April 2013

Msiba Uhazili! Tabora

Marehemu: Mariam Jumanne Tandala
Uongozi wa chuo cha UHAZILI tawi la Tabora unasikitika kutangaza kifo cha mwanachuo wake ajulikanaye kwa jina Mariam Jumanne Tandala (30) kilichotokea alfajiri ya ya leo katika hospitali ya Kitete, mipamngo kusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Manyara katika wilaya ya Babati kwa mazishi inafanyika.  Marehemu aliyeugua kwa muda mfupi jana alikuwa ameolewa. Haikuweza kufahamika kama alijaaliwa kuwa na mtoto.

            "Wa Inna llah wa inna illahi Rajiun"
           Mungu ailaze roho ya marehemu mahala 
                        pema peponi.Amen!

Majonzi: Bwana ametoa Bwana ametwaa!

Wanachuo wakifuatilia dua na maombi yalikuwa yakifanywa ukumbini humo

Afisa utamaduni Tabora azindua Redss Miss Tabora 2013 rasmi!

Afisa Utamaduni wilaya ya Tabora Bw Katunzi akisisitiza jambo
Shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Tabora 2013 jana lilizinduliwa rasmi na Afisa Utamaduni wa wilaya ya Tabora Bw Katunzi katika ukumbi wa Frankman Palace ambapo jumla warembo saba walichukua fomu za ushiriki wa shindano hilo kubwa mkoani Tabora  katika uzinduzi huo uliofana. Miss Tabora ambayo imekuwa ikiandaliwa na kampuni ya Club Royal Entertainments kwa miaka minne sasa ni shindano lenye msisimko mkubwa mkoani humo.

Models wa Redds Miss Tabora wakiwa wamevalia fulana maalum zinazotolewa na mdhamini mkuu Tbl kupitia kinywaji chao cha Redds Premium cold.

Nassor Wazambi (Mkuu wa itifaki) wa kamati ya Miss Tabora 2013 akisisitiza jambo jana katika uzinduzi wa shindano hilo


Warembo wa Miss Tabora wakionesha Redds Premium cold.

Toka kushoto: Saad Masawila, Mkala Fundikira, Pili Issa (Miss Tabora 2010) na Zena Motte(Miss Singida 2012/13)

Baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Tabora waki pozi kwa picha!

Jon Myuzik avamia Tabora!

Msanii Jon Myusik aki pose!
Kushoto; Mkala, Pili Issa, Jon Myuzik na Danny Kijumbe at Las Vegas pub Tabora
Msanii wa muziki wa kizazi kipya John Myuzik ambaye anatamba na track yake mpya "TONIGHT" yupo Tabora kwa masuala ya ki familia, jana alijumuika na kamati ya Miss Tabora 2013 kwa kubadilishana mawazo mawili matatu na kamati hiyo.

Kushoto;Pili Issa, Aloyson Mlawa, John Myuzik na Danny Kijumbe.

Playstation mpya inauzwa!

Playstation  mpya XBOX 360 60gb nyeupe ina controller 1, inauzwa, ipo katika box lake, atakayenunua atapata game moja buure! kwa bei na maelezo zaidi mpigie simu Alvin 0687232973.

Dayna amtunza shabiki buku kumi!

Dyna na patna wake wa stejini.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava Dyna, wikiendi iliyopita alitoa mpya pale alipoamua kumtunza kijana mmoja ambaye yeye Dyna alimwita stejini ili asaidiane naye kuimba wimbo alioimba na Marlow (Mafungu ya nyanya). Kwa mshangao wa wengi kijana huyo pichani aliimba kwa umahiri mkubwa kiasi cha kushangiliwa na watu walioingia ukumbini Royal Garden. Wimbo huo ulipoisha Dayna aliamua kutoa pesa yake mfukoni sh elfu kumi na kumtunza kijana huyo ambaye aliigiza wimbo huo vizuri na kukonga mpaka moyo wa Dayna mwenyewe.
Kazini.
Ile ile.

Hapa Dyna akitoa sh 10,000/=

Majembe; Dj Kali, msanii Man Fley na Mshabiki wa Bongo Flava wakifuatilia show.

Msanii Man Fley na Mshabiki wake

Mmoja wa wamiliki wa klabu ya Royal Adam Fundikira na mkewe Joyce katikati wakifuatili onesho hilo

Chura Fashion Tabora inatisha ki noma!


Kwa nje Chura Fashion
Chura Fashion ni duka la nguo za kike na kiume, viatu na mazaga zaga kibao mjini Tabora. duka hilo ambalo lina section mbili yaaniya kike na kiume halina mfano mjini Tabora. Hasa katika kipindihiki weekend inakaribia nawashauri wale wapenda outing wasipoteze muda kuzunguka sijui Mtaa wa Salmini au wapi, we fika tu CHURA FASHION ujipatie mahitaji yako kwa bei rahisi, maneno matupu hayavunji mfupa jionee mwenyewe mazaga zaga toka Majuu hapo chini.

Mkurugenzi wa Chura Fashion akiwa na mteja
Pamba za kiume
Pamba za madada
Majembe ya Tabora.
Flat shoes kali za madada
Miguu mikali kwa majembe!
The man himself  director ma man Mashaka Chura

Kitale, Dyna na Kala Jeremaya wapagawisha Tabora

Kala Jeremaya mwingine!

Kala Jeremaya akiwarusha wapenzi wake katika ukumbi wa Royal Garden






Msanii wa vichekesho na muziki Kitale akifanya vitu vyake jukwaani Royal Garden Tabora.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava Kitale, Dyna na Kala Jeremaya jumamosi ya tarehe 6/4/2013 walitoa burudani safi katika manispaa ya Tabora ndani ya ukumbi wa Royal Garden. Onesho hilo ambalo lilifana sana pamoja na kuhudhuriwa na watu wachache kutokana na hali ya hewa kutishia mvua kunyesha amabapo mnammo majira ya saa 2 usiku manyunyu yalidondoka katika maeneo mengi mjini Tabora.
Baadhi ya washabiki wa Kitale wakifurahia show
Dyna akiwa na mshabiki mmoja aliyemwita jukwaani kuimba naye

Mziki kunoga!