September 2013

Washiriki wa Miss TPSC Tabora watembelea Cg fm

Nice Mbelwa(Meneja vipindi)akiwatambulisha washiriki wa Miss TPSC 2013 kwa mhariri wa habari wa Cg fm 89.5 Bw Titus Filipo.
Washiriki wa shindano la Miss TPSC 2013 jana walitembelea kituo cha  redio cha CG fm 89.5 ambapo walioneshwa jinsi ambavyo kituo hicho kinavyofanya kazi, vile vile walitembelea chumba cha habari, cumba cha utayarishaji na studio ambako walihojiwa na Nice Mbelwa na Vivian Pyuza.
Mkurugenzi wa Cg fm 89.5 Bw George Charles ambaye pia ni injinia wa kituo hicho cha redio.
Mtangazaji Vivian Pyuza akiwa studioni tayari kwa mahojiano na washiriki wa Miss TPSC

warembo pose!

Mratibu wa shindano la Miss TPSC 2013

Mmetuona? Joyce Lilian na Perpetua.


Paulina akijibu moja ya maswali toka kwa Nice Mbelwa na Vian Pyuza wa Cg fm 89.5 jana

Mshiriki Lulu akiwekwa mtu kati kwa maswali na watangazaji wa Cg fm 89.5

Mshiriki Miss Saada akicheka baada ya kuulizwa swali la kizushi

MSANII: ALLY NIPISHE amepania kuwaona live mashabiki wake wa Tabora

MSANII: ALLY NIPISHE
Msanii wa kizazi kipya anayetamba na vibao kama Ntalila, Nipulika, Daima na milele, Binadam (aliyoimba na AT) na kibao kikali kinachotamba hivi sasa cha MY amepania kuwaona live mashabiki wake wa Tabora huku akimtafuta "MY" siku ya shoo kali ya kumsaka Mrembo wa Chuo Cha Utumishi wa UMMA Tawi la Tabora.

NI TAREHE 27-09-2013
UKUMBI:  TPSC (UHAZILI )FUNCTION HALL
MUDA: MBILI USIKU MPAKA CHWEE
ALLY BAUCHA | PRODUCER, ACTOR NA DANCER
HAPATATOSHA JUKWAA LITAKAPOVAMIWA TENA KWA SUPRISE AMBAYO KILA ATAKAYE KUWEPO ATAJIVUNIA KUMWONA MSANII WA TOFAUTI SANA BONGO ANAYEBEBA SIFA YA NGULI MOJAWAPO NA MFALME WA DUNIA. 
#SUPRISE HAISEMWI WAZI FIKA JIONEE#
BAUCHA ATAKIPIGA KIBAO CHAKE KIPYA KWA MARA YA KWANZA TABORA HUKU AKIKELESHA MASHABIKI KWA KIBAO CHAKE MAARUFU CHA "KELELE"
----------
WADHAMINI:
------
GONALA PHAMACY,SCREENMASTERS,SALUM MCHELE ELECTRONICS|
 FRADO BUSINESS CARE| ALOY SON BLOG| GAMALO PUB|
ROYAL PRODUCTIONS| MKWABI ENTERPRISES LIMITED| MSWAPE ALUMINIUM WORKS| MILLARDAYO.COM|
CG FM 89.5| TABORA REST HOUSE| NBS CLASSIC| CLOUDS FM|
NDIBS COLLECTION| HOLIDAY PARK.
---------

Shinji Kagawa acheza na moto Old Trafford

Moyes akiwa na Shinji Kagawa ziarani Japan kiangazi hiki.
Mshambuliaji mchezeshaji wa ki Japan anayechezea kilabu cha Man United Shinji Kagawa ameeleza kuchukizwa kwake na kutopangwa na David Moyes katika kikosi cha kwanza cha Man United tangu msimu huu umeanza aliongea na vyombo vya habari baada ya kuisaidia timu yake ya taifa Japan kuishinda Ghana kwa goli 3-1 ambapo yeye alifunga goli moja. Aliulizwa kwa nini hachezi mechi za Man united na waandishi wa habari naye alijibu" Jibu la swali hilo analijua David Moyes ni vema mmuulize yeye"
Kagawa: Anafikiri anapaswa kuwemo katika kikosi cha kwanza Man united ingawa alichelewa kuripoti mazoezini.
Kutokana na kuwa na mechi za timu yake ya taifa katika kombe la shirikisho alizocheza Kagawa alijikuta akicheza mechi moja tu ya maandalizi ya msimu mpya ambapo pia alipewa mapumziko ya wiki mbili zaidi ya wenzie na hivyo kumfanya kuwa asiye na utayari wa kuanza msimu.

Kwa maoni yangu David Moyes anatakiwa amkumbushe Kagawa kuwa Man united ni kilabu kilichopata mafanikio makubwa huku kikiwa na usiri mkubwa ndani ya kilabu hicho, na sijapata kumsikia mchezaji akilalamika katika vyombo vya habari juu yakutopangwa na Sir Alex Ferguson kwa kuwa hakuruhusu mchezaji yeyote kuongea na vyombo vya habari hasa kwa habari hasi kama hiyo. Sir Alex amepata kusema mara nyingi kuwa meneja ni lazima awe ndio mhimili wa kila kitu katika klabu na meneja asiruhusu mchezaji kujiona mkubwa kuliko kikosi kizima, ndio maana nasema Moyes amkumbushe Kagawa jukumu lake.


