Mayweather amshinda Pacquiao kwa pointi na kuweka rekodi ya ushindi mara 48!
Floyd Mayweather akitua moja ya sumbwi kati ya mengi yaliyompa ushindi dhidi ya m Philipino Manny Pacquiao . Lile pambano la kuvunja rekodi ki pesa zilizohusishwa kwa mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hatimaye limefanyika katika ukumbi wa MGM Grand garden arena jijini Las Vegas ambapo Money Mayweather aliibuka mshindi kwa pointi 118-110, 116-112 na 116-112 pamoja na kuwa Pacquiao kama ilivyotarajiwa na wengi alirusha ngumi nyingi lakini zisizo na mashiko yeyote katika maana ya kumuingizia pointi kwa upande mwingine Mayweather alicheza kiujanja na kuepuka ngumi za Manny lakini huku akijiingizia pointi kwa masumbwi yake ya moja kwa moja na kuwapendeza waamuzi. |
Jamie Foxx akiimba wimbo wa taifa la Marekani, hata hivyo imeelezwa watumiaji wengi wa mtandao wa Twitter wakimshutumu aliuimba vibaya wimbo huo wa taifa |
Mayweather akipanda ulingoni huku akionesha sura yenye wasiwasi pamoja na kuwa alishinda pambano hilo. |
nGail Banawis, akiwa na Word Chorale waliimba wimbo wa taifa la Phillipines, |
Pacquiao akiingia ukumbini tayari kwa pambano |
Pacquiao akirusha sumbwi la mwilini dhidi Mayweather |
Pacquiao akipewa huduma wakati wa mapumziko. |
Money akipewa maelekezo na mkufunzi wake |
Money Mayweather akishangilia ushindi wake leo hii lakini mashabiki wengi nchini mwake walimbeza. |
Floyd "Money"Mayweather akiwa na mikanda yake na mmoja alioushinda leo hii. |
Ndege binafsi za watu maarufu na wenye fedha zao zikiwa zimeujaza uwanja wa Las Vegas kabla ya pambano Picha na habari kwa hisani kubwa ya mailonline |
Mratibu wa asasi ya Better Living Aid atoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi!
Watangazaji Hamisa Mussa Lubilo na Deogratius Yagomba wa VOT fm 89.0 wakimuuliza maswali mratibu wa asasi ya Better Living Aid walipomualika leo asubuhi katika kipindi cha Meza huru! |
Mkala Fundikira akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na watangazaji wa kipindi cha Meza huru, kipindi kinachoruka ktk kituo cha redio cha VOT fm 89.0 ya Tabora leo asubuhi. |
Mkala akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wenye kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino ya mkakati wa Imetosha. |
Fundikira pia alimshukuru Mh Munde Tambwe Abdallah kwa kutoa ahadi ya Mifuko 50 ya simenti, lori 10 za mchanga pamoja na tano za mawe na kokoto , alisema "Tena kabla sijasahau nimpongeze na kumshukuru sasa sana sana Mh Munde Tambwe kwa kutupa msaada ambao ni msingi, kwa maana ya kuwa ahadi yake ndiyo itaanzisha ujenzi wa majengo hayo ya vyoo na zahanati, hivyo basi na wengine wajitolee ili tusonge mbele"
Hoteli ambamo chakula cha usiku cha uchangishaji fedha kwa ujenzi wa vyoo na zahanati utafanyika baadae mwezi huu jijini Dar es Salaam iliyopo maeneo ya Ocean road. |
Aidha asasi hiyo ina mpango wa kuandaa chakula cha usiku jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Southern Sun baadae mwezi huu ambapo Mh Samuel Sitta(waziri wa uchukuzi) amekubali kuwa mgeni rasmi, karamu hiyo itaandaliwa ili kuchangisha fedha za kuwezesha miradi hiyo iweze kukamilika. "Bado tupo kwenye hatua za mwanzo za maandalizi lakini tunataraji karamu hiyo ya uchangishaji pesa ifanyike ama mwishoni mwa mwezi wa MEI au mwanzoni mwa mwezi Juni 2015. Pia Fundikira aliwashukuru Mh Aden Ragen(Mbunge wa Tabora mjini), Mh Munde Tambwe(Viti maalum), Sylvester Koka(Mbunge wa Kibaha) na wanachama na wote wa Better Living Aid kwa kuwezesha kifedha upulizwaji wa dawa kijiji cha Amani uliogharimu Tsh Laki 980.
Tembelea mtandao wa betterlivingaid.Blogspot.Com ujue zaidi kuhusu asasi hii na malengo yake au piga namba 0754 666620 kwa maelezo.
MBUNGE NDESAMBURO NA MEYA WA MOSHI JAFARY MICHAEL WAENDELEA NA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA MOSHI MJINI.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika jirani na Super Market ya Nakumat. |
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo wakimsikiliza Ndesamburo. |
Ndesamburo akizungumza. |
Baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakimsilikiza Ndesamburo. |
Msatahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara . |
Mbunge waMoshi mjini Philemoni Ndesamburo
akimsikiliza Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi.(hayuko pichani) akiwa
na viongozi wengine wa Chadema. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi. |
MASHINDANO YA LUCY OWENYA CUP YAZINDULIWA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI.
Mbunge wa viti Maalumumkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akiwasili katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini na kushirikisha kata 16 za jimbo hilo. |
Baadhi ya wananchi waliohudhulia ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015. |
Mbunge Owenya akicheza ngoma katika shrehe za ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup. |
Baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo zikiwakatika uwanja wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya uunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015. |
Mratibu wa mashindano hayo,Charles Mchau akizungumza jambo katika ufunguzi wa mashindano hayo. |
Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya akisalimianana mwamuzi Batista Mihafu wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo. |
Mbunge wa Viti maalumu ,Lucy Owenya akikagua baadhi ya timu zinazpshiriki mashindano hayo . |
Mbunge Lucy Owenya akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup. |
Hatimaye wakazi wa kijiji cha Amani Tabora usiku wa leo watalala bila kero ya kunguni!
Kijji cha Amani kinavyoonekana |
Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya.
Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.
Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa |
Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa |
Hpa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro |
Job DONE |
Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini |
Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa |
Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho |
Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo. |
Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa kunguni na wadudu wengine. |
Rundo la mahindi likiwa limotolewa nje kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni nani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa. |
Baadhi ya panya waliokutwa ndani ya chumba cha mkazi mmoja wa kjijini hapo leo. |
Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni |
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid Mkala Fundikira kushoto akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma. |
Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa. |
Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji |
Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita kiasi. |
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)