mkalamatukio

Ilikuwa balaaaa!

Keyboy na Dj maarufu Ommy Composer
 Siku ya Alhamisi tarehe ya tarehe 2/04/2013 bendi maarufu ya Mapacha Watatu ilitumbuiza mjini Tabora katika ukumbi wa Frankman Palace ambapo mambo mengi yalijiri ikiwemo vituko hebu jionee mwenyewe!
Kanyaga twende!
Meneja wa bendi Hamis Dakota akijimwaga na mmoja wa washabiki waliohudhuria onesho hilo
Mwango aka Benny Ngwasuma akiserebuka na Mariam Zidane
Hamis Dakota, tena akijiachia na mdada mwenye makeke mengi!
Sichezi na shemeji: Jose Mara aligoma kucheza na mwanadada ambaye ilidaiwa ni shemeji yake.
Wadau wakimcheka Jose Mara wa Kimara kwa kugoma kukamatia.

Baunsa Muddy naye alionja raha ya kukamatia,  Duh sijui Muddy alilpata usingizi?
Duh cheki! Juma Kapipi aduwaa!

Mbona hujaniimba Khalid?
Uuuuuuuh! Ngoma inogile! Mikono juu!
Papaa Biggie na Mariam Zidane waki pozi kwa snap!
Uzinduzi wa albam Yarabi nafsi!

Mapacha watatu wazindua albam Tabora!


UZINDUZI; Chokoraa kushoto na Jose Mara wakizindua album mpya katika ukumbi wa Frankman, Tabora.
Bendi ya Mapacha watatu usiku wa alhamisi katika ukumbi wa Frankman Place mijini Tabora, walizindua album yao mpya iendayo kwa jina la Yarabi nafsi yenye nyimbo nane ambamo kuna watunzi kadhaa akiwemo Jose Mara, Khalid Chokoraa na nyota wengine wakali wanounda bendi hiyo pia wametunga nyimbo kadhaa. Katika hali ya kujutia pengine Bendi hiyo iliwasili Tabora ikiwa na cd chache za albam hiyo mpya ambazo ziliisha bila wao kutegemea

Mdau wa mapacha watatu!

Siku Mapacha watatu walipovamia Tabora!

Bendi machachari ya Mapacha watatu toka jijini Da re Salaam ilifanya onesho kabambe mjini Tabora katika ukumbi wa Frankman Palace usiku wa   alhamisi. Bendi hiyo ikiwa china ya mkurugenzi wake Jose Mara(Mzee wa Kimara) na rapa machachari Khalid Chokoraa ilikuwa njiani kueleka Kahama na ambako walifanya onesho siku ya Ijumaa na leo Jumamosi watakuwa jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Bendi ya Mapaha watatu akifanya vitu vyake jukwaani

Wanenguaji wakimwaga vimbwanga!

Shughulikaaaa!

Mariam Zidane akinengua!

Mikono mbele, twende!


Washabiki wa Mapacha watatu wakiongozwa na Benny Ngwasuma wakila bata ndefuuuu!

Msiba Uhazili! Tabora

Marehemu: Mariam Jumanne Tandala
Uongozi wa chuo cha UHAZILI tawi la Tabora unasikitika kutangaza kifo cha mwanachuo wake ajulikanaye kwa jina Mariam Jumanne Tandala (30) kilichotokea alfajiri ya ya leo katika hospitali ya Kitete, mipamngo kusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Manyara katika wilaya ya Babati kwa mazishi inafanyika.  Marehemu aliyeugua kwa muda mfupi jana alikuwa ameolewa. Haikuweza kufahamika kama alijaaliwa kuwa na mtoto.

            "Wa Inna llah wa inna illahi Rajiun"
           Mungu ailaze roho ya marehemu mahala 
                        pema peponi.Amen!

Majonzi: Bwana ametoa Bwana ametwaa!

Wanachuo wakifuatilia dua na maombi yalikuwa yakifanywa ukumbini humo

Afisa utamaduni Tabora azindua Redss Miss Tabora 2013 rasmi!

Afisa Utamaduni wilaya ya Tabora Bw Katunzi akisisitiza jambo
Shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Tabora 2013 jana lilizinduliwa rasmi na Afisa Utamaduni wa wilaya ya Tabora Bw Katunzi katika ukumbi wa Frankman Palace ambapo jumla warembo saba walichukua fomu za ushiriki wa shindano hilo kubwa mkoani Tabora  katika uzinduzi huo uliofana. Miss Tabora ambayo imekuwa ikiandaliwa na kampuni ya Club Royal Entertainments kwa miaka minne sasa ni shindano lenye msisimko mkubwa mkoani humo.

Models wa Redds Miss Tabora wakiwa wamevalia fulana maalum zinazotolewa na mdhamini mkuu Tbl kupitia kinywaji chao cha Redds Premium cold.

Nassor Wazambi (Mkuu wa itifaki) wa kamati ya Miss Tabora 2013 akisisitiza jambo jana katika uzinduzi wa shindano hilo


Warembo wa Miss Tabora wakionesha Redds Premium cold.

Toka kushoto: Saad Masawila, Mkala Fundikira, Pili Issa (Miss Tabora 2010) na Zena Motte(Miss Singida 2012/13)

Baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Tabora waki pozi kwa picha!

Jon Myuzik avamia Tabora!

Msanii Jon Myusik aki pose!
Kushoto; Mkala, Pili Issa, Jon Myuzik na Danny Kijumbe at Las Vegas pub Tabora
Msanii wa muziki wa kizazi kipya John Myuzik ambaye anatamba na track yake mpya "TONIGHT" yupo Tabora kwa masuala ya ki familia, jana alijumuika na kamati ya Miss Tabora 2013 kwa kubadilishana mawazo mawili matatu na kamati hiyo.

Kushoto;Pili Issa, Aloyson Mlawa, John Myuzik na Danny Kijumbe.

Playstation mpya inauzwa!

Playstation  mpya XBOX 360 60gb nyeupe ina controller 1, inauzwa, ipo katika box lake, atakayenunua atapata game moja buure! kwa bei na maelezo zaidi mpigie simu Alvin 0687232973.