MTOTO AWAKIMBIA WAZAZI WAKE JIJINI DAR ES SALAAM KUKWEPA KUKEKETWA
Kamanda wa Polisi Ilala, Salum Hamdun |
Na Dotto Mwaibale
MTOTO mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kivule Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam jina lake linahifadhiwa ameelezea jinsi alivyofanikiwa kuwatoroka wazazi wake ili asikeketwe.
Mtoto huyo hivi sasa analelewa na msamaria mwema baada kufungua kesi Kituo cha Polisi cha Stakishari Ukonga kufuatia kufikishwa kituoni hapo kwa ajili ya kujisalimisha na kuelezea madhila aliyotaka kufanyiwa.
Wakati mtoto huyo akijisalimisha katika kituo hicho kuna taarifa za ndani kuwa kuna mpango wa kuwakeketa watoto 85 wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 15 katika manispaa hiyo ambapo watoto zaidi ya 30 wanadaiwa kukeketwa.
Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com mtoto huyo alisema hawezi kurudi tena nyumbani kwao kwa kuhofia kupigwa na kukeketwa ambapo ameomba msaada wa hifadhi kutoka kwa watanzania.
"Baada ya baba yangu kufariki nyumbani kwetu Tarime tulikuja na mama hapa Dar es Salaam kwa kaka yake Chacha Nyanchiri anayeishi Kitunda Kivule karibu na Shule ya Msingi Misitu" alisema mtoto huyo.
Alisema katikati ya wiki iliyopita alifika bibi yake mzaa baba yake aliyemtaja kwa jina la Boke na kuwaambia yeye na wenzake wajiandaa kwenda kukeketwa.
Mtoto huyo alisema kwamba siku ya alhamisi majira ya saa mbili usiku wakiwa nyumbani kwa mjomba wao anakoishi na mama yake alifika bibi mzaa mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Debora huku akiwa ameongozana na mama yake Happyness na kuwaambia yeye na watoto wengine wawili wa mama yake mkubwa wakaoge ili waende kukeketwa.
Alisema ili kukwepa kukeketwa alipokwenda bafuni alifanikiwa kutoka na kupita njia nyingine na kufanikiwa kuwatoroka wazazi wake na kwenda kujificha kwenye pagala na ilipofika saa tatu usiku alifika eneo la kwa Mpemba akielekea darajani ambapo alikutana na dada mmoja aliyemsimulia mkasa huo.
Alisema dada huyo alimchukua hadi nyumbani kwake ambako alilala na siku iliyofuata alimpeleka kituo cha Polisi cha Stakishari kwa ajili ya usalama wake.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye alikataa kutaja jina lake alisema kuna mpango wa kuwakeketa watoto 85 kabla ya kuisha kwa mwaka huu wa 2016 na kuwa karibu watoto 30 wamekwisha keketwa.
Alisema shughuli hiyo inasimamiwa na wazee wa kimila wa kabila la kikurya na kuwa ngariba mkuu wa kazi hiyo ya kukeketa watoto hao yupo eneo la Nyamuhanga na kuwa baada ya kukeketwa ufanyiwa sherehe kwa siri katika baadhi ya nyumba zilizopo jirani na ngariba huyo.
Mwenyekiti wa Serikali wa mtaa anaoishi mtoto huyo, Dominick Mlimi alisema hana taarifa ya mtoto huyo kutoweka nyumbani kwao.
"Jana niliwaona baadhi ya watoto wa kike wa familia ya Nyanchiri wakiwa hapo barabarani lakini kuhusu kutoweka kwa mtoto huyo kwa kuhifia kukeketwa sijazipata" alisema Mlimi.
Mke wa Chacha Nyanchiri ambaye anaishi na mtoto huyo Regina Wilison alikiri mtoto huyo kuondoka usiku baada ya kufika nyumbani hapo bibi yake na mama yake ingawa alisema hawakutoa taarifa kwa mtu yeyote ya kutoweka kwake.
"Mwenye mamlaka ya mtoto huyo ni mama yake ambaye ametoka asubuhi kwenda kumtafuta mtaani mimi sihusiki naye na wala sijui walichomuambia ingawa siku zote tulipokuwa tukizungumzia kuhusu kukeketwa mtoto huyo alikuwa akionesha hofu" alisema Wilison.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun alisema hakuwa na taarifa kuhusu tukio hilo ingawa aliahidi kuwasiliana na wasaidizi wake ili kulifuatilia na kutoa taarifa kamili.