Wachezaji nguli wa soka wahoji kutochezeshwa Carrick jana

Michael Carrick Pass master!
Wachezaji nguli wa soka wa zamani wakiongozwa na Gary Linneker jana walihoji ni vipi mcheza wa daraja la juu kiungo wa Man United hakupangwa katika mechi ya Ukrayne dhidi ya England pamoja na England kuonesha wazi kushindwa kumiliki mpira kwa vipindi virefu katika mchezo huo, Linneker ambaye alipata kuzichezea Fc Barcelona ya Spain na Totenham Hotspurs ya jijini London aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kama hivi
Kana kwamba haikutosha Lineker kushangazwa naye Dietmar Hamman aliyekuwa kiungo wa Liverpool na Man City
  kupitia mtandao huo huo naye ali tweet
Hamann naye alishangazwa na kukosekana Carrick katika kikosi cha England jana, katika hali ya kushangaza zaidi hata Roy Hodgson alipoamua kumpumzisha Jack Wilshere na kuamua kumuingiza Ashley Young ambaye si kiungop wa kati wakati Carrick alikuwepo benchini na England ilimuhitaji kwa kushindwa kumiliki mpira. Hata hivyo England ilifanikiwa kutoka sare na hivyo kuendelea kuongoza kundi H kwa pointi 16.

Kula panya na zabibu kavu kwamnusuru kifo baada ya kukaa njaa miezi minne!

Raul Fernando Gomez (58) aliyepotea kwa miezi minne akiwa katika safari ya kutembea kwa miguu katika milima huko nchini Uruguay Amerika ya kusini akitokea nchini Chile aliokolewa jumapili na kundi la wa Argentina waliofika katika eneo hilo la milima wakifanya utafiti juu barafu (snow). Huku akiwa amepungua karibu kilo 3, na kupoteza virutubishi mwilini katika sakata hilo,madaktari wamesema atarudi katika hali yake ya kawaida baada muda mfupi?
Gomez akionesha jinsi alivyokonda
Gomez ambaye alisafiri kutoka Chile kwenda Argentina mnamo mwezi Mei kwa pikipiki kwa bahati mbaya pikipiki hiyo iliharibika njiani na hivyo kulazimika kutembea kwa miguu ambapo alipotea njia baada ya kimbunga kutokea. Maafisa toka jimbo la kaskazini magharibi mwa Argentina walimkuta akiwa katika kibanda kilichopo futi elfu 9318 kutoka usawa wa bahari, Gomez akiwa dhoofu wa hali alifanikiwa kutembea kwa taabu ambapo alifungua mlango wa kibanda hicho ndipo maafisa hao waliokuwa wakipita eneo hilo wakamuona. 

Akibebwa baada ya kuokolewa


Gavana wa San Juan aliliambia gazeti la Diario de cuyo "Huu ni muujiza, bado hatuamini kilichotokea, Tulimpatia simu akaongea na familia yake, pia nilimuuliza wewe ni mwenye kuamini? akajibu " sikuwa lakni sasa ni mwenye kuamini! Kwa muda wote huo Gomez alikuwa akila zabibu zilizokauka, sukari na panya. Madaktari wameeleza kuwa Gomez anatibiwa shinikizo la damu na ukosefu mkubwa wa virutubisho na maji mwilini.
Akipakiwa katika machela ili apelekwe hospitali

Matibabu; Akiwa amelazwa hospitali mjni San Juan.


Habari kwa hisani ya Dailymail, picha kwa hisani ya AP na Reuters.

Breaking news! Jaji wa Redds Miss Tabora afariki asubuhi hii!

Marehemu Terry Mbaika siku ya shindano la Redds Miss Tabora 2013
Aliyekuwa jaji katika shindano la Redds Miss Tabora 2013 Miss Terry Mbaika (pichani kushoto) amefariki leo hii asubuhi katika hospitali ya Jeshi ya Mirambo mjini Tabora. Taarifa zimeeleza kuwa Madame Terry ambaye ni Mkenya ki uraia alikuwa Mc maarufu mjini hapo na alikuwa akimiliki duka la virutubishi liitwalo TIENS, alilazwa katika hospitali hiyo na baadaye kuruhusiwa lakini hali yake ikawa mbaya na kurudishwa hospitalini hapo na hatimaye kufariki asubuhi ya leo. Nikiwa mwenyekiti wa kamati ya Redds Miss Tabora 2013 natoa salamu za rambi rambi kwa famila yake, kwani Marehemu Terry akishirikana na majaji wenzie waliwezesha kwa kiasi kikubwa kulifanya shindano hilo kupata washindi watatu ambao walikubalika na watu wote waliodhuria shindano hilo mapema mwaka huu katika ukumbi wa Frankman Palace mnamo tarehe 31/05/2013. Tumepoteza mdau muhimu na daima tutamkumbuka Terry MbaikaMungu ailaze roho yake pema peponi. Amen!
Kutoka kushoto Majaji Evans, Terry Mbaika, Mkala Fundikira, Irene Madumba na Wendy Charles.
Majaji kazini kwa umakini.
Hapa jaji Terry Mbaika akimfuatilia kwa umakini na ukaribu mshiriki wa Redds Miss Tabora 2013 katika shindano la kipaji.