mkalamatukio

Tuzo za Filamu 2015 zafana, Serikali Yahaidi Neema

Mwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015 jana. Mwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015jana.Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa kwenye filamu aliyotwaa mwanaye (marehemu Kanumba) kwenye tuzo za Filamu 2015. Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa kwenye filamu aliyotwaa mwanaye (marehemu Kanumba) kwenye tuzo za Filamu 2015Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015.
Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Mama yake marehemu Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.Mama yake na Steven Kanumba akilia baada ya kuitwa ampokelee tuzo mwanaye. Mama yake na Steven Kanumba akilia baada ya kuitwa ampokelee tuzo mwanaye.
Irene Paul (Best Actress) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. 
Irene Paul (Best Actress) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.

John Kalage (Best Director) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.

Irene Paul (Best Actress) akipongezwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Irene Paul (Best Actress) akipongezwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipeana mkono na viongozi wa meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipeana mkono na viongozi wa meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Grace Mapunda Best Actress Supporting Role) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Grace Mapunda Best Actress Supporting Role) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipokea tuzo kwa niaba ya msanii mwenzake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 janaMwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015 jana. Mwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015 jana.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

 SERIKALI imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na kujenga mazingira mazuri ili kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika, ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza katika tasnia ya filamu. Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa Tuzo za Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za filamu. Dk. Mukangala alipongeza juhudi za baadhi ya wafanyabiashara wa filamu na wasambazaji ya kudhibiti uharamia wa kazi za filamu, lakini aliwataka kuifanya kazi hiyo kwa manufaa ya wadau wote na sio kwa manufaa binafsi. "...Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanya biashara ya filamu yanaimarishwa. Pamoja na hayo ni vyema wasambazaji na wafanya biashara wengine wa filamu wenye uwezo wakaepuka kulidhibiti soko la filamu kwa nanufaa yao binafsi ili kujenga ushindani sawa," alisema Dk. Mukangala. Aliwataka wasanii na wadau wote wa filamu kuhakikisha wanaboresha kazi zao zaidi na kufuata vigezo vinavyotambulika ili kuzitangaza kazi zao hata nje ya nchi. "Napenda mtambue kuwa ubora wa bidhaa za filamu ni moja ya vigezo vya kuwa na soko bora la filamu, kwani filamu bora hujitangaza zenyewe. Tuhakikishe kuwa tunaongeza weledi na ubunifu. Hivi ndivyo vigezo vilivyoifanya sekta ya filamu nchi zilizoendelea kufika hapo ilipo," aslisema Waziri Dk. Mukangala. Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA), Simon Mwakifwamba aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga chuo maalumu kwa ajili ya filamu ili kuijengea uwezo zaidi tasnia kwani inamchango mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa makundi anuai. Waliojishindia tuzo za filamu kwa mwaka huu 'Tanzania Film Awards 2015 (TAFA)' katika vipengele mbalimbali ni pamoja na Irine Sanga (Best Screen Play), Hissan Muya (Best Actor Supporting Role), Grace Mapunda Best Actress Supporting Role), Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian), Irene Paul (Best Actress), John Kalage (Best Director) na wengineo.a Tuzo za filamu nchini ‘Tanzania Film Awards’ 2015 (TAFA). Tuzo hizi kubwa ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Conference Center. Zimewezeshwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani Production.

MANDHARI MWANANA YAWAVUTIA WATALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO


Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa katika gari kuelekea kilele cha Shira katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Kundi la Pili la watalii wa ndani wakiwa katika eneo la uwanda wa Shira mara baada ya kufika kwa usafiri wa gari hadi katika eneo hilo.
Afisa Masoko wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro akizungumza na watalii wa ndani kabla ya kuendelea na safari ya kutembelea vivutio mbalimbali viyoko katika uwanda wa Shira yakiwemo mapango ya Shira Caves.
Safari ya kuelekea katika vivutio vya asili katika uwanda wa Shira ,hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU),Faustine Bee akitizama mandhari katika uwanda wa Shira wakati akipanda mlima huo kuelekea katika mapango ya Shira.
Raia wa kigeni wakipata kumbukumbu katika maeneo mbalimbali ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Watalii wa ndani wakichukua taswira mbalimbali mara baada ya kufika kilele cha Shira ndani ya Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Faustine Bee akichukuliwa taswira na kijaa wake baada ya kufika eneo la Shira hut.
Safari ya kuelekea kutizama mapango ikiendelea.
Watalii wa ndani wengine waliweka kumbukumbu.
Safari ikaendelea.
Baada ya kupanda vilima watalii wa ndani pia walipata nafasi ya kupumzika.
Watalii wa ndani wakiwa katika mapango ya Shira ambayo yalitumiwa na wapagazi wakati wa zoezi la kupandisha watalii wakati wa safafri ya kuelekea kilele cha Uhuru,
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Prof,Faustine Bee akifurahia mara baada ya kuingia katika mapango ya Shira.
Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika Prof,Faustine Bee akizungumza jambo kuhusu miamba iliyoko katika mapango hayo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mwanga wakiongozwa na meneja wao ,Innocent Silayo(wa pili toka kulia) wakishuka mara baada ya kutembelea vivutio  katika uwanda wa Shira.
Mmoja wa watalii wa ndani ,Dkt Gaspaer Mpehongwa ,(Kulia) akizungumza jambo na wageni wakati akiwaonesha moja ya picha inayoonesha namna ambavyo volcano ilivyo ripuka na kutengenza uwanda wa Shira.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

KAMPUNI YA BONITE BOTTLERS YAMWAGA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MOSHI VIJIJINI.


Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Joyce Sengoda akiwasalimia wananchi katika vijiji vya Mikocheni ,Kilungu na Chemchem vilivyofikwa na mafuriko hivi karibuni wakati uongozi wa kampuni hiyo ulipofika kwa ajili ya kutoa msaada.
Meneja Masoko na mauzo na wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd Christopher Loiruk akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika vijiji hivyo.
Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa sukari kilo 750 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.
Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa maji zikiwa ni  katoni 500 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.
Meneja muajiri wa Bonite Bottlers ,Joyce Sengoda akikabidhi ndoo za mafuta kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga ambazo zimetolewa 30 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemchem.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akipokea msaada wa sabuni kutoka kwa meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers,Christopher Loiruk kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akipokea msaada wa unga kutoka kwa Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers,Joyce Sengoda kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko.
Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga akizungumza mara baada ya kupokea msaada kutoka kampuni ya Bonite Botttlers kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.
Eneomoja wapo ambalo wakazi wake wameathirika kwa mafuriko katika kijiji cha Kilungu.
Msaada wa maji ambayo yametolewa kwa waathirika wa mafuriko katika vijiji hivyo ili kupunguza kutokea kwa maradhi ya tumbo yanayoweza kutokea kwa matumizi ya maji machafu.
Unga wa ngano ukishushwa kwa ajili ya waathirika hao.



Baadhi ya nyumba zilizo athirika na mafuriko hayo.

Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo ambao baadhi yao bado wako katika kambi iliyopo kijiji cha Kilungu wakiishi katika zahanati ya kijiji hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.