May 2014

Baadhi ya wageni waliohudhuria shindano la vipaji Miss Dar Indian Ocean!

Mfanyabiashara Teef Fundikira akiteta kitu na Mkurugenzi wa kampuni ya Aset Bibi Asha Baraka.
Mdau wa tasnia ya urembo Bi Hawa  Mkamba(kulia) akiwa na rafiki yake.
Kutoka kushoto Asha Baraka, Mkurugenzi wa Lino International inayoandaa shindano la Miss Tanzania na Khadija Kalili muandaaji wa Miss Pwani
Mfanyabiashara Bw Hassan akiwa na muandaaji wa Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahma Yusuf.


Shindano la Miss Dar Indian Ocean litafanyika jumamosi ya tarehe 7/06/2014 katika ukumbi wa Chichi Hotel, Kinondoni.
Wadau wa urembo wakifuatilia onesho hilo kwa umakini mkubwa! 
Wazee wa kazi: Hashim Lundenga na Bw Bosco Majaliwa
Mkuu wa itifaki na nidhamu Bw Ephraim Makoye
Toka kushoto Hassan, Hidani Ricco na Boy George(Muandaaji wa zamani wa Miss Kinondoni) 

Wajue top five wa vipaji Miss Dar Indian Ocean!

Shindano la urembo la Miss Dar Indian Ocean likiwa linakaribia, siku ya ijumaa  tarehe 23/5/2014 wapenzi wa tasnia ya urembo jijini Dar na wilaya zake walishuhudia mchuano mkali wa kugombea ushindi wa kipaji katika ukumbi wa Chichi hotel ambapo warembo watano kati ya 15, walifanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la kipaji zitakazofanyika siku ya kumtafuta Miss Dar Indian Ocean ambayo ni Jumamosi ya tarehe 7/6/2014 katika ukumbi huo huo maridhawa wa Chichi hotel. Onesho hilo lilihudhuriwa na kamati ya Miss Tanzania pamoja na Miss Tanzania 2012 Salha Israel, pamoja na wadhamini kama CXC na wengine wengi. Dalili zinaonesha show ya Miss Dar Indian Ocean itakuwa si mchezo kwani kwa onesho dogo tu la kipaji ukumbi na jukwaa vilipambwa vilivyo na kampuni maaurfu ya Vayle Springs. Mtandao huu ulipoongea na muandaaji wa shindano hilo Bibi Rahma Yusuf ambaye anaanda shindano hilo kupitia kampuni yake ya Rahmat Entertainments alisema kwa kujiamini "Hii ni trela tu muvi yenyewe ni tarehe 7June ukikosa show hiyo bora uhame mji" Onesho hilo la vipaji lilidhaminiwa na Chichi hotel.
Kutoka kushoto ni Suzzete Fetrick, Mary Amos, Sasha Deogratius, Camilla John na Getrude Massawe, hawa ndio walioingia fainali za Miss Dar Indian Ocean Talent show.
Judges: Kutoka kushoto ni jaji Hassan, Husna Sajent na Iddi Zonki
Kutoka kushoto ni muandaaji wa Miss Mwanza Bw Dotto, Yusuf Omari aka Boy George, Salha Israel na katibu wa Miss Tanzania Bw Bosco Majaliwa wakifuatilia kwa makini shindano la vipaji.