Mtoto huo alisema watoto wenzake waliofanyiwa vitendo hivyo bado wapo majumbani mwao wakijiuguza majeraha na kama vyombo vya usalama vitahitaji kwenda kuwaonyesha walipo yupo tayari.
Taarifa ambazo tumezipata jana kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mtoto huyo na mama yake zimeeleza kuwa polisi walifika katika nyumba hiyo na kumkamata Regina Wilson, mama ya mtoto huyo Happyness na watu wengine wawili na kupelekwa kituo cha polisi Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.
SUALA LA UKEKETAJI MKOANI MARA BADO NI PASUA KICHWA.
>
Baadhi ya wasichana wakitoka kukeketwa wilayani Tarime mkoani Mara, kumbuka mwezi Disemba, kila baada ya miaka miwili, ni msimu wa ukeketaji na tohara kwa baadhi ya Koo za Wakurya
BMGHabari
Pamoja na juhudi za Serikali, Wanaharakati na Watetezi wa haki za binadamu (Wanawake na Wasichana) katika kuhakikisha kwamba suala la ukeketaji linatokomezwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Mara na Arusha, bado suala hilo ni pasua kichwa kwani linafanyika, iwe kwa uwazi ama usiri.
Mtandao wa Binagi Media Group umeshuhudia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Tarime wakisherehekea msimu huu wa ukeketaji (Mwezi Disemba kwa baadhi ya koo, ikiwemo Watimbaru) ambapo wasichana wadogo wanafanyiwa ukeketaji.
Shamra shamra zinafanyika hadharani licha ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, kuonya kwamba yeyote atakayebainika kujihusisha na ukeketaji atachukuliwa hatua za kisheria.
Baadhi huamini kwamba msichana akikeketwa huleta heshima kwake na kwa familia na huwa tayari kwa ajili ya kuolewa na hivyo kuwapatia wazazi mahari (ng'ombe). Hatua hii husababisha baadhi ya mabinti kukosa fursa ya kuhitimu masomo yako na kujikuta wakiolewa, Aidha kwa kupenda ama kulazimishwa na wazazi/walezi wao. Suala la unyanyapaa miongoni mwa wasichana waliokeketwa na ambayo hawajakeketwa ni jambo ambalo pia huongeza msukumo wa wasichana kutaka kukeketwa. Mbaya zaidi, unyanyapaa huo huenda hadi kwa baadhi ya wanaume kukataa kuwaoa wale ambao hawajakeketwa na hivyo kusababisha ugumu wa kutokomeza suala hilo.
Tayari Ngariba mmoja aitwaye Angelina ppCharles (50) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezaji kwa kosa la kumfanyia ukeketaji mmoja wa wasichana wilayani humo huku wengine wawili wakidaiwa kukabiliwa na kesi ya aina hiyo. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Mhe.Martha Mpaze.
Wakati hayo yakiendelea, zipo kauli mbalimbali wilayani Tarime kwamba hivi sasa wasichana hawakeketwi kama zamani bali wakifika eneo la tukio hupakwa unga kwenye uso na maumbile yao na kufanyiwa matambiko ya kimila na shughuli huishia hapo na kinachofuata ni shamra shamra za kucheza ngoma ya ritungu na kurejea nyumbani.
Hata hivyo utafiti uliofanywa mwishoni mwa mwaka jana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na idadi ya watu duniani, UNFPA, kwenye mikoa 13 nchini ikiwemo Mara, umebaini kwamba katika maeneo mengi nchini, wanajamii wanazo mbinu mpya za kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kukumbatia mila potofu ikiwemo ukeketaji. Utafiti huo ulibaini kuwa, suala la kuwapaka unga usoni wasichana wilayani Tarime ni kuuficha tu ukweli kwamba wasichana hao hawakeketwi wakati ukweli ni kwamba hukeketwa.
Itoshe tu kusema kwamba, elimu zaidi inahitajika ili kuwanusuru wasichana wanaotoka kwenye makabila yanayojihusisha na ukeketaji kwani madhara yake ni makubwa ikiwemo kupoteza damu nyingi, kupata madhara kabla na baada ya kujifungua, kupoteza uwezo wa kufurahia tendo la ndoa, uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa ikiwemo Virus vya Ukimwi na wakati mwingine kupoteza maisha.
