Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja
wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.
Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili
hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama
ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali
yake, lakini pia atawabana wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao
hawalipi kodi
Magufuli amewataka Wananchi kumuamini
kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na
kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake
na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura.
Wananchi na Mabango yao
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka
kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo mchana.
Wakazi wa Nguruka waifuatilia Mkutano.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa
Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa
wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika
Nguruka mkoani Kigoma.
Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi
ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe
kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni
humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya akina mama wakishangilia jambo
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia
wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kwenye mkutano wa kampeni za Uraisi
jioni ya leo.
Baadhi
ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika
kijiji cha Kalinzi,ambapo mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia
aliwahutubia wananchi.
Wakazi wa mji wa Nguruka,mkoani Kigoma wakifuatilia mkutano wa hadhara
Wananchi na mabango yao
Kada
maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba
akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia
chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na
kuwaomba ridhaa wakazi wa kigoma ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano wa kampeni za Urais
Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni
Picha zote na Michuzi Jr