Mgeni rasmi katika mbio hizo ,Waziri mkuu
Mstaafu ,Fredirck Sumaye akiingia uwanjani huku akihitimisha mbio za
km 21 .
WANARIADHA wa
Tanzania Joseph Theofily wa klabu ya riadha ya Holili
ya mkoani Kilimanjaro na Failuna
Abdi wa klabu ya riadha ya Winning Spirit ya jijini Arusha wamefanikiwa kupeperusha
vyema Bendera ya taifa baada ya
kuibuka washindi wa kwanza katika mbio za kimataifa za Ngorongoro
Marathoni kwa upande wa wanaume na wanawake.
Mwanariadha Theofily alifanikiwa kumaliza mbio za
km 21 akitumia muda wa saa 1:03:09 na
kujinyakulia kitita cha sh Mil, 1. mbele ya wakongwe wengine kutoka nchi za Kenya ,Uganda na Malawi
huku Gabriely Gerald wa klabu ya
Winning Spirit ya jijini Arusha akishika nafasi ya
pili akimaliza mbio akitumia saa
1:03:36 na kujinyakulia kitita cha sh laki 5.
Emanuel Giniki
alifanikiwa kushika nafasi ya tatu na kujinyakulia zawadi ya sh 250,000,nafasi ya nne ikichukuliwa na
Ezekiel Therop huku mwanariadha
Mohamed Msenduki wa klabu ya Wining Spirit ya jijini Arusha akimaliza nafasi ya tano.
Mwanariadha wa kike Failuna aliyerejea hivi
karibuni kutoka nchini Brazil
kushiriki mashindano ya mbio za Km 15 ambazo
alifanikiwa kumaliza mbio hizo
katika nafasi ya saba,aliwaongoza wakongwe kama Banuelia Bryton ,Marry Naali Jackline sakilu na
Catherine Range akimaliza mbio
katika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa 1:10:25.
Failuna aliyejinyakulia zawadi ya kitita cha kiasi
cha sh Mil,1. alifuatiwa kwa
karibu na mpinzani wake Nathalia Elisante aliyetumia muda wa 1:14:40 na kuzawadiwa kitita cha sh
500,000 huku nafasi ya tatu
ikichukuliwa na Magdalena Crispine aliyetumia muda wa
1:15:56, nafasi ya nne na
tano ikienda kwa Anjelina Tsere na Merry Naali.
Mbio za kimataifa Ngorongoro Marathoni zinafanyika
zikiwa na lengo la kuwawezesha watoto
wa jamii ya kimasai kupata elimu ikiwemo kumalizia shule ya Endulen iliyoko Ngorongoro na kutangaza
urithi wa utalii kupitia hifadhi ya
taifa ya Ngorongoro huku ikishirikisha pia mbio za Kilomita tano kwa wafanyakazi wa taasisi
mbalimbali pamoja na Km 2.5 kwa wanafunzi.
Kwa picha zaidi ingia hapa,
www.dixonbusagaga.blogspot.com |