Inaelezwa kwamba msichana anayekeketwa hulipia kiasi cha shilingi elfu 35 hadi 40 ambapo wazee wa kimila hugawana pesa hiyo na mangariba hivyo inawezekana suala hili linakuwa na ugumu kutokomezwa maana ni sehemu ya ujira kwa wazee na mangariba hao.
Inadhaniwa kwamba zaidi ya wasichana 3,000 kwa Koo moja ya kabila la Wakurya hukeketwa kwa kila msimu. Kabila la Wakurya lina Koo 13.
Wakazi wa Wilaya ya Tarime wanasema, msukumo wa ukeketaji umepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Wanasema suala la elimu juu ya madhara ya ukeketaji pamoja na mwingiliano wa makabila mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa wa Mara, umesaidia japo kwa kiasi kidogo kupunguza ari ya ukeketaji.
Kataa Ukeketaji, haina umuhimu kufurahia mila na tamaduni zenye athari katika jamii. Vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuwakama na kuwafungulia mashtaka.
Wakati haya yanaendelea, zaidi ya wasichana 250 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mara na Arusha, wamehifadhiwa katika kituo cha kuwahifadhi wasichana waliokimbia ukeketaji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime.
BMG inaamini kwamba, Imani humalizwa kwa Imani. Suala la Ukeketaji ni Imani hivyo itolewe elimu yenye uhusiano wa kiimani ikiwemo maandiko matakatifu (dini) hatua ambayo itasaidia kuwanusuru wasichana wengi na suala hilo la ukeketaji.
Amana Bank FC yaichabanga Dar community bank mabao 8-1!
Kikosi cha Amana FC ikiwa tayari kwa mchezo hapo juzi. |
Timu ya mpira wa miguu ya Amana Bank FC juzi iliichabanga timu ya Dar Community Bank mabao 8-1 katika mchezo wa mashindano ya mabenki yanayoendelea katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Amana Fc iliutawala kwa vipindi vyote viwili, ikiongozwa na nahodha wao Muhsin Mohmed aliyefunga magoli matatu, huku kiungo mchezeshaji wa timu hiyo machachari Ally Khamisi akiifungia mabao matatu pia kabla Anthony Mahimbali na Ally Abdul wakihitimisha karamu hiyo ya magoli.
Awali Amana Fc ilicheza na Access Bank Fc katika mcheko mkali na wa kusismua ambapo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao mawili kwa mawili, matokeo hayo yameifanya Amana Fc kuongoza msimamo wa ligi hiyo ya mabenki ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu ikiwa na pointi 7 na magoli 13. Amana Fc ipo katika kundi B ambalo lina timu za Mkombozi Fc, Access bank na wenyewe Amana Fc.
Amana Fc imejikuta ikiingia robo fainali ya mashindano hayo baada ya kupewa ushindi wa pointi 3 na magoli matatu baada ya timu ya Mkombozi kutotokea uwanjani hivyo wakazawadiwa ushindi wa chee. Akiongea na mtandao huu meneja masoko wa benki hiyo Juma Msabaha Jr amesema vijana wao wapo vizuri na wana matarajio mazuri kushinda mechi yao ya robo fainali ambayo itachezwa baadae wiki hii katika uwanja wa Karume jijini Dar.
Mkurugenzi wa Amana bank afunga wiki ya huduma kwa wateja tawi la Mwanza!
Mkurugenzi wa benki ya Amana Dk Muhsin Masoud akimkabidhi zawadi mteja Yasmin Ismail Mussa kwa utunzaji bora wa fedha katika tawi la Mwanza.
Benki ya Amana leo hii imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo katika tawi la Mwanza mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud alitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wenye sifa tofauti tofauti kama ioneshavyo pichani.
Mkurugenzi huyo alikutana na wateja mbali mbali tawini hapo ili kubadilishana nao mawazo na pia kupokea maoni toka kwao katika kuboresha huduma kwa wateja wa benki hiyo pekee ya Ki Islamu nchini.
