Tafrija ya Tanzania bloggers yafana Serena hotel!
Mwenyekiti wa Mtandao wa mabloga Tanzania Bw Joachim Mushi (The habari blog) akisisitiza jambo wakati akiwakaribisha wageni waalikwa na mgeni rasmi. |
Mgeni rasmi katibu mtendaji wa MCT Bw Kajubi Mukajanga na Blogger Othman Maulid(Zanzibar leo) |
Kutoka kushoto Mkala Fundikira(keronyingi blog), Jennifer Zighilla(Chingaone blog) na Joshua Fanuel |
Mgalula Fundikira, Peter Moe na Mkala Fundikira |
Mrs Issa Michuzi, Shamim na mdau |
Kutoka kushoto Rahel Pallangyo, Chingaone, Malunde na Monica Joseph Monfinance |
Malunde1, Mgalula Fundikira, Faraji Swai na Mdau |
Mgalula Fundikira, Henry Mdimu (Balozi IMETOSHA MOVEMENT) Mkala Fundikira na Rahel Pallangyo |
Malunde1 akisalimiana na Mgeni rasmi Bw Mukajanga. |
Mdau, Malunde na Jo Mwaisango(Mbeya yetu) |
Msanii Jhikoman alikuwepo pia |
Wakala wa Mdhamini Vodacom, NMB na Raha |
William Malecela( Blog ya wananchi) |
Afisa uhusiano wa Vodacom Bw Kevin Twissa akihutubia hafla hiyo |
Toka kushoto ni Mgeni rasmi Bw Kajubi D Mukajanga, Joachim Mushi, Issa Michuzi, Othman Maulid, Josh Fanuel na Henry Mdimu. |
Chingaone,Josh Fanuel na Father Kidevu |
Mwakilishi kutoka USA embnassy ya Tanzania |
Msanii Jhikoman akitumbuiza na wimbo wa Ushirkina na John Kitime (Cheka na Kitime blog) |
Jhikoman akipiga gitaa |
Mkala Fundikira, Woinde Shizza na Faraji Swai |
Mgeni rasmi akikata Ndafu |
Mkala na Rose Ndauka(Bongo movie star) |
Freddy, Khadija Kalili(Bongo weekend) na Mkala |
Rose Ndauka, Mkala na mwenyekiti Mushi |
Mabloga wafanya dhihaka miongoni mwao |
Mdau na Rose Ndauka |
Adela kavishe (dallykavisheblog) |
Mdau na Chingaone |
Zainul Mzige(Mo Blog) na Woinde Shizza. |
Shabiki wa Chelsea mpigania haki za binadamu atuhumiwa kwa ubaguzi Paris!
Bw Richard Barklie akihutubia kongamano la haki za binadamu nchini India |
Bw Barklie ambaye pia ni mkurugenzi katika taasisi ya hiari mjini Belfast Northen Ireland ya WAVE TRAUMA CENTRE ameshasimamishwa kazi na taasisi hiyo kupisha upelelezi.
Barklie ambaye ni mmiliki wa tiketi ya msimu ya Chelsea fc akiwa na wenziwe watatu walimsukuma Bw Syla asiingie ndani ya treni (METRO) huku wakiimba (we are racists we are racists this is how we ike it) Sisis ni wabaguzi na hivi ndivyo tupendavyo. Police nchini England imeshawatambua watuhumiwa lakini hakuna aliyekamatwa mpaka sasa, Idara hiyo ya polisi imeeleza upelelezi utaingia hatua inayofuata.
Hata hivyo kupitia mwanasheria wake Bw Barklie amakanusha kuhusika na vitendo vya kibaguzi vilivyotokea siku hiyo lakini anakiri kuwepo eneo la tukio, na amedhamiria kujisafisha.
Metropolitan police pia imeeleza haiwezi kukamata mtu kwa makosa aliyoyafanya nje ya Uingereza, kwa mawazo yangu basi bila shaka Polisi ya Paris itabidi iiombe serikali ya England washukiwa wapelekwe Ufaransa kwa mahojiano na pengine kushtakiwa iwapo itaonekana wana kesi ya kujibu.
Kilabu cha Chelsea kupitia meneja wa timu Jose Mourinho kimeelzwa kusikitishwa na tukio hilo na kuwa kitawafungia wote watakapatikana na kesi ya kujibu. Taarifa ya msemaji wa kilabu hicho cha jijini London ameelza kuwa mmiliki wa timu hiyo Bw Roman Abramovich ametiwa kinyaa na kitendo hicho. Pia kilabu hicho kimeshamkaribisha Bw Syla London katika mchezo wa marudiano kati ya timu hizo mbili.
Picha ya Bw Barklie iliyochukuliwa toka cctv. |
Hotuba India |
Barklie akiwa katika harakati za haki za binadamu barani Afrika. |
Bw Suleyman Syla ndiye mhanga wa tukio la kibaguzi lililotokea stesheni ya treni za chini ya ardhi (METRO) jijini Paris Ufaransa. |
Msanii Moses Bushagama aka Mez B afariki dunia leo!
Mez B enzi za uhai wake! |
Msanii Moses Bushagama aka Mez B aliyewahi kung’ara na ngoma ya kikuku cha mama Roda ambayo mimi Mkala Fundikira nilimfanyia video yake katika miaka ya 2000 katika studio za Royal Productions, pamoja na nyimbo zingine nyingi amefariki dunia leo mjini Dodoma ambako mama yake huishi baada ya kuugua kifua kikuu(TB). Binafsi nimeshtushwa na kifo chake hasa baada ya kupata habari za kifo chake bila kufahamu kama alikuwa akiugua kwa muda.Mez alikuwa na kipaji cha aina yake na sauti laini, tutamkumbuika daima.
Mungu ilaze pema roho yake!
Picha kwa hisani ya Dj Choka
Homa ya mchezo kati ya Coastal union na Simba sports club yapamba moto!
Wakazi wa jiji la Tanga, viunga vya vyake na mikoa ya jirani leo hii watapata burudani inayotarajiwa kuwa ya kupendeza leo hii jioni mnamo saa 10.15 za jioni wakati Wekundu wa Msimbazi Simba SC itakapoingia katika stadia ya Mkwakwani kucheza mchezo wa Vodacom Premier league 2014/15 dhidi ya Coastal union ya jijini hapa kuwania pointi 3 muhimu hasa kwa Simba ambayo imekua ikifanya vibaya msimu huu na kupelekea hofu kwa washabiki wake kuwa uenda ikateremka daraja. Mpambano huo bila shaka utaoneshwa LIVE na kituo cha Televisheni cha AZAM ambacho mitambo yake imeonekana mje ya uwanja wa Mkwakwani, kama ionekanavyo hapo chini.
OB Van ya Azam Tv ikiwa tayai kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Mkwakwani stadium. |
Sare za Simba SC zikiwa zimeanikwa kwa mauzo nje ya uwanja wa Mkwakwani |
Mshabiki wa Simba kushoto akijadili bei ya fulana ya timu hiyo ya jijini Dar es Salaam karibu na uwanja wa Mkwakwani. |
Mfereji mpya wa maji wahatarisha watumia barabara ya Boma Tabora!
Kushoto unaonekana mfereji wa maji. |
Barabara ya Boma inavyoonekana pichani |
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)