MANDHARI MWANANA YAWAVUTIA WATALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO
Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa katika gari kuelekea kilele cha Shira katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro. |
Kundi la Pili la watalii wa ndani wakiwa katika eneo la uwanda wa Shira mara baada ya kufika kwa usafiri wa gari hadi katika eneo hilo. |
Safari ya kuelekea katika vivutio vya asili katika uwanda wa Shira ,hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU),Faustine Bee akitizama mandhari katika uwanda wa Shira wakati akipanda mlima huo kuelekea katika mapango ya Shira. |
Raia wa kigeni wakipata kumbukumbu katika maeneo mbalimbali ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Watalii wa ndani wakichukua taswira mbalimbali mara baada ya kufika kilele cha Shira ndani ya Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Faustine Bee akichukuliwa taswira na kijaa wake baada ya kufika eneo la Shira hut. |
Safari ya kuelekea kutizama mapango ikiendelea. |
Watalii wa ndani wengine waliweka kumbukumbu. |
Safari ikaendelea. |
Baada ya kupanda vilima watalii wa ndani pia walipata nafasi ya kupumzika. |
Watalii wa ndani wakiwa katika mapango ya Shira ambayo yalitumiwa na wapagazi wakati wa zoezi la kupandisha watalii wakati wa safafri ya kuelekea kilele cha Uhuru, |
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Prof,Faustine Bee akifurahia mara baada ya kuingia katika mapango ya Shira. |
Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika Prof,Faustine Bee akizungumza jambo kuhusu miamba iliyoko katika mapango hayo. |
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mwanga wakiongozwa na meneja wao ,Innocent Silayo(wa pili toka kulia) wakishuka mara baada ya kutembelea vivutio katika uwanda wa Shira. |
KAMPUNI YA BONITE BOTTLERS YAMWAGA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MOSHI VIJIJINI.
Meneja Masoko na mauzo na wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd Christopher Loiruk akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika vijiji hivyo. |
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akipokea msaada wa unga kutoka kwa Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers,Joyce Sengoda kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko. |
Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga akizungumza mara baada ya kupokea msaada kutoka kampuni ya Bonite Botttlers kwa ajili ya waathirika wa mafuriko. |
Eneomoja wapo ambalo wakazi wake wameathirika kwa mafuriko katika kijiji cha Kilungu. |
Msaada wa maji ambayo yametolewa kwa waathirika wa mafuriko katika vijiji hivyo ili kupunguza kutokea kwa maradhi ya tumbo yanayoweza kutokea kwa matumizi ya maji machafu. |
Unga wa ngano ukishushwa kwa ajili ya waathirika hao. |
Baadhi ya nyumba zilizo athirika na mafuriko hayo. |
Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo ambao
baadhi yao bado wako katika kambi iliyopo kijiji cha Kilungu wakiishi
katika zahanati ya kijiji hicho. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
UNESCO YAAHIDI KUWASAIDIA WATANZANIA KUKABILI DHULUMA DHIDI YA WANAOISHI NA ALBINISM
Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia).
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Mwanza
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeahidi kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati akizungumza na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.
Mwakilishi huyo wa Unesco amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa mkoa kumsalimia na kumweleza hatua zinazochukuliwana Unesco katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism.
Akifafanua zaidi alisema kwamba UNESCO haijatenga fedha zitakazotumika kuendesha kampeni mahsusi bali itatumia uwezo wa kiufundi uliopo kwa wataalamu walionao na kwamba wanakusudia kuona kwamba miaka 15 ijayo watoto wanaozaliwa nchini Tanzania wanakuwa huru pasipo na viashiria vya kuhatarisha maisha vinavyosababishwa na mauaji ya watu wenye albinism.
Akimkaribisha Bi Zulmira ofisini kwake, Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo alisema kwamba ingawa kuna utulivu katika kipindi hiki mkoani Mwanza, bado mkoa wake unaendelea kukabiliana na viashiria vinavyosababisha ukatili kwa watu wenye albinism na wazee.
Bwana Magesa alisema imani potofu zilizopo zinazosadikika kufanikisha biashara za uvuvi wa samaki, uchimbaji wa madini na wanasiasa kuendelea na madaraka ni miongoni mwa sababu kubwa za mauaji hayo yaliyoitia doa jeusi jamii ya kitanzania nje ya mipaka.
Alisema kwamba jitihada zinafanywa kukabiliana na imani hizo potofu kwa kuihamasisha jamii kutoziamini na kwamba madaraka na utajiri unatokana na juhudi, kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.
Aidha amesema mkoa wake umekuwa ukihakikisha kwamba makundi yanayotumika kuua watu wengine kwa kushirikisha jamii yanavunjwa na pia kuwachukulia hatua kali wote wanaobainika kushiriki kwa njia moja au nyingine.
Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa alisema kwamba hali ya amani itatawala pale tu watu watakapobaini kwamba kuua ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ni kosa la jinai.
Alisema pindi binadamu watakapokiri kwamba binadamu wote ni sawa na kuishi na albinism sio ‘mzimu’ watabadili mwelekeo mzima wa fikra potofu kimaisha na kuishi kwa amani na kuthaminiana.
Bi Zulmira alimwambia mkuu wa mkoa kwamba UNESCO kwa kushirikiana na wadau wengine wataendesha makongamano yenye lengo la kushirikisha jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayo changia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhuluma zinazofanya dhidi ya watu wenye albinism.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) akizungumza na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyeambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Mwaza, Faisal Issa.
Warsha hizo zitafanyika kwa wakati tofauti katika kipindi cha wiki mbili wilayani Sengerema, Misungwi, Msalala na Bariadi. Warsha hizo zilizoanzia Sengerema Jumatano na kumalizika Ijumaa zitafuatiwa na Misungwi Mei 25 hadi 27, Msalala Mei 28 hadi 30 na Bariadi kuanzia Mei 28-30.
Katika warsha hiyo pamoja na kujadili mada mbalimbali, mijadala itahusisha viongozi wa serikali, wanasiasa, viongozi wa kidini na kimila na hoja kubwa itakayojadiliwa ni dhana ya kisayansi ya albinism, mitazamo ya jamii kuhusu dhana hiyo, makundi mbalimbali ndani ya jamii, tofauti kati ya utamaduni na asili.
Pia watajadili kubainisha na kuanisha matatizo, changamoto na hatari zinazowakabili watu wenye alibinism na kuchambua mambo yanayochangia uwepo wa changamoto na hatari kwa watu wenye alibinism.
Katika majadiliano hayo pia mikakati inayoweza kupunguza au kumaliza kabisa matatizo changamoto na hatari zinazowakabili watu wenye alibinism katika jamii yetu itatazamwa.
Watoa mada wanatarajiwa kutoka katika halmashauri, vyama vinavyotetea maslahi ya albinism, mbunge anayetetea maslahi ya watu wenye albinism Al-Shaymaa Kwegyir na mwakilishi kutoka baraza la taifa la dawa asilia.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiendelea na maongezi na ugeni huo ofisini kwake jijini Mwanza.
Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia), akielezea nia ya Shirika lake kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism nchini alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ofisini kwake jijini Mwanza.
Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia).
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)