Kilele hicho cha wiki ya huduma kwa wateja kimefanyika katika matawi yote ya benki hiyo ambayo kwa Dar es Salaam ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na Main, vile vile Arusha na Mwanza.
|
Mkurugenzi wa Amana Bank Dk Muhsin Masoud akimzawadia Bw Juma Kivuruga kwa kuwa mfanyakazi bora kwa tawi la Mwanza, Kivuruga alipigiwa kura na wafanyakazi wenziye wa tawi hilo. |
Daud Lweno akizawadiwa na Mkurugenzi wa Amana Bank kama mteja mzuri kulipia miamala ya TRA katika tawi la Mwanza. |
Mteja Yasmin Ismail akikata keki ya kuadhimisha miaka minne tangu kufunguliwa kwa benki hiyo, huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao wakifuatilia tukio hilo kwa umakini. |
Bw Juma Msabaha meneja huduma kwa wateja wa Amana bank akijibu baadhi ya maswali kuhusu benki hiyo toka kwa waandishi wa habari. |
Meneja wa tawi la Mwanza Saleh Awadh akiongea na mteja wa benki hiyo. |
Hawa Maftah wa Amana Bank akimhudumia mteja mapema leo katika tawi. |
Mkurugenzi Dk Muhsin Masoud akiongea na mmoja wa mamia ya wateja aliokutana nao leo katika tawi la jijini Mwanza ambako alikuja rasmi kwa shughuli ya ufungaji wa wiki ya huduma kwa wateja. |
Picha ya pamoja wafanyakazi wa benki hiyo na mkurugenzi wao. |
Zainab Barker ambaye ni meneja huduma kwa wateja wa tawi la Mwanza. |
Ibtisam Akrabi akimhudumia mteja katika tawi la Mwanza. |
Mahmoud Maimu akimhudumia mteja. |
Benki ya Amana yazindua wiki ya huduma kwa wateja baada ya kutimiza miaka minne!
Mteja wa muda mrefu wa bemki ya Amana Bw Masoud Khalfan ambaye akizindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Main la benki ya Amana jijini Dar ka kukata utepe. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud, Kulia ni mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mohamed Mussa, kushoto ni mteja wa siku nyingi wa benki hiyo Bw Dossa. |
Mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mussa kushoto akiwa na mkuu wa kitengo cha fedha Bw Fahad Hamid siku ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. |
Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Amana Bank imeadhimisha miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24 Novemba 2011. Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi siku ya jumatatu wote walikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi yetu yote ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.
Meneja wa tawi la Main Bi Aisha Awadh akimwelekeza kitu mteja wa benki mama Sangawe. |
Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7 Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na za kisasa. Amana Bank mpaka sasa ina matawi saba ambapo manne yapo jijini Dar nayo ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na main ambapo ndipo makao makuu ya benki hiyo ya aina yake nchini.
Mfanyakazi wa benki ya Amana (Kushoto) akiwahudumia wateja kwa viburudisho katika siku ya wiki ya huduma kwa wateja wiki hii. |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidi. Tunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.
Mtoa huduma kwa wateja Bi Zainab wa tawi la Mwanza akimhudumia kwa viburudisho mteja wa benki hiyo. |
Mteja huyu akijipatia huduma katika tawi la Mwanza |
Huduma kwa wateja. |
Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya 27/11/2015, kwa hafla ya kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank ambapo mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud atakuwa katika tawi la jijini Mwanza mjini kukutana na wateja na kupokea maoni na ushauri wa kila aina utakaotolewa na wateja wao.
Baadhi ya wateja wakijipatia huduma katika benki ya Amana tawi la jijni Arusha. |
Huduma kwa wateja zikiendelea jijini Arusha. |
INTRODUCING NEW MOVIE ; MAISHA NI SIASA
MAISHA NI SIASA is a political film that tells a story of sacrifice, patriotism, loyalty, heroism, challenges and the role that bloggers and social media activists play in post independent African politics and ongoing democratization process. Produced by 24Hrs Media, The 7thElement & Kileleni Production, Directed by Shahid Ansari, the movie is casted by Paul Mashauri, Loue Kifanga, Bahati Chando, Violet Mushi, Godwin Gondwe, Carl Bosser, Hudson Kamoga Zenno kahumba and others.
Maisha ni Siasa will be launched at Century Cinemax, Mlimani City on Wednesday 14 th October 2015 from 6:30 PM featuring the Red Carpet Experience and Cocktail Function with casts and crew members. About 1,000 guests will attend the launch including seasoned leaders, members of political parties, journalists, bloggers, activists, corporate executives, entrepreneurs and friends of movies.
