali lakini akafariki baadaye. 

Obama na Beyonce wazushiwa jambo!

Mtandao wa dailystar.co.uk wa nchini Uingereza ambao ni maarufu kwa habari za kidaku, leo hii umechapisha habari ilizodaiwa na mwandishi wa habari Mfaransa Paschal Rostain kuwa gazeti linaloheshimika nchini Marekani la Washinton Post linatarajiwa kuandika habari kuwa the most powerful man in the world, Rais wa Amerika Bw Barack Obama ana mahusiano ya kimapenzi na mwimbaji Byonce Knowles ambaye ni mke wa mwanamuziki Jay-Z. Rostain alikaririwa akisema "Unajua katika siku hizi kuna habari kubwa inatarajiwa kuchapishwa na gazeti la Washington Post kuwa Obama na Beyonce wana uhusiano usiofaa, na akaongeza "Dunia nzima italiongelea hili sana" 

Lakini msemaji wa gazeti hilo Wasington Post Bw Kriss Coratti alipoulizwa juu ya habari hiyo akasema hana habari yeyote juu ya hilo ila akaongeza Rais Obama na mkewe wamekuwa na matatizo hivi karibuni, "Lakini sijui zaidi ya hapo"

Baada ya yote hayo Paschal Rostain sasa ameeleza kuwa hajawahi kusema kitu chochote ya Rais Obama na mkewe.

Beyonce  kupitia msemaji wake alikanusha madai hayo na kusema "Ni kichekesho". Hata hivyo inafahamika kuwa familia ya Obama ni rafiki na familia ya Beyonce Knowles ambapo Beyonce aliimba siku ya kuapishwa Barack Obama na vile vile aliimba katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Michelle Obama kutimiza miaka 50.
Ahsante sana kwa wimbo mzuri. Obama akimshukuru Beyonce siku ya kuapishwa kwake.
Siku ya kuapishwa Obama
Happily married; Beyonce na mumewe Jay-Z