To preview the teaser, TV interviews, cast list and their profiles and to know more about the launchplease visit our website at www.maishanisiasa.co.tz, our facebook page at www.facebook.com/maishanisiasa and or our youtube channel
DC PAUL MAKONDA AONGOZA MATEMBEZI YA VYAMA VYA SIASA KUOMBEA NCHI AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akihutubia wananchi baada ya kupokea matembezi ya amani ya vyama vya siasa yaliyofanyika kuanzia eneo la Magomeni hadi viwanja vya Kinondoni Biafra Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Chama cha Union For Multi Party Democratic (UMD), Abdallah Tumbo akihutubia katika mkutano huo.
Katibu wa Wilaya ya Kinondoni wa Chama cha UDP, Makoye Ikoles, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha UPDD, Salim Choya akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Athuman Shesha akihutubia katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani wa dini zote Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, akiongoza dua za kuombea nchi amani katika mkutano huo.
Dua la kuombea taifa ikiendelea.
Vijana wa Jogging wakishiriki matembezi hayo.
Matembezi yakiendelea.
DC Makonda (katikati), akiwa na Viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki maandamano hayo.
Vijana wa Jogging wakiwa jukwaa kuu wakiimba wimbo maalumu wa amani.
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema kila mtu ana wajibu wa kuilinda na kudumisha amani iliyodumishwa na waasisi wa nchi hii hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Makonda alitoa mwito huo wakati akihutubia wananchi baada ya kupokea matembezi ya kuombea nchi amani yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra Dar es Salaam leo.
Maandamano hayo yameratibiwa na Makonda katika wilaya yake kwa niaba ya watanzania wote.
Makonda alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizodumu kwa amani na amani hiyo ilidumishwa na waasisi wa Taifa hivyo imebaki kuwa kimbilio na tegemeo kwa watanzania.
Alisema ili kuwaenzi waasisi hao ni kutunza tunu hiyo na kwamba yapo mataifa yamepita katika nyakati mbalimbali za uchaguzi lakini hawana amani kama tuliyonayo hivyo tuna wajibu mkubwa kuitunza.
"Vipo viashiria vya uvunjifu wa amani, lakini ikumbukw kuwa amani ni kubwa kuliko ahadi za mgombea yoyote wa chama cha siasa hivyo hakuna kinachoweza kufanywa na mgombea yeyote kama hakuna amani,"alisema.
Hata hivyo Makonda alisema kuwa aliandika barua kwa kila chama cha siasa ambapo vyote vilithibitisha kushiriki lakini cha kushangaza baadhi havijahudhuria kwa kutoa sababu zisizo na msingi wowote kama kutokuwa na nauli na mambo mengine.
"Niliviandikia barua vyama vyote, lakini vingine havijahudhuria kwa makusudi hivyo dalili mnayoona hapa ni dalili tosha kuwa amani wanayohubiri kwenye majukwaa si hii wanayoitaka,"alisema Makonda.
Makonda aliongeza kuwa vyama vilivyoshiriki katika maandamano hayo ya amani ni CCM, CUF, UPDP, UDP,UMD, Jahazi asilia na vilabu vya Jogging .
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum alisema mtu yeyote asiyependa amani ni adui wa Mungu.
Sheikh Alhad aliitoa kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam leo wakati alipoongoza dua maalum ya kuombea amani wakati wa maandamano ya vyama vya siasa yaliyofanyika kuanzia eneo la Magomeni hadi viwanja vya Kinondoni Biafra.
Alisema kuwa anavipongeza vyama vilivyothibitisha kushiriki maandamano hayo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Konondoni, Paul Makonda na kamati ya ulinzi kwa kuandaa shughuli hiyo.
Alisema kuwa kuna baadhi ya vyama ambavyo vilitakiwa kushiriki lakini havijashiriki ambapo havijaathiri chochote na kuweka wazi kuwa wachache wanaweza kufanya mambo kwa ajili ya wengi.
"Kuna baadhi ya vyama havijashiriki maandamano haya, hivyo vikumbuke kuwa watu wachache wanaweza kufanya mambo kwa ajili ya wengi hivyo ni jambo kubwa na kwamba mungu analisikia,"alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi na wawalikishi wa vyama hivyo walisema kuwa watanzania wanapaswa kupiga kura kwa amani pia walishamaliza wakatulie nyumbani kusubiri matokeo kutoka kwa mawakala wanaowaamini waliowaweka vituoni.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)